Moja ya watu wanaofanya kazi kubwa ktk kuirekebisha jamii ni KALAPINA lkn watu hawamuoni, kipindi chake kizuri lkn hakina wadhamini ila bado hajakata tamaa, huyo dogo nilimuona yy na mama yake ambaye alikuwa mwathirika wa madawa ila sasa anatumia methadone, inatia huruma sana pamoja na mazingira magumu aliyokulia huyu dogo bado form six kapiga II - 11 PCB (kwa wanaoijua shughuli ya PCB advance nadhani lazima watatoa salute kwa huyu dogo) na amechaguliwa SUA (Bsc in industrial engineering and management) ila mkopo hana (sijui bodi wanaangalia vigezo gani). Huyu anahitaji msaada sana, mimi mwenyewe nimeguswa ila uwezo sina, anatia huruma kama ingewezekana bodi wasikilize rufaa ya huyu kijana. Big up brother pina usichoke, kupitia ww watu wanajifunza mengi