Tuupigie kura Mlima Kilimanjaro kwenye World Travel Awards 2017

maharage ya nazi

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
344
230
Kama maelekezo ya Tanzania Tourist board yanavyoeleza, tuipigie kura Mlima Kilimanjaro kwenye tuzo za "World Travel Awards 2017" mwisho wa kura ni mwezi wa nane mwaka huu. Wingi wa kura zetu ndio utakaoipa Mlima Kilimanjaro hatua za kushinda. Tukiweka Ml. Kilimanjaro kwenye medani ya ushindi ndivyo fursa za kitalii zitaweza kuinufaisha Tanzania yetu. Pia unaweza kupigia kura kampuni zingine za kitanzania katika shindano hilo.

World Travel Awards - Africa Nominees 2017
 
Si kweli kama kilimanjaro inafahamika kwa wote kama ni hot! Tusichoke kutangaza vivutio vyetu.
2016 In Africa Morocco watalii 10.4 milioni kwa mwaka
Afrika kusini 9.5 m, Misri 9.6m, Tunisia 6.5m, Zimbabwe 1.8m, Mozambique 1.8m,
Tanzania 1.3m. Bado tuko chini sana.

Hii haihusiani na serikali, tunapofanya jitihada ya kampeni ya kuleta watalii tunawasaidia watanzania makundi na mmojammoja kama wapagazi, waongozaji, madereva, wapishi, wachuuzi n.k katika kujipatia rizki.
 
Hata Zimbabwe wametushinda kwa idadi ya watalii mkuu!? Au watalii huwa wanenda kupiga picha na "Simba wa Afrika" Tata Komredi Jongwe Robert Mugabe!?
 
Vitu hatuhitaji vipigiwe kura

Unaanzaje kuupigia kura mlima kitu ambacho kiko in natural
Na ukipiga kura kitabadisha uhalisia wa kuwa mlima mrefu kuliko yote balani africa?
 
Zimbabwe watatushinda kwa sababu wanapigia debe victoria falls-zambezi river na wana mbuga za wanyama.
Utalii unaleta faida kwa wananchi si tu kwa serikali kwa sababu kila mtanzania atafaidika directly au indirectly--wakilipa kodi itanufaisha kwa serikali kuongeza huduma za kimaendeleo, pia wananchi wanapata riziki kwa kuuza bidhaa za vyakula, mbogamboga, bidhaa za utalii, n.k na wao wakipata kipato wanaenda kununua vingine kinachomsaidia mtanzania mwingine. Utalii ni ya pili kwa kuleta pato la taifa, inazidi hata madini.

Maliasili tulizokuwa nazo lazima zitufaidishe, tukisema natural attractions then tukabaki kujionyesha wenyewe hatutapata faida navyo.
Watanzania tuchangamke, tuwe warahisi kuitetea nchi yetu, wakenya ndio wanatushinda hivihivi, changamoto za serikali isitufanye kudharau kila tulichokuwa nacho
 
Si kweli kama kilimanjaro inafahamika kwa wote kama ni hot! Tusichoke kutangaza vivutio vyetu.
2016 In Africa Morocco watalii 10.4 milioni kwa mwaka
Afrika kusini 9.5 m, Misri 9.6m, Tunisia 6.5m, Zimbabwe 1.8m, Mozambique 1.8m,
Tanzania 1.3m. Bado tuko chini sana.

Hii haihusiani na serikali, tunapofanya jitihada ya kampeni ya kuleta watalii tunawasaidia watanzania makundi na mmojammoja kama wapagazi, waongozaji, madereva, wapishi, wachuuzi n.k katika kujipatia rizki.
Elekeza watu basi jinsi ya ku vote hapo,najua wengi watapata shida kama ilivyokuwa kwangu hatimaye mtu anaamua kuacha.Elezea baada ya kufungua hiyo link nini kifanyike.
 
Hivi kuna haja ya kuupigia kura mlima ambao no doubt ni maajabu ya dunia? Anyway, wanakata sh. Ngapi kwa kila sms nitakayotuma
 
Kupiga kura hauhitaji sms, ila kwa internet, ingia kwenye link hii
World Travel Awards - Africa Nominees 2017

Ujisajili na baada ya kujisajili, ingia kwenye bara la Africa na hapo tafuta kipengele cha destination upiga kura, africa's leading beach destination weka zanzibar, africa's leading national park weka serengeti nat park, africa'a leading tourist attractions weka mount kilimanjaro na kuendelea. Mfano huu hapa chini
20170421_112547.jpg
 
Francis Da Don, kweli Mlima Kilimanjaro ni Maajabu ya dunia ila wengi hawafahamu kuna mlima kilimanjaro na vivutio vingi Tanzania. Marekani unawauliza watu hata Tanzania hawaijui sasa itakuwa nchi zingine? Kivutio ni kukitangaza sio kujivunia chumbani
 
Back
Top Bottom