Tutu aunga mkono sheria ya kujitoa uhai

Tutu aunga mkono sheria ya kujitoa uhai

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,345
Reaction score
15,850
130827120808_desmond_tutu_464x261_reuters.jpg

Aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana nchini Afrika kusini Desmond Tutu


Aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana nchini Afrika kusini Desmond Tutu ameingilia kati mjadala kuhusu kuwasaidia wanaotaka kujitoa uhai,akisema kuwa anaunga mkono haki ya wale wanaougua kupitia kiasi kuamua kujitoa uhai kwa heshima.


Amesema kuwa alihuzunishwa na vile rafikiye Nelson Mandela alivyoteseka siku za mwisho za maisha yake na kwamba ilikuwa fedheha na ukiukaji wa heshima kwa shujaa huyo.

Katika ripoti yake ilioandikwa katika gazeti moja la Uingereza la Observer ,kiongozi huyo wa dini aliyestaafu amesema kuwa sheria zinazowazuia watu kusaidiwa kujitoa uhai zinazua maswali mengi kuhusu hali ya maisha na kuhusu vile watu wanavyotumia fedha ili kuongeza kipindi cha maisha yao.

Matamshi yake yanajiri wakati ambapo bunge la Uingereza linaandaa kujadili mswada wa kusaidiwa kujitoa uhai baadaye wiki hii.

Bwana Tutu pia ametaka sheria za Afrika kusini kuangaziwa upya kuhusu kusaidiwa kujitoa uhai.


Chanzo:
BBC Swahili
 
Namuunga mkono sioni faida ya mtu kuteseka wakati tunajua hawezi kupona.
 
Laana hii,huyu Tutu anaongea vitu kama mlevi.
anasema lengo ni kumuondoshea mateso mgonjwa ana uhakika gani akifa huko ndo anaenda kupumzika.
Wavimba Macho watampongeza kwa kauli za kijuha kama hizi.
 
Laana hii,huyu Tutu anaongea vitu kama mlevi.
anasema lengo ni kumuondoshea mateso mgonjwa ana uhakika gani akifa huko ndo anaenda kupumzika.
Wavimba Macho watampongeza kwa kauli za kijuha kama hizi.

Sasa akiendelea kubaki katika Hali ya mateso ndio kutampatia nafuu? Tunajua mwisho wake atakufa tu, kwann aendelee na mateso ikiwa tunajua atakufa?
 
Back
Top Bottom