Tutafuteni hela vijana

Tutafuteni hela vijana

G55-MGODI

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2016
Posts
1,353
Reaction score
1,825
Wanajamiiforums tafuta pesa zako upunguze kumuita kila mtu, "MKUU, KIONGOZI,MKURUGENZI, BOSI!" Unajiabisha sana mwanangu.

Tafuta pesa kijana wangu ili hata Polisi wakikukuta umetulia sehemu wakuulize "MKUU KUNA SHIDA YOYOTE?"

Hata wewe binti yangu tafuta pesa hata siku unapewa appointment ukafika kabla bae wako hajafika uwe na ubavu wa kuagiza hata kinywaji kuliko kusimama nje ukitoa macho utadhani mwewe unazengea kifaranga kumbe unamsubiri aje! Loh!

Tafuta pesa ili eupuke usumbufu wa kujitambulisha kwa kujieleza sanaaa. Unajua mimi ni mtoto wa binamu yake na Trump.Mara ooh, nilisoma na mtoto wa Kikwete. Unaona mateso yote hayo?

Tafuta pesa uepuke kurushiwa mapepo kwenye mikutano ya injili. Ndiyo!! Kwani watumishi huwa wanaelekezea wapi mapepo? Sikule walikokaa maskini??

Tafuta pesa usionekana mkorofi. Kama huna hata kwenye vikao vya familia ukinyosha mkono kuchangia hoja wanasema unataka kuleta fujo, kumbe ana bonge la point!

Tafute pesa uepuke kulala kwenye guest zenye ndala zenye miguu tofauti na rangi tofauti ili usiziibe. Maskini haaminiki kuanzia kwao hadi guest!

Tafuta pesa makonda wa daladala wasikutukane kama yule babu aliyesema KONDA, ONGEZA SAUTI TUMSIKILIZE BABA WA TAIFA------ UNGEMSIKILIZA BABA WA TAIFA UNGEKUWA NA GARI LAKO!

Tafuta pesa ili ukienda ugenini wasiwe na hofu na wewe kwamba unaweza kuondoka usiku wa manane umewaibia.

Tafuta hela ndugu wa mke wakuite SHEMEJI, kama hauna watakuita MUME wa mama! Ohooooo!🤓🤓🤓

Pesa inapatikana through smart working and not hardworking
 
Naomba npe hata mbinu/njia/ajira moja tu ya kutngeneza hata elfu 15 kwa sku. mwanangu n bora kukosa wazazi kuliko kukosa pesa.
 
Bado pesa sio mwarobaini wa hizo changoto ulizoainisha zitokanazo na ukosefu wa pesa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom