MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 12,695
- 31,487
Ashakuum si matusi, maskini akipata matako ulia mbwata, hizi ni moja ya kauli za wahenga wetu. Hakika nyingi ya kauli hizi zina mafunzo makuu lakini zipo kauli potofu na kengefu.
Aliye juu mngoje chini, hakika hii ni kauli kengefu, inayochochea uvivu, kwanini usichukue ngazi umfuate?
Aidha, mgaa gaa na upwa hali wali mkavu, hii hakika ni kauli potofu, inachochea uzururaji na kuzalisha ma-beach boys wanao zurura kwenye pwani zetu
Pamoja na hizo hapo juu, ipo hii matata sana, mficha uchi hazai, hii inachochea ukahaba, yaani mwanamke au mwanaume anashauriwa auanike uchi wake hadharani, seriously?
Nyingine ni ndondondo si chururu, hapa wahenga wanatuzingua, vitu visivyo fanana siku zote haviwezi kuwa sawa, ni kichagizo tu
Nyingine mbaya kabisa, inayotumiwa na wenzetu makolo, eti wamekufa kiume, kweli? kufa ni kufa tu, hakuna kufa ki-kike au ki-ume
Bila ya kupoteza muda, endelea kuchakata kauli/misemo kengefu na potofu ili tuwafokee wahenga wetu