Tutashuhudia kutangazwa kwa hali ya hatari?

Tusipoangalia vizuri tutashuhudia jambo ambalo halijawahi kutokea nchini tangu maasi ya jeshi 1964 na pengine pia tangu vita ya Kagera; kutangazwa kwa hali ya hatari (state of emergency) ili hatimaye kurudisha hali ya usalama nchini. Kutangazwa kwa hali ya hatari na rais kunatoa nafasi kwa vyombo mbalimbali kufanya kazi katika ulinzi wa sheria za juu zaidi na ambapo sheria nyingine zinaweza kuwa suspended na hata haki ya habeas corpus kusitishwa.

I hope hatutafika huko maana tukifika itakuwa ni doa kubwa zaidi la utawala wa Kikwete... maana tayari madoa yapo..

Kiwanda At Work.

Sema Mwka 64 Majeshi yaliasi na kumtoa Nyerere madarakani na Waingereza ndio wakasaidia kumrudisha. Mbona una umauma maneno?

Tarehe 20 Januari, 1964 kulitokea maasi katika Tanganyika Rifles. Nyerere alirudishwa madarakani na jeshi la Waingereza lililoletwa kumaliza maasi.

[1] Kwa kiasi cha siku mbili Nyerere alikuwa hafahamiki yuko wapi. Wanajeshi walikuwa wakiwasiliana na Oscar Kambona kujaribu kutatua mgogoro uliokuwepo. Dossa Aziz ndiye aliyemtorosha Nyerere kutoka Ikulu akapita nae lango kuu Nyerere akiwa amejificha katika gari la taka chini ya takataka. Dossa akiwa na bunduki yake alienda na Nyerere hadi Kigamboni kwenye nyumba iliyokuwa ufukweni pwani ambayo ilikuwa ikitumiwa na Gavana kama mahali pa kupumzika. Baadae Rashid Kawawa aliyekuwa makamo wa rais alikwenda pale na wakawa pamoja na Kambona ambae alikuwa kiungo kati ya serikali na wanajeshi walioasi. Nyerere mwenyewe hajakieleza kisa hiki kwa yoyote. Baada ya kujitokeza waandishi wa habari walimuuliza alikuwa wapi wakati wote wa uasi wa wanajeshi. Nyerere kwa ukweli kabisa alijibu, ‘Nilikuwa Dar es Salaam’.

Soma zaidi: http://www.google.co.tz/url?sa=t&rc...sg=AFQjCNEL6uTZ0sCQLL9n9TZTve8cloptCA&cad=rja
 
ila tuache mizaha hali ni mbaya,kinacho-sikitisha wanaosababisha hali hii wanajulikana ila mmmmmmmmmmmm!!!!!!!! MUNGU anajua yaliyofichika, nadhan ponda na wenzake wanashangilia, maana mungu wao yuko kazini kuivuruga TZ yetu
 
Duh, kituko cha mwaka ni kwamba Pinda yupo Uingereza, Kikwete yupo Oman, na Makinda yupo India. Kwa maana hiyo nchi ipo chini ya Ghalib Bilali, yuleyule mpinga muungano. Hivi anaweza kuzuia hizi fujo kweli au atachochea ili iwe sababu ya Muungano kuvunjika? Yetu macho kwa kweli.
 
Mambo yanabadilika kwa haraka sana. Busara ingetumika ili viongozi wote wakuu walio nje ya nchi warudi nyumbani haraka. Najua State visit inaandaliwa kwa muda mrefu lakini rais anatakiwa akatishe hiyo visit arudi, haraka na ahutubie taifa.
Mkuu nakupa pole sana kwani hilo lingewezwa kufanywa na kiongozi anaejali watu na taifa lake.Anaweza akarudi akakuta hali hii na siku inayofuata akaondoka kwenda nchi nyingine.

Tuna bahati mbaya kama taifa na kibaya zaidi hata ndani ya chama chake wamekaa kimya kanakwamba wao sio watanzania.Angekuwepo Nyerere hakika asingemvumilia ila waliobaki karibu wote akili zao zinafanana.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hizi mbegu za udini si za JK kama tunavyoaminishwa bali ni mipango ya CCM ili kubaki madarakani sasa yameanza ndo tunaona JK mbaya mfano mwaka 1995 TLP ilipokua tishio walikuja na UKABIRA kikafa kibudu miaka ya 2000 CUF walipokua na nguvu CCM tena kikaja na sera za udini CUF nayo ikaonekana ni chama cha waislam nacho kikaishiwa nguvu...

2005 udini ukaibukia makanisani kua JK ni chaguo la mungu bila kujua hao maaskofu walikua wanatenda zambi ya ubaguzi ya kuwaaminisha waTZ na uku kuna wagombea wengine, sasa hiyo zambi haitapita iviivi itawarudia uko makanisani mpaka watubu kwa mungu kua MUNGU HAKUA NA CHAGUO BALI WOTE KWAKE NI SAWA
 
Kuanzia leo onward nakuwa makini kuchangia hoja za Mzee Mwanakijiji...nimegundua ni shushushu. Ukicheza nae utanyea debe. I salute you sir!!

Hahahaha.Mkabidhi BWANA kila kitu naye atafanya
 
Nasikitika sana rais aliyeitwa chaguo la Mungu leo anaiingiza nchi kwenye ushetani
 
yaani sijaona rais wa kucheka cheka tu hata kwenye jambo la kuwa serious kweli rais tunaye yaani ni full mzingo ndani ya taifa
 
Mambo yanabadilika kwa haraka sana. Busara ingetumika ili viongozi wote wakuu walio nje ya nchi warudi nyumbani haraka. Najua State visit inaandaliwa kwa muda mrefu lakini rais anatakiwa akatishe hiyo visit arudi, haraka na ahutubie taifa.

This incident is outrageous, is this the type of culture the CCM government has created. Still more to come, i feel for my country be destroy by power monger to divide us in order to rule us
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Haiwezekani hali ya usalama nchi iwe hivi??!! Raisi ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu yupo wapi? Pinda yaye yu Uingereza!! KWa kuwa ni Waislam ambao Rais ni muislam mwenzao na mkuu wa Jeshi la Polisi na yule wa kanda maalum basi jua hakuna kitu!! Ingekuwa ni wakristu wanafanya hivi ungekuta wameshauawa wote kwa sababu wanategemewa ndo wataipa ushindi upinzani 2015.

Tuwe na ukweli ndani yake. Ila nataka kuwaambia wakritu kuwa, ifikapo 2015 makanisa yawe ni maeneo ya hotuba za kisiasa!! Rudisheni ile amani ambayo Marehemu Mwalimu Baba wa Taifa aliyekuwa mkatoliki aliijenga mioyoni mwetu. Ninaandika haya kwa machungu makubwa sana. Leo hii tunaitana kwa udini, ukanda na ukabila, vitu ambavyo mkristu yule Nyerere na Benjamini Wiliam Mkapa walivikataa kabisa maana walijua madhara yake.

JMK imetosha. We are not confortable with you!!!
 
Tusipoangalia vizuri tutashuhudia jambo ambalo halijawahi kutokea nchini tangu maasi ya jeshi 1964 na pengine pia tangu vita ya Kagera; kutangazwa kwa hali ya hatari (state of emergency) ili hatimaye kurudisha hali ya usalama nchini. Kutangazwa kwa hali ya hatari na rais kunatoa nafasi kwa vyombo mbalimbali kufanya kazi katika ulinzi wa sheria za juu zaidi na ambapo sheria nyingine zinaweza kuwa suspended na hata haki ya habeas corpus kusitishwa.

I hope hatutafika huko maana tukifika itakuwa ni doa kubwa zaidi la utawala wa Kikwete... maana tayari madoa yapo..
Hatutafika huko, si kwa sababu hali haipo hivyo, la hasha. Hatutafika huko kwa sababu rais hatotaka, kama ulivyoonyesha, kuongeza madoa kwenye rekodi ya utawala/uongozi wake.
 
Kiwanda At Work.

Sema Mwka 64 Majeshi yaliasi na kumtoa Nyerere madarakani na Waingereza ndio wakasaidia kumrudisha. Mbona una umauma maneno?

Tarehe 20 Januari, 1964 kulitokea maasi katika Tanganyika Rifles. Nyerere alirudishwa madarakani na jeshi la Waingereza lililoletwa kumaliza maasi.

[1] Kwa kiasi cha siku mbili Nyerere alikuwa hafahamiki yuko wapi. Wanajeshi walikuwa wakiwasiliana na Oscar Kambona kujaribu kutatua mgogoro uliokuwepo. Dossa Aziz ndiye aliyemtorosha Nyerere kutoka Ikulu akapita nae lango kuu Nyerere akiwa amejificha katika gari la taka chini ya takataka. Dossa akiwa na bunduki yake alienda na Nyerere hadi Kigamboni kwenye nyumba iliyokuwa ufukweni pwani ambayo ilikuwa ikitumiwa na Gavana kama mahali pa kupumzika. Baadae Rashid Kawawa aliyekuwa makamo wa rais alikwenda pale na wakawa pamoja na Kambona ambae alikuwa kiungo kati ya serikali na wanajeshi walioasi. Nyerere mwenyewe hajakieleza kisa hiki kwa yoyote. Baada ya kujitokeza waandishi wa habari walimuuliza alikuwa wapi wakati wote wa uasi wa wanajeshi. Nyerere kwa ukweli kabisa alijibu, ‘Nilikuwa Dar es Salaam’.

Soma zaidi: http://www.google.co.tz/url?sa=t&rc...sg=AFQjCNEL6uTZ0sCQLL9n9TZTve8cloptCA&cad=rja

Ama kweli jf ni zaidi ya darasa kwqni sikuwa nayajua hayo
 
Naona mna mawazo mgando kama chadema hiyo kitu ya hatari haipo kwa hao wajinga hata shule hawajaenda hivi hamshangai walioko vodacom,serikalini,benki hawatoki makazini kwao kwenda kuandamana kwa upuuzi huo!!
 
MMM nani anaweza kutangaza hali ya hatari kama Rais wa nchi hayupo nchini?kuna taarifa tumepata baada ya huko uarabuni ataelekea Japan

legally yes; madaraka yake ya kutangaza hali ya hatari ni ya kwake mwenyewe lakini ana uwezo wa kuyakasimu kwenye baadhi ya mambo n.k lakini vile vile yanaweza kutolewa na mtu ambaye atatoa kwa jina la Rais. Lakini kikiwaka hiyo safari nyingine akiendelea nayo basi ndio itakuwa imekula kwetu.
 
Kuanzia leo onward nakuwa makini kuchangia hoja za Mzee Mwanakijiji...nimegundua ni shushushu. Ukicheza nae utanyea debe. I salute you sir!!

mmh.. na wewe nawe; mnatishwa mno. Mtu akisema yuko Usalama wa Taifa mnaogopa, mtu akizungumza hivi mnadhani ni shushushu. Mashushushu wa kweli hawajulikani na wala huwezi hata kumhisi! Mtanipa ujiko ambao hata sina wala sifikirii kuwa nao.
 
Mambo yanabadilika kwa haraka sana. Busara ingetumika ili viongozi wote wakuu walio nje ya nchi warudi nyumbani haraka. Najua State visit inaandaliwa kwa muda mrefu lakini rais anatakiwa akatishe hiyo visit arudi, haraka na ahutubie taifa.

Kwani nchi ina viongozi? Wote wapo omaa mwingine yupo wingereza kaenda kuongelea mambo yake ya nyuki na madam spika yupo zake India
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wakati hali ya usalama imekuwa hivi bado kiongozi mkuu wa nchi anakata mitaa ughaibuni. Ndio maana mie siku hizi nikimuona mtu anakimbilia sana ikulu namuogopa kama JK.
 
Tusipoangalia vizuri tutashuhudia jambo ambalo halijawahi kutokea nchini tangu maasi ya jeshi 1964 na pengine pia tangu vita ya Kagera; kutangazwa kwa hali ya hatari (state of emergency) ili hatimaye kurudisha hali ya usalama nchini. Kutangazwa kwa hali ya hatari na rais kunatoa nafasi kwa vyombo mbalimbali kufanya kazi katika ulinzi wa sheria za juu zaidi na ambapo sheria nyingine zinaweza kuwa suspended na hata haki ya habeas corpus kusitishwa.

I hope hatutafika huko maana tukifika itakuwa ni doa kubwa zaidi la utawala wa Kikwete... maana tayari madoa yapo..

Sasa ndio nakubaliana na usemi wa Dr. Slaa kuwa nchi haitatawalika. Kumbe alikuwa anamaanisha kushindwa kwa uongozi ulioingia marakani kwa kuchakachua. JMK ameshindwa kutawala.
 
Back
Top Bottom