Tutatosha kweli hapa duniani?

Tutatosha kweli hapa duniani?

Mkuu mbona ninaona kama umejijibu?
Hiyo ipo kiimani zaidi. Ufufuo uongelewao na yesu ni hukumu. Kufufua ukilichukulia kwa kiswahili sanifu ni kuhuisha. Sasa kufufua 'wazima' na wafu! Kwanini wazima wafufuliwe kabla hawajafa?
Kiama maana yake ni mwisho wa dunia. Hapo kutakuwa na makundi mawili, 'wazima' ( watakatifu)na 'wafu' (waliotenda dhambi).
Lakini kiuhalisia hakuna kitakachokuwepo hai wakati kiama kinafika. Uelewe kila nafsi itaonja mauti.
Hizo imani zingine za Kibudha za kuzaliwa upya sizijui.
Asante sana
 
Unauliza duniani tutatosha siku ya hukumu watakapofufuliwa wote walokufa(imani ya kikatoliki), si ndio ?

Kama ndivyo interesting qn
Ila [HASHTAG]#sky eclat[/HASHTAG] amenukuu kuhukumiwa 'wazima na wafu' kitu ambacho kwa mtazamo wangu kufufuliwa kwa wafu sio lazima kwani hukumu itakuwa huko huko. Kama watafufuliwa kwanza basi hawatakuwa wafu tena bali wazima, hii inaleta mkanganyiko.

Kwa upande mwingine dunia inaweza kutosha kwani kuna scientific evidence kwamba the universe inatanuka, pia dunia nayo inaongezeka ukubwa ikilinganishwa na miaka mingi iliyopita. Ingawaje, hatujui mpango wa Mungu wazaliwe watu wangapi kabla ya hiyo hukumu, halafu na capacity ya dunia.

Kingine, kama Yesu Kristo alitembea kwenye maji na kuingia sehemu zilizofungwa baada ya ufufuko, basi wengine watasimama au kukaa kwenye maji wakati wa hiyo hukumu!!!

Kitu kingine, kwani jambo hilo litachukuua muda gani kwa mujibu wa saa zetu? Pia, hilo zoezi litaendeshwaje?
 
Lakini Mungu si anajua pale unapozaliwa tu kwamba huyu atashinda
na huyu atashindwa? (kwa Mujibu wa imani hizo)
Kama ni hivyo basi tunaonewa....hatufanyi vitu kwa utashi wetu....tumerithi na ni kama vilisha pangwa....
 
Back
Top Bottom