Jikoni kwa Evelyn Salt na Mentor: Mapishi ya Cupcakes

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Messages
20,331
Points
2,000

Mentor

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2008
20,331 2,000
Karibuni tena jikoni kwetu. Katika pitapita mitandaoni tulikutana na mapishi haya ya cupcakes (wengine wanaita 'queen cakes'). Recipe iliyotuvutia zaidi ni hii ya kutengeneza 'dough' moja kisha kuitumia kutengeneza cupcakes zenye ladha (flavour) tofauti tofauti. Tizama picha hapa chini. Mapishi haya yanapendeza sana kama unatengeneza kwa ajili ya sherehe. Unakuwa na ladha tofauti tofauti na una uhakika kila mtu atapata ladha aipendayo.

crazycupcakes.jpg


Kama kawaida tunaanza kwa kuainisha mahitaji.


MAHITAJI YA MSINGI:

- mashine ya kuchanganyia unga (ingawa kwa wepesi wa dough yetu unaweza kuchanganya hata kwa mwiko ingawa mashine itakusaidia kufanya kwa ufanisi)
- Oven (kwa kweli ingawa zamani mama aliwahi kupika keki kwa jiko la mkaa, sijui jinsi ya kupika cupcakes kwenye mkaa)
- cupcake tray (tray ya kuwekea cupcakes zako wakati wa kuoka (kama tray la kupikia vitumbua vile ingawa hili lina shape ya cupcakes)
- vikatarasi vya cupcakes
- vipimo [siri kubwa ya upishi (hasa wa kuoka) ni vipimo. Fanya investment ya mara moja tu, nunua vipimo vya vikombe na vijiko.]

MAHITAJI (ya the main dough):

- sukari nyeupe (kikombe kimoja)
- butter (kikombe kimoja - iwe laini lakini sio kimiminika kama mafuta ya kupikia)
- mayai manne (4)
- Unga wa ngano (gramu 240 au kikombe 1 na 2/3)
- maziwa fresh (vijiko viwili vya mezani/chakula)
- baking powder (kijiko cha chai kimoja)

HAKIKISHA kuwa una kila kiungo unachokihitaji kabla hujaanza pishi lako usije ukaishia katikati...

20180520_152248.jpgJINSI YA KUTENGENEZA THE MAIN DOUGH:

- Kwenye bakuli lako (au mixer bowl kama unatumia mashine), ponda ponda 'butter' yako hadi ilainike kabisa.

- Ongeza sukari kisha endelea kuchanganya hadi mchanganyiko wako wote upate rangi ya njano iliyofifia

- Ongeza mayai yako (MOJA MOJA). Kila unapoweka yai moja hakikisha umechanganya mchanganyiko vyema kabla hujaongeza yai lingine.

- Ongeza unga na baking powder kisha endelea kuchanganya

- mwisho ongeza maziwa na umalizie kuchanganya mpaka upate mchanganyiko flani 'amazing' yaani smooth flani (unakuwa mzito kiasi kuliko uji).

BAADA YA HAPO: uache mchanganyiko wako kwenye bakuli lake kisha tuhamie kwenye kutengeneza flavour sasa.


MAHITAJI YA FLAVOURS na JINSI YA KUCHANGANYA:

LABDA nielezee jinsi ya jumla ya kuchanganya.

- Kwa kuwa sisi tumetumia flavour sita, basi tulihitaji kuwa na vibakuli sita tofauti.

- kwenye kibakuli kimoja, unachukua robo kikombe cha mchanganyiko wako hapo juu kisha unauchanganya na mojawapo ya maelekezo namba 1 - 6.

- Kwahiyo kwa mfano unataka cupcake za karoti, basi unachukua robo kikombe ya mchanganyiko wako wa juu, kisha unaongeza karoti zako zilizokuwa 'grated', unachanganya na zabibu zako kavu na mdalasini kwa vipimo vilivyoelekezwa. Vyote unavitia kwenye kibakuli kimoja kisha unachanganya mpaka vichangamane vyema.

- Fanya hivyo kwa flavor zote unazotaka....

1. CARROT CAKE CUPCAKE
- karoti iliyokatwakatwa au 'grated' (nusu kijiko cha chakula) nimekosa neno sahihi la grated
- zabibu kavu (kijiko kimoja cha chai - zikatekate ziwe ndogo zaidi)
- mdalasini (robo kijiko cha chai)

carrot.jpg


2. PEANUT BUTTER CUPCAKE
- Cocoa powder (vijiko viwili vya chai)
- peanut butter (kijiko kimoja cha chakula)

peanut butter.jpg


3. LEMON CUPCAKE

- maganda ya limao yakiwa 'grated' (kijiko kimoja cha chai)
- vanilla 'extract' ladha (kijiko kimoja cha chai)

lemon.jpg


4. BIRTHDAY CAKE CUPCAKE

- Vanilla 'extract' (robo kijiko cha chai)
- karanga lozi 'extract' (robo kijiko cha chai)

birthday.jpg


5. RED VELVET
- cocoa powder (nusu kijiko cha chai)
- rangi ya chakula (nyekundu)

red velvet.jpg


6. OREO COOKIES

- biskuti za oreo (zipondeponde zisiwe unga kabisa)

oreo.jpg


BAADA YA KUCHANGANYA VYOTE kwenye vibakuli vyako,

- weka vikaratasi vyako vya cupcakes kwenye sinia tayari kwa kuweka mchanganyiko

- unachukua mchanganyiko wako unaumimina kwenye vikaratasi vyako. Hakikisha haujai sana maana baada ya kuoka utamwagikia nje.

- WASHA jiko lako (oven) kwa moto wa degree 350 Fahrenheit au 177 Celsius au kama watumia oven ya gesi, basi namba 4.

- moto ukishafikia, tia tray yako kwa dakika 18 hadi 20.

- jinsi ya kujua kama cupcakes zako zimeiva mpaka ndani ni kubonyeza pale juu katikati. Pakibonyea na kutoa maji maji basi bado haijaiva, irudishe na uongeze dakika tatu tatu kisha uwe unaangalia. Ukibonyeza na ikabonyea tu vizuri kama cushion basi toa jikoni na uziache zipoe (usiwe na nchecheto wa kuzila kabla hazijapoa).

- baada ya kupoa kabisa, cupcakes zako zitakuwa ziko tayari kwa kuliwa ama kurembwa (frosting).

20180520_172710.jpg


NB: SOMO la FROSTING ama kuremba cupcakes zako litawajia siku nyingine....

20180520_174246.jpg
Wasalaam wapendwa,
Mentor & Evelyn Salt .
 

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Messages
20,331
Points
2,000

Mentor

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2008
20,331 2,000
That's my sweet mangii....
Kumbe na maganda ya lemon yanatumika, huwa nahisi yaweza kuwa machungu nmezoea maganda ya machungwa.
Ahsante kwa ujuzi mpya
Yanafaa sana...ila lazima uyakate vipande vidogo vidogo (waaita grating). Ile harufu ya limao kwenye kuoka...mpaka majirani lazima waje kuulizia aisee.

Siku nyingine tukipika LEMON BARS itabidi tuje kutoa somo hapa!


Upo vizuri mkuu, hongera.
Tunajaribu mkuu...weekend mubashara na le wife Evelyn Salt

Dah ungejua hapa nilipo... Nisingefungua huu uzi
Una options mbili;

1. tumia uchawi uje, kuna cupcakes kadhaa zimebaki

2. fanya kuzunguza na mkeo Demiss .
 

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Messages
20,331
Points
2,000

Mentor

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2008
20,331 2,000
Nakumbuka pork ribs yangu. Nilikwambia usiniweke sana pia hamu ikaisha.
Nitajitahidi kurekebisha ratiba kisha tuwasiliane...ila kuanzia mwezi ujao tafadhali!

nenda kamshauri mwenzio anataka kuloweka nyama kwenye JD..hahaha nimesoma comment yake nikacheka halafu nikaogopa anaweza asiamke aisee.
 

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
35,047
Points
2,000

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
35,047 2,000
Nitajitahidi kurekebisha ratiba kisha tuwasiliane...ila kuanzia mwezi ujao tafadhali!

nenda kamshauri mwenzio anataka kuloweka nyama kwenye JD..hahaha nimesoma comment yake nikacheka halafu nikaogopa anaweza asiamke aisee.
Uko mfungo na wewe nini??. Yule anataka kuzimika tu . Kwanza nyama itapoteza ladha.
 

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Messages
20,331
Points
2,000

Mentor

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2008
20,331 2,000
Uko mfungo na wewe nini??. Yule anataka kuzimika tu . Kwanza nyama itapoteza ladha.
Hahaha huyo menu yake itaitwa: JD Barbeque.

Mfungo tena? Oooh kisa nimesema mwezi ujao? Hapana...mwezi huu wikiendi zilizobaki ziko booked kazini na majukumu mengine, nitakuwa nakudanganya nikikuahidi chochote.

Ila nitajitahidi kabla hamu yako iishe. Uje na mwanao...
 

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
35,047
Points
2,000

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
35,047 2,000
Hahaha huyo menu yake itaitwa: JD Barbeque.

Mfungo tena? Oooh kisa nimesema mwezi ujao? Hapana...mwezi huu wikiendi zilizobaki ziko booked kazini na majukumu mengine, nitakuwa nakudanganya nikikuahidi chochote.

Ila nitajitahidi kabla hamu yako iishe. Uje na mwanao...
Nitakuja nae labda akipikiwa na wewe atakula.
 

Forum statistics

Threads 1,343,448
Members 515,058
Posts 32,785,202
Top