Tuwakumbuke wazazi wetu bila kujali walipo au sisi tulipo

lugoda12

Senior Member
Jul 28, 2018
160
337
Tuwakumbuke wazazi wetu bila kujali walipo au sisi tulipo. 👌

Mzee alipeleka simu yake kwa fundi ikatengenezwe, Fundi akamwambia mzee mbona simu yako hii sio mbovu kabisa, Mzee akamuuliza fundi kama sio mbovu kwanini sasa watoto wangu hawanipigii. 🥲 Tuwapigieni wazazi wetu walau mara mbili kwa wiki.
 
Asante sana ndugu yangu kwa ujumbe mwanana ila na hao wazee wajifunze kuishi vema na watoto wao wangali wana nguvu za kutafuta.

Kutelekeza watoto ujanani kisha kutegemea waje kukujali uzeeni kwa kutegemea vitisho vya taasisi ya dini eti utakosa radhi ya baba/mama ilhali hukuwaomba wakuzae, hiyo imepitwa na wakati. People no longer fear religious threats.

Kila mmoja should play his part accordingly so we could avoid these unnecessary blames and name calling.
 
Mzazi ni mzazi bila yeye usingekuwepo.
Nisingekuwepo ningepungukiwa nini? Tena Africa, bara lililojaa kila aina ya laana?

Wazazi watimize wajibu wao, laa sivyo acheni kuzaa kama hamuwezi kutunza watoto.

Ninakaa uswahilini ninaona mengi sana. Unaona mtu anazaa mtoto kwa sababu wenzake wanamwambia umri unaenda, cha ajabu la kumpa huyo mtoto hana.

Mtoto (single mother) naye anazaa mtoto.
 
Nisingekuwepo ningepungukiwa nini? Tena Africa, bara lililojaa kila aina ya laana?

Wazazi watimize wajibu wao, laa sivyo acheni kuzaa kama hamuwezi kutunza watoto.
Sometimes unaweza kukua ukakuta umepandikizwa sumu dhidi ya mzazi mmoja ukadhani ni kweli, ulipaswa kujua hapo awali kabla mmoja hajaacha kutekeleza majukumu yake ni nini kilitokea? Pengine alisalitiwa, au aliambiwa mtoto si wake, japo ni wake? Tusihukumu bila kupata ukweli wa pande zote.
 
Ninakaa uswahilini ninaona mengi. Hali inatisha sana.
 
Asante sana ndugu yangu kwa ujumbe mwanana ila na hao wazee wajifunze kuishi vema na watoto wao wangali wana nguvu za kutafuta.

Kutelekeza watoto ujanani kisha kutegemea waje kukujali uzeeni kwa kutegemea vitisho vya taasisi ya dini eti utakosa radhi ya baba/mama ilhali hukuwaomba wakuzae, hiyo imepitwa na wakati. People no longer fear religious threats.

Kila mmoja should play his part accordingly so we could avoid these unnecessary blames and name calling.

Kweli wazazi wanaweza kuwa walikosea ila rudisha hatua nyuma kidogo tu kama hawakupendi mbona walikulea hata kama kwa kiasi kidogo.simama na asili yako ambayo ni wazazi wako.Ungekuwa wapi wangekutoa ungali mimba? wao pia wanajuta kuto wajibika kwao juu yako. Samehe ichukue kama funzo kwa wanao walee kwa upendo kadri ya uwezo wako. Ukiiendekeza hiyo laana itakumaliza hata wewe ,kuwa mchora mstari sema baba alikosea nimesamehe sitaki hili lije kutokea kwa wanangu na vizazi vyao na Mungu atakuinua.
 
Kweli wazazi wanaweza kuwa walikosea ila rudisha hatua nyuma kidogo tu kama hawakupendi mbona walikulea hata kama kwa kiasi kidogo.simama na asili yako ambayo ni wazazi wako.Ungekuwa wapi wangekutoa ungali mimba?
Ningetolewa nikiwa mimba, maana yake ni kwamba nisingezaliwa Africa, bara la hovyo kuliko yote hapa duniani. Ninajutia kuwa muafrika.
 
Kwa akili hii hata ungezaliwa ulaya hakuna kitu ungefanya,Afrika hii hii watu wanajenga,hii afrika watu wanamiliki ukwasi mkubwa.ulaya wengi ni wapangaji.
 
Asante sana ndugu yangu kwa ujumbe mwanana ila na hao wazee wajifunze kuishi vema na watoto wao wangali wana nguvu za kutafuta.

Kutelekeza watoto ujanani kisha kutegemea waje kukujali uzeeni kwa kutegemea vitisho vya taasisi ya dini eti utakosa radhi ya baba/mama ilhali hukuwaomba wakuzae, hiyo imepitwa na wakati. People no longer fear religious threats.

Kila mmoja should play his part accordingly so we could avoid these unnecessary blames and name calling.
Sio dini wala tamaduni ila mfumo walotulea wazazi wetu ni mfumo wa kijamaa zaidi yaan mfumo wa kutafuta maisha ya kileo ya kukuza watoto bila kujiwekea akiba ili siku hawana nguvu ziwasaidie.
Wengine waliuza mifugo na mazao ili twende shule au kuhudumia sisi hivyo tunapofanikiwa tusikate mizizi yao.

Ila kizazi chetu ndo tunapaswa kujiandaa na mfumo wa ki bepari mfumo wa kivyo vyako, tusizae watoto wengi na tusiache kujiwekea akiba za uzee na miradi ambayo itafanya kazi angali hatuna nguvu.

Hivyo wazazi wetu tusiwatenge hawakujiandaa na tunachojidai sisi kuwa kila mtu na maisha yake.

Mjini tunakoishi tunavuja hela sanaa tunasahau wazazi vijijini wakiteseka

Elfu kumi kwa wazazi wetu wa kijijini ni kubwa mnoo.
 
Back
Top Bottom