Tutumie Michezo Kutangaza Utalii

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE COSATO CHUMI - TUTUMIE MICHEZO KUTANGAZA UTALII

"Wawindaji wazawa hawawezi kushindana na wawindaji Wakubwa, nashauri Wizara ya Maliasili na Utalii itenge 70% kwa ajili ya wawindaji wageni na 30% kwa ajili ya wawindaji wa ndani" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Nashauri tutumie michezo kutangaza utalii lakini pia kama taratibu za ikolojia zinaruhusu kwenye hifadhi zetu kuwepo na viwanja vidogo vya michezo ikiwemo vya mpira wa miguu, kikapu ili watalii wanapokuja kutalii pia wanapata nafasi ya kujiburudisha kwa michezo" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Tutumie michezo kutangaza utalii, mfano ukaamua kuwekeza kwa mwanariadha na ukamsaidia vifaa, kuweka kambi, mwanariadha huyu atakapokwenda kushiriki Bristol Marathon itakuwa ni mvuto kwa nchi yetu na itachochea kuvutia watalipa" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Misitu ni zaidi ya Mbao, kuna Milunda, Nguzo, Plywood, Utomvu unagemwa kwenye miti nk, ndio mana tunasema kwa pamoja mazao ya misitu yanachangia zaidi ya 3% katika pato la Taifa" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Kuna kufikisha umeme kwenye vitongoji 15 kila jimbo, tutahitaji nguzo, ni misitu. Ujenzi wa mji wa serikali tutatumia milunda, mbao, marine board ni misitu, kwa hivyo sekta ya misitu ni muhimu sana" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

Nawapongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kurejesha wanachokipata kwa jamii, wametujengea mabweni, wameboresha soko letu, ni wakati sasa na makampuni mengine yanayonufaika na msitu kurejesha wanachokipata kwa jamii" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Wananchi wa Mafinga, Mufindi, Njombe na Iringa tunataka kujua haya mambo ya hewa ya ukaa, sisi tutanufaikaje mana tunapanda miti, tunatunza vyanzo vya maji, tunachangia hewa safi, tunapata nini?" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Nashauri Wizara ya Maliasili na Utalii mshirikiane na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) ili kuona na sisi Iringa na Njombe tunapataje fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, mana miti tunapanda" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Mradi wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) utekelezaji wake unasuasua sana, mtendeeni haki Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia, kwani aliuzindua mradi huu Februari 12, 12/2/2018 akiwa Makamu wa Rais, sasa miaka mitano lakini unasua sua sana" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Great Ruaha Marathon inatarajiwa Julai 8, mwaka huu, hili ni tukio la kipekee, mbio za marathon ndani ya hifadhi ya Ruaha itasaidia sana kutangaza utalii kusini" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini

"Nawapongeza chama cha mashindano ya mbio za magari, kwa kufanyia mbio hizo kwenye msitu wa Sao Hill, hii inasaidia sana kutangaza utalii kupitia michezo" - Mhe. Cosato Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini
 

Attachments

  • Fx29HEJX0AAOS4-.jpg
    Fx29HEJX0AAOS4-.jpg
    61.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom