Tuwakatae Wahuni Wote

Tuwakatae Wahuni Wote

ERTUGRUL BEY

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
11,529
Reaction score
21,530
file_0000000055ec71fd87ea5b2484893222 (1).png

My people,​

Kwa kila mwanaharakati ambaye anaikosoa Serikali hakika anajua matokeo au madhara ambayo atakutana nayo leo au kesho

Ndio maana comrade Pole pole alijua na alikuwa tayar kulipia gharama hiyo ,kuonyesha kwamba alikuwa tayari kwa lolote litakalo mkuta akaamua kubakia hapa hapa hali akijua usalama wake hauko asilimia Mia moja,na kweli kilichotokea wote tunakijua

Nini nataka kusema hapa, mwanaharakati yoyote yule awe ndani ya nchi au nje ya nchi basi vita yake na Serikali isimfanye mwananchi wa kawaida akashindwa kuendesha maisha yake ya kila siku,akashindwa kujifanyia shughuli zake za kiuchumi ambazo zinamfanya apate mkate wake wa kila siku na familia yake

Wanaharakati wengi tena hawa waliopata hifadhi nchi jirani au kwengine kokote kule,wao wanafadhiliwa na maisha yao yanaendelea kama kawaida,lakini wanataka sisi tuache shughuli zetu za kutuingizia kipato na kucheza nyimbo zao kuikomboa nchi kwa njia ambayo sio salama na kuyaweka maisha yetu rehani.

Wanatanzania hakuna shujaa kwenye kuhatarisha maisha yako,kudhibitisha hili ndio maana wao wapo huko nyuma ya keyboard kazi yao ni kutuhamasisha kuhatarisha amani ya nchi yetu pendwa Tanzania

Wao wanathamini uhai wao ndio maana wamekimbia nchi hii kulinda uhai wao,lakini wanataka sisi kuweka uhai wetu mashakani,hapana inatosha sasa,tuseme hapana kwa hawa Wanaharakati,kama kweli wana mapenzi na sisi waje hapa Tanzania na wawe front line tuandamane pamoja,tupigwe virungu pamoja,tupigwe risasi pamoja na tuwekwe selo pamoja

Gen Z you have got a lot of life a head of you,una ndoto nyingi za kutimiza lakini usikubali kuwaste your life In the name of kuikomboa Tanganyika, hatuna nchi inaitwa Tanganyika bali tuna nchi inaitwa Tanzania,kwahiyo usipiganie kitu ambacho hakipo now, bali pigania Amani ya Tanzania ambayo ndio urithi wetu

Amani ndio tunu au zawadi muhimu ambayo kila mtanzania anatakiwa kuilinda kwa wivu mkubwa sana,yoyote ambaye kwa namna moja au nyingine anataka kuhatarisha Amani yetu huyo ni adui yetu mkubwa ama awe kiongozi wa Serikali,Dini au kikundi chochote cha watu,tuseme hapana kwa watu hawa,hawana nia nzuri na Taifa letu

Ungana na Team Amani kupambana bila kuchoka na waovu na wahuni wote ambao hawana nia njema na TANZANIA YETU

Tutaelewana tu mdogo mdogo

Ni hayo tu!!
 
Mkuu anayevuruga amani ni serikali, hiki kinachotokea sasa hivi ni matokeo sio chanzo. Mzigo ambao wananchi wanalazimika kuubeba ili kulinda hiyo amani ya Tanzania ni mkubwa mno.
Sawa serikali imeharibu amani,je na sisi tuendelee kuiharibu au walau tujitahidi kurekebisha ili walau mambo yasiharibike sana
 
Njia ipi ya kurekebisha mkuu? Mfano utekaji ulianza wakati wa Magufuli watu walikuwa wakiupigia kelele ila hadi sasa ndio unazidi badala ya kupungua, sasa hivi imekuwa kama mchezo tu. Sasa niambie sie wananchi kipi tunachoweza kufanya maana sasa hata kuukemea tu pia tunaogopa.

Kwahiyo ili tuendelee kuonekana Tanzania ni nchi ya amani inabidi tu kukubali jambo kama hilo la utekaji ambalo kadri muda unavyozidi kwenda nalo linazidi.
 
Ni sahihi kabisa umeanza zamani na sasa unashamiri

Kwa mazingira haya je mwananchi afanyeje?

My upinion since wanaotekwa ni wale tu ambao wanaikosoa serikali basi ili uwe salama kaa mbali na harakati zitakazo kuletea madhara,iko hivyo

Kinyume na hapo umejiweka rehani wewe mwenyewe na hakuna wa kumlaumu

Maoni yangu yanaweza yasikubaliwe na wengi and which is fine lakini ndio njia salama kwa sasa
 
Hivi ulipitaje kwenye usahili wewe? Mi nilifikiri mliolipwa wote kuja kuisafisha serikali yenu haramu huku kwenye mitandao mna uwezo mzuri wa kujenga hoja?
Hilo sio tatizo langu ni mtazamo wako,kama ningesema linalokupendeza usinge sema haya

Swala hapa ni amani yetu ndio tunu yetu tuilinde kwa wivu mkubwa sana
 
Msingi wa Amani ni haki huwezi kutenganisha hilo hakuna amani bila na haki

Ukazingatia haki amani huja bila kutumia nguvu
 
Amani kwenu ni kuteka na kupoteza watu sio?

Serikali gani msiyotaka ukosoaji?
Si kila ambaye anawaza tofauti na nyinyi yupo upande wa serikali

Mimi ni mwananchi wa kawaida ambaye siyaendei mambo kwakuwa majority wanaamini hivyo ila naliendea jambo kwakuwa ni sahihi na salama kwa wakati husika
 
Maajabu kweli! mleta mada anasema tanganyika haipo ila zanzibar ipo, yaani alivyo zwazwa anasahau kuwa nchi mbili zimeungana ndipo ikazaliwa tanzania! kumbe uko uvccm kuna mazwazwa namna hii?
 
Kwahiyo kwa sasa hivi ni sahihi kushikilia raia kwenye vituo vya polisi bila kuwapeleka mahakamani sio, ni sahihi kuua raia na kupoteza miili yao ndugu zao wasipate fulsa ya kuwazika sio?

Wananchi wameamua kukataa huo ujinga.
 
Ni sahihi kabisa umeanza zamani na sasa unashamiri

Kwa mazingira haya je mwananchi afanyeje?

My upinion since wanaotekwa ni wale tu ambao wanaikosoa serikali basi ili uwe salama kaa mbali na harakati zitakazo kuletea madhara,iko hivyo

Kinyume na hapo umejiweka rehani wewe mwenyewe na hakuna wa kumlaumu

Maoni yangu yanaweza yasikubaliwe na wengi and which is fine lakini ndio njia salama kwa sasa
Hicho ndio nachokisema kwamba moja ya mzigo mkubwa ambapo wanalazimika kubeba wananchi katika kulinda amani ya hii nchi.

Shida ni kwamba hilo suala ni gumu kuwezekana sio wote wataweza kufanya hivyo mkuu na hata kama endapo watu wote watafanya hivyo unadhani hali itakuaje kwamba kuwe hakuna ukosoaji kabisa serikali iwe na uhuru 100% wa kufanya lolote?

Kinachotokea sasa hivi ni baada ya watu kuvumilia na kuchoka, alipoingia Samia watu walikuwa na matumaini makubwa tena hawa hawa ambao unaona ni wanaharakati ambao wanataka kuvuruga nchi.
 
Duuh aisee mzee si unatengeneza bomu sasa.

Kama utekaji unafanywa kweli na serikali si hata watu wenye nia ovu watatumia mwanya huo kuteka watesi wao, ndio kama hali ilivyofika sasa.
Na sio kutekwa tu bali watu wanajiteka wenyewe kutengeneza drama kwasababu ishakua trend sasa.

Yaani unaona makosa, yasikemewe!! Kwa dunia ya sasa hilo sahau mkuu, utakua unampigia mbuzi gitaa na kudhani atacheza.
 
Nakubaliana na wewe kwamba ni kweli hali ya kisiasa si rafiki kwa sasa,je ni sahihi na wewe kuweka nafsi yako hatarini kwa sasa?

Kama huwezi kuwa na subira kwa yanayoendelea sasa basi fanya harakati for your own risk, ila usitegemee huruma za watanzania

Pole pole yupo wapi leo?

Tumeshamsahau au sio,basi na yeyote yule ambaye ataweka roho yake rehani tutamsikitia kwa muda then tutamsahau

Linda uhai wako na kiwiliwili chako
 
Ungeanza kwanza kukemea ufisadi, utekaji, na uonevu mwingine huo ndio umesababisha amani kutoweka

We unataka watu waonewe na wakae kimya tu kama mifugo, hata mifugo hua ina resist uonevu

Ngoja nimalize kwa kukutukana wewe ni coward na hapa unataka wote tuwe kama wewe
 
Duuh aisee mzee si unatengeneza bomu sasa.

Kama utekaji unafanywa kweli na serikali si hata watu wenye nia ovu watatumia mwanya huo kuteka watesi wao, ndio kama hali ilivyofika sasa.
Na sio kutekwa tu bali watu wanajiteka wenyewe kutengeneza drama kwasababu ishakua trend sasa.

Yaani unaona makosa, yasikemewe!! Kwa dunia ya sasa hilo sahau mkuu, utakua unampigia mbuzi gitaa na kudhani atacheza.
Binafsi sipendezwi na utekaji kabisa ila sasa nitafanyeje,unafikir sitamani kuandika dhidi ya serikali?

Ila navalue my life zaidi I have got my family to take care,wanasema kunguru muoga huficha mbawa zake

Pinga serikali kwa utashi wako na ukipatwa na lolote usimlaumu mtu
 
Ungeanza kwanza kukemea ufisadi, utekaji, na uonevu mwingine huo ndio umesababisha amani kutoweka

We unataka watu waonewe na wakae kimya tu kama mifugo, hata mifugo hua ina resist uonevu

Ngoja nimalize kwa kukutukana wewe ni coward na hapa unataka wote tuwe kama wewe
Kuna njia nyingi salama za kudai haki lakini huwezi kufanya siasa za hatari etu uonekane jasiri huo ni ujinga,ndio maana wanaharakati wahuni wamekimbia nchini kwa kuhofia uhai wao,je wao sio waoga?

Think big
 
Maajabu kweli! mleta mada anasema tanganyika haipo ila zanzibar ipo, yaani alivyo zwazwa anasahau kuwa nchi mbili zimeungana ndipo ikazaliwa tanzania! kumbe uko uvccm kuna mazwazwa namna hii?
Unajitekenya halafu unacheka mwenyewe, leo tuna nchi inaitwa TANGANYIKA?
 
Back
Top Bottom