Tusiwe wepesi wa kuhukumu mapema

Tusiwe wepesi wa kuhukumu mapema

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,988
Mume na mke wakiwa kitandani ukimya ukiwa umetawala huku mume akionekana kanuna sana.

Mke akawa anawaza.

"Kwanini haongei na mimi? Mbona amebadilika ghafla?, Nini kimemkasirisha?, Au ana mwanamke mwingine siku hizi?, Au mimi simvutii tena?, Anataka kuniacha?, Najua mama yake hanipendi au kashamtafutia mwanamke mwingine?, Mh.. yaani ndio naelekea kuwa single mother?, Nani atanioa mimi kashanizalisha watoto watatu?. Eeeh Mungu wangu inusuru ndoa yangu nakuomba".

Ikawa ni mawazo juu ya mawazo kwa mke yule uku akijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.

Baadae, akaamua liwalo na liwe ni heri amuulize nini tatizo.

"Honey una shida gani tokea umerudi umekasirika na hutaki kabisa kuongea na mimi hata chakula nilichokuandalia haujakigusa?"

Ndipo mumewe akajigeuza kumuangalia mkewe kwa hasira huku macho yamemuwiva akasema.

"Hivi inawezekanaje katika dunia hii sisi Barcelona tufungwe na Liverpool goli 4 kwa sifuri wakati uwanjani tuna Messi, Suarez, Coutinho enhee, haya si mambo ya ajabu kabisa haya?"

Mke wake akashusha pumzi ndefu akaishia kutabasamu tu akazima taa akajilalia zake.

Wadada kuna wakati huwa mnajipa mashida wenyewe tu kwa ndoa zenu
[emoji2][emoji2][emoji13]
 
Nimekuja speed nikajua kuna mkasa kisha funzo. Kumbe kutambiana na ligi za wenzetu.
 
Ni moja ya mfano bora kabisa, sometimes tunawaza ya kwetu kabisa tatizo wao wanavyoyafsiri sasa ndo shida.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom