Explainer
JF-Expert Member
- Dec 16, 2015
- 516
- 504
Si hoja ngeni machoni mwa wana JF.
Natanguliza shukrani za dhati kwa members wote wa JF, kwa umoja, uzalendo na mshikamano mzuri katika kuchangi hoja.
Kama kisemavyo kichwa cha hoja hii hapo juu, ndugu zangu tukianzia humu JF tujifunze kuukataa utumwa na ukoloni wa kileo unaotufanya tuendelee kushika chati katika orodha ya nchi maskini duniani na ikiwa ni moja wapo ya nchi chache duniani iliyobalikiwa rasilimali nyingi sana. Rasilimali watu tu, pekee inatosha kututoa katika umaskini, bila kujali hata dhahabu,Tanzanite ambayo inavunwa kwetu lakini nchi za mbali ndo wanaoongoza kwa mauzo yake, gesi, misitu, wanyama pori na vitu vingi naweza kuvitaja kwa siku nzima.
Inasikitisha tumekubali kuvigawa hivyo vyote kwa mataifa bila kutumia maarifa, na pia kwa kusikitisha zaidi tumeigawa hata rasilimali hadhimu ya utu wa mtanzania na sasa tungali watumwa wa wahindi, wachina, waturuki na jamii kubwa ya dunia hii ya leo. Tunaitwa majina ya kibaguzi, kunyanyaswa, kudhihakiwa na mambo milioni yanayoumiza tukiwa ndani ya nchi yetu,
ikiwa mwekezaji wa ndani yaani mtanzania halali na mwenye asili ya India anaajiri watu wengi kutoka nje ya nchi, tena wale wa asili yake na akiweka wazi ubaguzi katika nyanja zote. Wazawa tukibaki kuwa makuli na maskini wakubwa na haijalishi haka kama unakipaji na uwezo wa taaluma fulani, nafasi zote na mikataba bora na mishahara minono ni ya wageni tu wanakusanya na kujenga uchumi imara kwao. Kila kona kero za ubaguzi zimejaa zimejaaa na inatia uchungu sana kuendelea kuutumikia utumwa waliopitia babu zetu
Wana JF tukiwa kama chambo na msingi wa ujenzi wa taifa jipya huru chini ya MH:Rais wetu mpendwa tuwe mfano katika kuutanguliza uzalendo mbele kwa manufaa ya taifa letu zuri, tukidumisha amani yetu mshikamano na umoja. Mchango wa hoja yako ndio uzalendo wako katika kutetea maslahi ya Tanzania