Tusome: Utawala ukifitinika hauwezi kusimama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusome: Utawala ukifitinika hauwezi kusimama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kingwipa1, Sep 20, 2010.

 1. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Utawala ukifitinika hauwezi kusimama, ni ujumbe wenye maneno machache lakini ukiwa umebeba ujumbe mzito.

  Utawala wa CCM umefitinika na kwa hiyo ni mwaka wa kuaga ikulu. Tumeshuhudia migogoro mingi kuanzia chama tawala ambacho ndicho kinaunda serikali na baadae tumeona jinsi watawala wetu wanavyotumia nguvu na pesa kutaka kumalizana kisiasa. Hiyo ni picha wazi kuwa serikali iko bize kupigana vikumbo ili kunyakua rasilimali za taifa.

  Kwa kufitinika huko ni wazi kuwa kidole kimeshaandika kwenye ukuta na wenye kujua alama za nyakati tunajua kuwa CCM haiwezi kusimama kama chama tawala.

  mene mene tekeli na perezi!!
  naomba wadau tuweke migogoro iliyoko ndani ya chama tawala na serikali yake ili tuone ni kwa kiasi gani serikali hiyo haiwezi kuwa moja tena.
   
 2. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Pole sana Kingwipa1, maandishi yako yanadhihirisha kwamba una uchungu mkubwa na ubadhirifu uliopo nchini. Kiukweli inauma sana pale unapotambua kwamba thamani ya mtanzania mzalendo ni second priority kuliko thamani ya wageni, mafisadi na wanyonyaji wa uchumi wa nchi yetu.

  You can just imagine kwamba wakati Mwakalebela anatoswa ubunge kwa kutoa rushwa ya pengine laki moja, Endrew Chenge anapitishwa na kamati kuu hata baada ya kudhihirika wazi kwamba alikula rushwa ya mabilioni ya fedha kutoka BAE system ili kuitia hasara Tanzania katika ununuzi wa Rada. Basil Mramba anapitishwa kugombea ubunge pamoja ya kwamba ndiye aliyekuwa waziri wa fedha wakati mabilioni ya shilingi yalipochotwa kutoka EPA, na tayari amefunguliwa kesi mahakamini. Hii haiingii akilini kabisa. Haya nayo ni ushahidi kwamba mtanzania mkulima ua mfanyakazi wa kawaida hana nafasi ndani ya CCM.

  Ndugu zangu, tuna kazi kubwa mbele yetu, kazi hiyo ni kuirudisha nchi mikononi mwa watanzania wazalendo, kuikomboa nchi kutoka kwa mafisadi wachache wanaojinufaisha kwa kuwakandamiza masikini walio wengi. Tujipange, tuamue, tunaweza! Yes we can!!! Say no to CCM in 31st October.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mjomba,

  Samahani, sijui kama nitaeleweka kirahisi.

  Lakini naona kama mnaulizia kwetu listi ya migogoro yenu ili muisawazishe fasta kabla ya anguko kuu la MNYAMA!
  Kwa vile tumeshakuelewa hatuthubutu kuitaja hiyo migogoro ili muendelee kujikaanga kwa mafuta yenu wenyewe!...
  Propaganda hizi mlizojifunza KULE Afrika ya Kusini nyie Green Guards haziwezi kumshinda mwanamageuzi yeyote!
  POLE NDUGU...msalimie sana Yusufu Makamba!
   
 4. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  PakaJimmy,
  Sina uhakika kama unanielewa vizuri. Mimi ni mwanamapinduzi halisi na si radical revolutionalist, unajaji kutoka angle moja na hapo ndipo unapo-miss point.

  Anyway mimi ninaloliona ni anguko la utawala kwa kuwa sasa utawala wa CCm umeshatoka kwa wananchi kikapewa kikundi fulani na baadae kimenyang'anywa na kupewa familia ya JK.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ajidhaniaye amesimama AANGALIE asianguke.

  Kuna kuanguka na kushindwa kusimama tena kama UNIP ya zambia.
  CCM wakishapigwa za uso uchaguzi huu ndo imetoka hiyo.
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ajidhaniaye amesimama AANGALIE asianguke.

  Kuna kuanguka na kushindwa kusimama tena kama UNIP ya zambia.
  CCM wakishapigwa za uso uchaguzi huu ndo imetoka hiyo.
   
Loading...