Tutengeneze simple cookies

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,711
Reaction score
62,651
Hi guys hope mko poa,. Kwa ambao mko na changamoto mbalimbali Mungu awafanyie wepesi mkae sawa,..

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada,. Leo tutengeneze biscuits nzuri na tamu Sana,. Ingredients nilizotumia ni Corn flour, maziwa ya unga, condensed milk, butter pamoja na cocoa powder

1. Hatua ya Kwanza utaweka corn flour 500g kwenye bakuli Safi,. Utaongezea maziwa ya unga 100g , condensed milk 300g na butter 100g then utaanza kukanda
2. Utakanda kwa dakika kama nne hivi au tano hadi ulainike na uache kushika mikononi,. Then utaugawanya madonge mawili,. Moja dogo utaweka cocoa powder vijiko viwili vidogo halafu utaendelea kukanda hadi libadilike rangi to chocolate color
3. Ukishakanda yote vizuri utaandaa meza yako ya kukatia,. Utakata donge ambalo Lina rangi kidogo utakata na ambalo haina rangi liwe kubwa kuzidi kidogo halafu utayaunganisha usukume kwa pamoja
4. Sukuma kwa urefu then utakata kwa shapes unazopendelea,. Mie nilikatakata shape ya Love, ua star na duara,. Ila kila mtu na shapes zako unavyoweza kukata
5. Utaandaa baking trays zako ziwe Safi utaweka baking paper halafu utazipanga na kuzipaka butter tena juu kidogo
6. Utabake kwa Moto wa 150 juu na chini kwa muda wa dakika15,. Ila make sure oven yako iko preheated dakika 5 kabla hujaziweka... Zikiwa tayari utazitoa uziache zipoe na zitakua tayari kuliwa ..
Ni laini na tamu sana


Muwe na mchana mwema🤗🤗
 
Imekaa unyamaa…

Next time tengeneza herufi:

X A M D
 
Kama Bado hujaoelewa au huna mpenzi niambie I have a good news for you!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…