Tutakuheshimu Mzazi kwa yaliyo Mema na sio Mambo ya kishenzi na kidhalimu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
TUTAKUHESHIMU MZAZI KWA YALIYO MEMA NA SIO MAMBO YA KISHENZI NA KIDHALIMU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Angalizo: Lugha itakayotumika inaweza kuwa Kali. Hivyo kama sio Mpenzi wa Lugha Kali, na unahitaji Roho yako iwe na utulivu nakuomba usisome, uishie hapahapa. Kukaidi, madhara yoyote yatakayo kupata nisihesabike kama sehemu ya madhara hayo, Bali wewe mwenyewe.

Juzi hapa nilikuwa naangalia TBC ONE, Huko nikakutana na habari ya kishenzi na kidhalimu iliyotokea Huko Mkoani Mara, "KUOLEWA NA KABURI" ndio title ya Habari Ile.

Yaani kuna wazazi washenzi na Wadhalimu sijapata kuona. Sisi Watibeli Jambo Hilo halikubaliki. Kwetu kuwa mzazi haimaanishi utaheshimiwa hata ukitenda mambo ya kishenzi na kidhalimu. Huo unafiki hatuna. Mimi kama Robert Mtibeli, huo unafiki sijawahi kuwa nao.

Kwa kifupi kisa kipo hivi kama kilivyoripotiwa TBC ONE;
Binti anakuja kutolewa Mahari(nayo ni Mila ya kishenzi na kidhalimu), Baada ya taratibu za Mahari kumalizika, Binti anachukuliwa, hapo hamjui anayeenda kumuoa yaani hamjui mumewe, kukataa hawezi kisa anaheshimu ushenzi na udhalimu WA wazazi wake.

Anaenda kwenye ukoo wa mumewe, huko atakuwa na Yule aliyekuja kutoa Mahari ambaye Wakati huo alimfahamu kama Mshenga kumbe ni Ndugu wa Marehemu ambaye amekuja kumuolea Ndugu yake.

Anaulizia Mumewe Yuko wapi, ndio anaambiwa ukweli kuwa; Mumewe alikufa na Kaburi lake liko pale nje(anaonyeshwa) Kwa hiyo ameolewa na Kaburi. Mwanamke wa Watu anabaki kushangaa, anarudi nyumbani kwao kuuliza kulikoni Wazazi wanamfukuza binti Yao, pasipo kujali hisia za Binti wao, pasipo kuangalia nafasi ya Binti Yao. ATI kisa walichukua Mahari.

Na wanampa vitisho cha kipuuzi na kipumbavu, mara sijui laana(ambayo hawajui hata maana yake kwani wanaakili ndogo hata kama walimzaa, kuzaa na Akili hakuna uhusiano wowote).

Binti Kwa kutojua Haki Kwa sababu alizaliwa kwenye kizazi kidhalimu, familia na ukoo wa kidhalimu(dhulma), naye anakubali kujidhulumu Kwa dhulma aliyotendewa na Wazazi wake, anawasikiliza.

Anarudi alipoolewa(huku mumewe akiwa ni marehemu), anaendelea na Maisha ya ujane wa kishenzi, anakosa Haki zake kama MKE, ikiwa ni pamoja na kukosa mtu wa kumtatulia mambo yake kama MKE, na Yule aliyemuolea Kaka yake humjibu mara Kwa mara kuwa Mimi sio Mumeo.

TBC ONE imeonyesha Wanawake zaidi ya watatu waliokumbwa na utamaduni huo. Kumaanisha sio MTU mmoja.

Nimetoa kisa hicho kama kielelezo na mfano WA moja ya Matendo ya kidhalimu na kishenzi yanayoyafanywa na Baadhi ya Wazazi Kwa ubinafsi wao, na udhulamati wao, na ushenzi wao, na unyama wao.

Mimi kama Taikon, ndiye Mtibeli halisi; Hata angekuwa mzazi wangu, upuuzi wa namna Hii hauvumiliki, na hatutauvumilia bila kujali Matokeo.

Kuwa na adabu na heshima ni kuheshimu Matendo Mema ya Watu. Kuwa mzazi haitoshi kuheshimiwa, Uzazi ni jukumu la viumbe wote, nasemaga hata panya anazaa. Heshima na Haki ndio itafanya Watoto wakuheshimu. Na sio kuzaa

Kama kuzaa ndio heshima basi Watu wangezaa Watoto elfu ili wapate heshima elfu yaani heshima nyingi.
Mimi pia ni mzazi lakini kuzaa kwangu siwezi Kutumia kama kigezo cha kutenda mabaya alafu nitake kuheshimiwa.

Kuna Wazazi hutishia Watoto wasio na utambuzi, wasio na Elimu ya Kiroho, Elimu ya miungu, Elimu ya dunia, wakiwatisha na kulazimisha heshima wasiostahili. Sisi Watibeli Hilo halipo.

Hata Mimi, nikiwa Kama Baba, Watoto wangu, najua mtasoma mambo haya kama nilivyowaandikia katika nyaraka mbalimbali, yakuwa hata ni Mimi Baba yenu, ikiwa nitaleta mambo ya kishenzi na kidhalimu, basi sistahili kupewa heshima.

Mniheshimu Kwa kuwafundisha YALIYO MEMA. Na mafunzo yapo ya mdomo na Matendo. Lakini kama nitawafunza ushenzi na udhalimu msiniheshimu, mnidharau Kwa sababu niliamua kujidharau. Na Mungu aliyeumba huu Ulimwengu hatawahesabia Hatia. Kwa sababu Mungu wa Tibeli ni Mungu wa HAKI.

Kuwafundisha Watoto maadili sio tuu kuwaambia Bali ni pamoja na kutenda. Ili waweze kukuheshimu. Vinginevyo hakuna heshima hapa.

Hivi unamfanyia Binti yako wa kumzaa mambo ya kidhalimu, kisa maslahi yako ya Mahari(Biashara haramu). Unashindwa kumsikiliza mtoto yeye anataka nini kwenye Maisha yake.
Ubinafsi na ukatili wa Hali ya juu Kabisa.

Alafu mnakuja na maneno yenu ya kishenzi na kidhalimu, ooh! Mzazi hakosei, mara kitanda hakizai haramu, yaani maneno ya kidhulma dhulma yanayotamkwa na Wadhalimu.

Hivi umemuuza mtoto Kwa MTU asiyempenda unategemea ataishi Kwa Raha, unategemea hataleta Watoto wa nje?

Haki na Ukweli ni muhimu. Mzazi kama unashida na Pesa, tafuta zako au muombe Mungu akupe bahati mtoto wako afanikiwe kisha akukumbuke, akulipe fadhila.

Haya unakuta mzazi anasema Mimi sio Mama yako au Baba yako, kwani Nani aliyejitambulisha Kwa mwenzake? Watoto huzaliwa wakiwa hawajui kitu chochote, ukisema yeye sio mwanao ni sawasawa na ulivyosema yeye ni mwanaye, ukweli unaujua mzazi na sio Mtoto. Tena mzazi anayekuambia hivyo anakuambia akikushinikiza ufanye Jambo ambalo sio HAKI na wala halimhusu(halipo katika mipaka yake). Huo ni ushenzi.

Mtoto akishakua mkubwa muache aendelee na Maisha yake.

Ajifunze mambo mazuri Kwa kukuona sio unavyomwambia.

Mifumo ya kidhalimu na kishenzi imegharimu Maisha ya familia nyingi Mno. Watu Hawana upendo Kwa sababu wanaongozwa na Kanuni na tamaduni za kibinafsi.

Tuache ubinafsi ambao ndio huzaa udhalimu na ushenzi.
Mtu kumzaa haimaanishi unamamlaka juu yake katika Maovu na ushenzi wako.

Na Sisi Watibeli tunawaambiaga kuwa tupo tayari kupewa laana(kama wanavyofikiriaga) kuliko kuunga mkono udhalimu na ushenzi Kwa kisingizio cha Uzazi.

Acha nipumzike sasa. Ni Yule Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli, yenye mbawa mbili irukayo toka Ulimwengu mmoja kuelekea Ulimwengu mwingine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
download (1).jpeg
 
Back
Top Bottom