Pole sana Kingwipa1, maandishi yako yanadhihirisha kwamba una uchungu mkubwa na ubadhirifu uliopo nchini. Kiukweli inauma sana pale unapotambua kwamba thamani ya mtanzania mzalendo ni second priority kuliko thamani ya wageni, mafisadi na wanyonyaji wa uchumi wa nchi yetu.
You can just imagine kwamba wakati Mwakalebela anatoswa ubunge kwa kutoa rushwa ya pengine laki moja, Endrew Chenge anapitishwa na kamati kuu hata baada ya kudhihirika wazi kwamba alikula rushwa ya mabilioni ya fedha kutoka BAE system ili kuitia hasara Tanzania katika ununuzi wa Rada. Basil Mramba anapitishwa kugombea ubunge pamoja ya kwamba ndiye aliyekuwa waziri wa fedha wakati mabilioni ya shilingi yalipochotwa kutoka EPA, na tayari amefunguliwa kesi mahakamini. Hii haiingii akilini kabisa. Haya nayo ni ushahidi kwamba mtanzania mkulima ua mfanyakazi wa kawaida hana nafasi ndani ya CCM.
Ndugu zangu, tuna kazi kubwa mbele yetu, kazi hiyo ni kuirudisha nchi mikononi mwa watanzania wazalendo, kuikomboa nchi kutoka kwa mafisadi wachache wanaojinufaisha kwa kuwakandamiza masikini walio wengi. Tujipange, tuamue, tunaweza! Yes we can!!! Say no to CCM in 31st October.