SoC04 Tuwaandae watanzania kutoitegemea TANESCO

Tanzania Tuitakayo competition threads

cilla

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
372
298
TUWAANDAE WATANZANIA KUTOITEGEMEA TANESCO

UTANGULIZI

Nchi yetu imepitia katika matatizo ya mara kwa mara ya ukatikaji wa umeme na mgao wa umeme kwa nchi nzima takribani miaka 30 sasa.Kwa miaka hiyo 30 Serikali zote zimekuwa na ahadi zenye matumaini ya kutatua kabisa changamoto ya kukatika kwa umeme na kumaliza kabisa tatizo la mgao wa umeme nchini. Matatizo haya ya umeme yameendelea kuwepo na kuathiri maisha ya watanzania, katika ngazi ya familia, wafanya biashara, watoa huduma na wazalishaji bidhaa na kutishia uchumi wa nchi yetu.

Pamekuwa na sababu nyingi zinazotajwa na serikali kama sababu ya kukatika kwa umeme na mgao wa mara kwa mara . Kati ya sababu hizo ni upungufu wa umeme Unaozalishwa ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji,
upungufu wa maji au gesi katika vyanzo vya kufufua umeme,uchakavu wa miundo mbinu nakadhalika.

Serikali kwa upande wake tangu uhuru imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika.Wakati tunapata uhuru tulikuwa tunazalisha megawati 67 zilizokuwa zinatosheleza mahitaji ya nchi kwa wakati huo, lakini sasa tunazalishakaribu megawati 2,138 lengo ikiwa ni kufikia megawati 5000 ifikapo mwaka 2025 kwa mujibu wa kauli ya Waziri wa Nishati ya hivi karibuni.

Kwa nyakati tofauti serikali imebuni na kutekeleza miradi mbalimbali kwa lengo lakuongeza uzalishaji wa umeme nchini ,

Pamoja na mafanikio makubwa yatokanayo na jitihada za serikali na wadau wengine katika kuongeza uzalishaji umeme nchini , bado serikali haipaswi kuridhika kwa sasa kwa sababu mahitaji ya umeme yana ongezeka kila siku kwa haraka kuliko uwezo wetu wakuzalisha..Na hii inathibitishwa na kauli ya waziri mwenyewe wa nishati Wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2024/25 waziri Biteko alisema kuna ongezeko la asilimia 14 la uzalishaji umeme nchini tangu june mwaka 2023 hadi march 2024 Lakini ongezeko hili la asilimia 14 ni dogo ukilinganisha na kasi ya ongezeko la mahitaji ya umeme nchini.Hii ina maanisha bado tunahitaji ubunifu wa vyanzo vingi vya uzalishaji umeme.

Katika kuifikia Tanzania tuitakayo katika upande wa nishati nini kifanyike?


NI MUHIMU SERIKALI IKABORESHA SERA YA NISHATI YA MWAKA 2015 IENDANE NA DUNIA YA SASA NA MABADILIKO YA ULIMWENGU.
Kama tunavyofahamu Sera ni jumla ya mipango, uhamasishaji, miongozo na mikakati, ya nchi iliyojiwekea ya namna gani mnatakavyoenenda kufikia malengo kama nchi.Kwa maana nyingine Sera inaweza kuifananishwa na ramani au dira yakukufikisha mahali Fulani.Kama utakosea katika kuunda sera maana yake unaweza usifike kule unakohitaji kufika.

Katika kuifikia Tanzania tuitakayo ni muhimu serikali ikaboresha sera ya nishati ya taifa ya 2015,sekta ya nishati jadidifu na mpango mkuu wa mifumo ya nishati wa mwaka 2016.Sera hii ya nishati ya 2015 pamoja na mipango miongozo yake ililenga kuongeza uzalishaji umeme asilimia 50 ifikapo mwaka 2025 unaotokana na nishati jadidifu.

Sera hii pamoja na mazuri mengi lakini imesahau jambo moja kubwa katika dunia ya leo,
dunia ya leo nchi zinapambana kuhakikisha idadi kubwa ya kaya katika nchi zinakuwa na mfumo wake wa umeme maarufu kama residential rooftop solar panel kama sehemu yakuondoa utegemezi mkubwa wa umeme kutoka grid za umeme wa serikali katika nchi zao.Sera hii ya 2015 hauna dira, kanuni,muongozo wala uhamasishaji wa aina hii ya uzalishaji umemejua ujulikanao kama home/ residential rooftop solar panel.

Australia kwa sasa inaongoza kwa kuwa na asilimia 15 ya kaya zenye mfumo wa umemejua(rooftop solar panel). Kulingana na takwimu za Energy Supply Association of Australia (2016) zaidi ya nyumba 1 kati ya 7 inamfumo wa solar(umemejua) ikifuatiwa na Ubeligiji, ujerumani alafu Uingereza(UK).Nchi nyingine nazo hazijabaki nyuma mfano Marekani katika dira yake ya nishati ya mwaka 2020 imepanga kufikia mwaka 2030 angalau kaya 1 kati ya 7 ziwe zinaumeme wake wa solar(umemejua).Na kwa mujibu wa utafiti robo mwaka uliotolewa na SEIA linasema kati ya June na September 2022 kwa mara ya kwanza Marekani imerekodi zaidi ya megawati 1500 kupitia mpango wa umemejua majumbani(Residential solar systems).Kwa kufanya hivi serikali unakuwa imepunguza mzigo mzito wa utegemezi wa umeme inayozalisha.


Tuondoe dhana potofu iliyojengeka kwa watanzania kwamba umeme jua ni mahitaji ya watu waliokatika maeneo ya vijijini yasiyofikiwa na umeme wa Tanesco.Tuwafanye watanzania pamoja na kuwa na umeme unaozalishwa na serikali wawe na umeme mbadala utokanao na nishati ya jua.

Takwimu mbalimbali za nishati zinatuambia sehemu kubwa ya umeme wetu unatumika katika matumizi ya mwanga (taa) ,na vifaa vidogo vidogo vya ki electronics kama kuchaji simu,redio,Runinga nk.maana yake ni kwamba kama watanzania au taasisi zitaamua kuwa na umemejua(home/residential solar panel} kwenye paa za majengo yao watapunguza utegemezi mkubwa wa umeme kwa ajili ya mwanga kutoka tanesco.

Hivi karibuni UNDP nchini wametuonyesha mfano mzuri wa kuigwa kwakuweka mfumo wa umemejua katika ofisi zake Oster bay, Dar es salaam wenye uwezo wakuzalisha megawati 187 kwa mwaka.Pia
Ifakara Health Institute (IHI) walifunga solar panel kwenye moja ya majengo yake mwaka 2021 kama sehemu ya kujitosheleza kwa umeme.

Ni wakati sasa na sisi tuone umuhimu wa kuchochea watu binafsi,taasisi na serikali kuona umuhimu wa kuwa na mfumo wa umemejua katika paa(roof) za majengo yetu na hata paa za maeneo ya maegesho ya magari. .
Serikali iboreshe sera ya nishati ya taifa ya 2015, kwa ;-

1.serikali kutengeneza kanuni na miongozo mahususi ya kuhakikisha inahamasisha ujenzi wa majengo yenye mfumo wa umeme mbadala wa solar.

2.Kuhamasisha jamii kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa makazi au majengo tunayojenga kuweka mifumo ya umemejua(solar rooftop panel).

3.Kuhamasisha watanzania kwakuwaondolea kodi kwenye vifaa vya uzalishaji umeme wa solar na vifaa vinavyotumia umemejua(solar).


4.Ili kupunguza gharama za vifaa vya solar serikali ishawishi wawekezaji makampuni mbalimbali za solar kuja kuwekeza nchini.

KAMA SERA ITABORESHWA

1: Tutapunguza utegemezi mkubwa wa umeme kutoka kwenye grid ya taifa.Umeme wa tanesco ya taifa utatumika kwa watumiaji wakubwa wa umeme kama viwanda ,shughuli zinazohitaji umeme mkubwa kama mashine za kusaga, kuchomelea, watumiaji wa majiko ya umeme, majokovu n.k .

2; watanzania watakuwa wamepunguza kwa kiasi kikubwa bili za umeme za kila mwezi

3; Utaifanya grid ya taifa kutolemewa na ongezeko la watumiaji wa umeme.

4; Umemejua ni rafiki wa mazingira

5.itaongeza ajira .


TUSILENGE TU KUONGEZA VYANZO VYA UMEME PIA TUFIKIRIE NAMNA YA KUPUNGUZA WAHITAJI WA UMEME KWAKUWASAIDIA KUWA NA UMEME WAO.
 
Sera hii pamoja na mazuri mengi lakini imesahau jambo moja kubwa katika dunia ya leo, dunia ya leo nchi zinapambana kuhakikisha idadi kubwa ya kaya katika nchi zinakuwa na mfumo wake wa umeme maarufu kama residential rooftop solar panel kama sehemu yakuondoa utegemezi mkubwa wa umeme kutoka grid za umeme wa serikali katika nchi zao.Sera hii ya 2015 hauna dira, kanuni,muongozo wala uhamasishaji wa aina hii ya uzalishaji umemejua ujulikanao kama home/ residential rooftop solar panel.
Solar panel for every home kila kijieneo kiwe ni kizalishaji cha umeme.

Halafu kuna mfumo fulani kama ruzuku sijui kama inawezekana pia, ule wa kuwalipa wazalishaji binafsi kulingana na umeme anaouweka katika gridi ya taifa. Inaweza kuwa kwa kuzitumia uniti tena bure kipindi hazalishi.

Mfano mtubanayo mifumo ya upepo, wakati wa upepo mkali atazidiwa umeme, ume.e unaozidi unaingia kwenye gridi na atalipwa. Vivyo hivyo mtu mwenye solar kubwa wakati wa jua kali sana. Sijui kama bongo inawezekana. Na itashindikanaje kamankwingine imewezekana?
 
Solar panel for every home kila kijieneo kiwe ni kizalishaji cha umeme.

Halafu kuna mfumo fulani kama ruzuku sijui kama inawezekana pia, ule wa kuwalipa wazalishaji binafsi kulingana na umeme anaouweka katika gridi ya taifa. Inaweza kuwa kwa kuzitumia uniti tena bure kipindi hazalishi.

Mfano mtubanayo mifumo ya upepo, wakati wa upepo mkali atazidiwa umeme, ume.e unaozidi unaingia kwenye gridi na atalipwa. Vivyo hivyo mtu mwenye solar kubwa wakati wa jua kali sana. Sijui kama bongo inawezekana. Na itashindikanaje kamankwingine imewezekana?
kabisa aise naona kama tumechelewa
 
Back
Top Bottom