Tutakaopata nafasi ya kutoa maoni ya katiba, please tusisitize jambo hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutakaopata nafasi ya kutoa maoni ya katiba, please tusisitize jambo hili!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Nyalotsi, Aug 19, 2012.

 1. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Suala la afya liwe ni haki ya msingi kwa kila mtanzania. Serikali iwe responsible na aina ya huduma za afya wanazopewa wananchi wake. Hii ina maana kwamba huduma zitakazotolewa na kituo/hospitali yoyote ziwe under regulations zinazoruhusu wananchi kuwashitaki wenye hospitali/kituo cha afya kama huduma walizopewa haziendani na gharama au ni tofauti na alizohitaji mgonjwa. Nimepitia kwenye katiba hii sijaona sehemu hili lilipoongelewa. Hii itasaidia pia kupunguza uharamia wanaofanyiwa wagonjwa na madaktari wasiokuwa na ethics zilizowakaa,wakazielewa vizuri. Asanteni kwa wale mtakaosaidia kulisemea hili, maana maoni mengi nimeona yanaelekea kwenye siasa tu.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nyalotsi usiumize kichwa katika hilo, ni rahisi kama ifuatavyo, ibara isomeke hivi;

  "ITAKUWA NI MARUFUKU KWA KIONGOZI WA SERIKALI YA JMT KUTIBIWA NJE YA JMT PAMOJA NA MAMLAKA YAKE" (ikithibitika kitaalamu kuwa ni lazima kiongozi huyo kwenda nje ya nchi kwa matibabu, basi madaraka yake ya kiserikali yatakomea hapo, na matibabu atakayoyapata yatagharimiwa na serikali)

  Hapatatumika nguvu nyiiiingi kuwalazimisha walete ma-ct scan, hawatawakorofisha madokta.

  Na kwa upande wa elimu iwe kama ifuatavyo,

  "ITAKUWA NI MARUFUKU SERIKALI YA JMT KUAJIRI MTUMISHI AMBAYE HAKUSOMA SHULE ZA SERIKALI MFULULIZO TOKA CHEKECHEA HADI KIDATO CHA SITA"

  Hapo nchi itaanza kunyooka.

  Unasemaje! nikupe na verse ya madini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. u

  usungilo JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 501
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  hii kitu ina ukweli wake. Kuna haja ya kuweka taratibu za aina ya wahudumu wanaotakiwa kuwepo kutoa huduma kwa kila level. Haiwezekani watu wanataka kuendelea kuturudisha nyuma kila siku. Inatakiwa kiwepo kipengele kinachoruhusu wananchi kuwashitaki madaktari pale wanapovunja taratibu za kitabibu.
   
Loading...