Waraka wa Idd kwa wanaume wanaowapiga wake zao

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,949
Iddi Makengo
16 hrs ·
STORI YA MAISHA YANGU; MUME WANGU NAOMBA LEO USINIPIGE!
“Mume wangu naomba leo usinipige, nimechoka sana mume wangu, naomba tu usinipige…” Mke wangu aliongea kwa unyonge, alikua amekaa sebuleni kachoka, mimi ndiyo nilikua nimetoka kazini.

“Inamaana unaniona mimi mjinga nakupiga tu bila sababu, kama umefanya kosa utapigwa tu mpuuzi mkubwa! Yaani mume wako anarudi kutoka kazini badala ya kumpokea unaanza kuongea habari za kupigwa! Mbwa mkubwa wewe! Shetani wewe, unataka nijisikie vibaya kuwa nakupiga piga bila sababu!” Nilijikuta nawaka, sijui hasira nilizotolea wapi lakini mke wangu alinitibua, kwa maneno yake nilimfuata na kutaka kumpiga.

Tofauti na siku nyingine mke wangu alikua amekaa tu, nilimsogelea mpaka alipokua kakaa, nikamshika nguo yake na kumnyanyua huu, nilishangaa alikua mwepesi sana, lakini sikujali, nilimsukuma na kumkanyaga tumboni, nikamalizia kwa matusi kadhaa kisha nikaingia zangu ndani. Hakunyanyuka pale alipokua amekaa na wala hakupiga hata kelele.

Sikua nimepanga kutoka, lakini niliona kama mke wangu amenikosea heshima, kaniharibia siku yangu, nilitoka na kumpita pale sebuleni, sikumsemesha kwani nilikua na hasira, nilienda mpaka mezani na kuchukua ufunguo wa gari, gari ya mke wangu.

Ingawa ilikua na jina langu lakini ilikua ni gari ambayo mke wangu alinunua kwa pesa zake lakini baadaye nilimlazimishia akabadilisha jina na kumpa. Nilikua nikiitumia kama yangu, alinunua kwaajili ya kuendea kazini, wakati huo sina kazi lakini nilikua nazurura nayo kufanya umalaya. Hata nilipopata kazi na kuwa na gari la kazini lakini bado nilimnyanyasa, sikumruhusu kuendesha na kama ikitokea anaendesha nilikua nampiga sana.

Niliondoka mpaka kwa Mama mmoja mtu mzima ambaye alikua ni mchepuko wangu wa muda mrefu, naye alikua ananihudumia na mara nyingi alikua akimpigia simu mke wangu kumtukana.
Mimi ndiyo nilikua namuambia, ampigie kumtukana ili mke wangu ajue kuwa mimi ni kidume na si kama yeye anavyonidharau.

Kila siku nilikua naamini kuwa mke wangua nanidharau ndiyo maana nilikua namdhalilisha kila siku. Usiku nilipigiwa simu, ilikua kama saa nane usiku, ilikua ni simu ya Mama yangu, nilishangaa na kuhisi kitu kibaya kimetokea, Baba yangu alikua anaumwa ana hali mbaya Kijijini, nilijua kama Mama ananipigia simu usiku huo basi labda ameshafariki.
“Uko wapi?” Mama aliniuliza baada ya salamu.

“Acha upumbavu, watu wanakutafuta haupatikani, simu umezima ya nini? Inamaana huna taarifa za msiba?” Nilishangaa, simu yangu sikuzima kabisa lakini Mama alikua anasema sipatikani, alitaja msiba nikajua Baba tayari, lakini kwa namna alivyokua anaongea Mama nikama hakuna kitu kimetokea kikubwa.
“Baba amefariki?” Niliuliza kwa kusikitika, nilijifanya kushangaa lakini ukweli ni kitu ambacho wote tulikua tunakisubiria.
“Chunga na mdomo wako! Tema chini! Mama Sadia, Mke wako kafariki! Yaani uasema upo nyumbani hata hujui kama mke wako kafariki?” Nilishikwa na butwaa kwani nilikua sijui chochote.

“Nitakua nimemuua mke wangu!” Niliwaza huku nikinyanyuka na kuvaa nguo, Mama bado alikua anaongea lakini sikujua hata anaongea nini? Niliwaza mambop mengi, niliwaza kuhusu Polisi, nilijua ni mimi, niliwaza labda nilimkanyaga vibaya, niliwaza kuhusu mwanangu Sadia, ndiyo kwanza alikua na miaka mitatu. Baada ya kukaa kwenye ndoa bila mtoto nilishakata tamaa mpaka nilipompata Sadia, kwanza mke wangu alipopata ujauzito nilijua si wangu, nilikua nampiga sana ili mimba itokea lakini Mungu aliniumbua, alikua ni mtoto wakike lakini alifanana kila kitu na mimi, hata ningekataa vipi isingeeleweka.

Nilikua na wasiwasi kuwa si wangu kwani tangu mdogo nilikua na tatizo la nguvu za kiume, nilikua siwezi kufanya mapenzi kwa zaidi ya dakika mbili, nalala na hata goli langu lilikua dhaifu, nlishahangaika kwa waganga mahospitalini kimya kimya kote naambiwa mbegu zangu hazina nguvu. Pamoja na kuujua ukweli lakini siku zote nilikua namshutumu mke wangu, namuambia yeye ndiyo mwenye matatizo nampig na niligoma kabisa kuongozana naye hospitalini, alipopata ujauzito niliukana kwani niliambiwa siwezi kupata mtoto kirahisi kwakua mbegu zangu hazina nguvu.

Nilipewa madawa mengi lakini kila nikipima niliona kama hayasaidii, nikaamua kuacha na kuhamia kwenye pombe na wanawake ili kujione kidume. Baada ya mke wangu kujifungua mwanangu niliacha manyanyaso kidogo, ndoa ikawa na amani lakini nilshazoea, nilikua sina raha, nilikua nahisi kwakua sina nguvu za kiume labda ananidharau, labda ana wanaume wengine, nilikua nampiga sana bila sababu, yaani hata kama akinifumania mimi, kosa ni langu lakini nampiga, sasa alikua amekufa, nilikua nimemuua.

Yule Mama niliyekua natembea naye aliniuliza, nilimuambia mke wangu amekufa kisha nikaondoka. Nilienda mpaka nyumbani nikiogopa, nilimpigia dada wa kazi, alikua analia tu, nikamuambia amtoe mtoto nnje naenda kumchukua. Lengo langu lilikua ni kumchukua mwanangu na kutoroka naye, kwangu ilikua bora kuondoka kuliko kesi ya mauaji. Kila mtu alikua anajua kuwa nampiga mke wangu na nilijua dada wa kazi kaona nikimpiga hivyo kama Polisi wakija basi atahojiwa na mimi nitakamatwa.

Nilifika nyumbani lakini Dada alikua bado hajatoka, niliangalia kulikua na watu wachache, nilitaka kuondoka, lakini kabla ya kufanya hivyo waliniona na kuanza kunipa pole, pamoja na kuwa ilikua usiku watu walikua wanakuja nyumbani kwangu. Nilingia nao, mke wangu alikua chumbani, niliingia na kumuta kama vile kalala..

“Kansa mbaya sana, yaani ziwa lote limeoza, Pole Kaka yangu, mimi sikujua…” Alikua ni Dada yangu, mimi mwenyewe sikujua kama mke wangu anaumwa, niliitikia pole yake na kumuambia atokea nataka kubaki na mke wangu.
Alitoka na kuniacha peke yangu, nilimfuata mke wangu kitandani, nikaamfunia titi moja la kulia lilikua lina kama limeisha flani, huku jingine likiwa limeoza lakini si sana. Nilishangaa kwani ni muda sana sijamgusa mke wangu, tangu ana ujauzito wa mtoto wetu niliacha kutembea naye mpaka alipojifungua.

Nilikua namuambia kuwa ananuka, ameharibika hanivutii lakini ukweli nikuwa nilikua siwezi kufanya mapenzi, hata kwa michepuko mingi niliishia kuilewesha na kuishikashika, sikua na hisia na sikua na nguvu kabisa, hata zile dakika mbili nilikua siwezi tena.

Kumbe baada tu ya kujifungua mke wangu aligundulika kuwa ana Kansa ya titi, alishafanyiwa upasuaji lakini haikusaidia, wakati huo mimi nilikua hapohapo nyumbani lakini sikujua kuwa mke wangu alishawahi kulazwa hospitalini mwezi.

Mara nyingi tu nilikua sirudi nyumbani na kumbe alikua akiwadanganya watu nimesafiri kikazi ili kulinda ndoa yake. Aisee nilipata mwanamke, niliumia sana siku anazikwa, kumbe siku ila ananiambia nisimpige nikuwa alikua anataka kufa kwa amani, mke wangu alifariki nikiwa siji kama anaumwa.

Ndugu walinipa pole, majrani waliniangalia tu kwani walikua wanajua tabia zangu lakini hakuna ndugu hata moja ambaye alijua. Walikua wananilindia siri yangu. Ni mwaka wa kumi sasa tangu mke wangu kufariki, sijaoa mwanamke mwingine, sio kwamba sitaki lakini siwezi, kila mwanamke nineyekua naye nikitembea naye kidogo ananiacha, nina msongo wa mawazo. Wakati Mama yake anafariki mwanangu alikua na miaka mitatu, lakini huwezi amini tangu siku hiyo mwanangu hajakubali nimguse, huwezi amini ni kama alikua anaona mambo yote niliyokua namfanyia Mama yake.

Nakumbuka ilikua ni baada ya kutoka kakaburini, mwanangu alikua analia, watu wakasema mpelekeni kwa Baba yake, walimleta, alilia mara kumi yake, huku akipiga kelele “Hitaki! Shitaki! Shitaki!” Aliongea huku akilia na kujirusha, tangu siku hiyo hakukubali kabisa nimguse. Sasa hivi ana miaka 13, anasoma Dadasa la 6 lakini hanipendi, ananichukia kama vile si Baba yake, Mama yake angekua hai au angekufa akiwa mkubwa ningesema kamuambia mambo mabaya, lakini si hivyo ananichukie tu.

Nafanya kazi, nina kipato kizuri lakini maisha kwangu hayana thamani, sijaoa, nasingizia bado nina uchungu wa mke wangu kumbe nina mengine.

Lakini nawaza je naweza kupata mwanamke mwingine kama mke wangu, pamoja na kujishusha, kujaribu kunipa furaha lakini sikuiona, nilibaki na maumivu yangu tu. Maisha yamekua magumu sana kwangu, natamani kurudisha siku nyuma, angalau niishi kwa amani na mke wangu, nimuonyeshe hata nusu tu ya mapenzi ambayo alikua ananionyesha lakini siwezi, najuta na sijui cha kufanya. Kama una mtu anakupenda na anakuonyesha upendo basi muonyeshe kwelikweli kwani muda wa kuishi hapa duniani ni mchache sana, acha kutumia kwa kuwa na kisirani.

****MWISHO;
Image may contain: 1 person, shoes and outdoor
 
Shida moja ya Iddi Makengo, hawaambii wanawake wapi haswa wanakosea hadi wananzisha mahusiano na mijanaume isiyo na utu
natamani kila mwanamke angegundua wanapokosea wao kabla ya kuwalaumu wanaume "WOTE"
Wanaume wengi ni wataratibu sana ila wanaume wabaya ambao ni wachache huonekana mara nyingi
 
Yani bro usemacho watu wengi sana hawakisemi au labda hawakijui ila kiukweli wanaume wenye tabia mbovu ni wachache ila wanaonekana sana ila wengi wapo wametulia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe, shida inaanzia kwenye kuchagua mume wa kukuoa. Vigezo ni mali na pesa wanasemaga mengine watavumiliana mbona hawavumiliani sasa?
 
Hii simulizi imenikumbusha mambo mengi.

Mama yangu alifariki kwa cancer ya ziwa ambayo ilipelekea cancer kusambaa mpaka kwenye ini. Niseme nini Mimi?

Baba yangu hakuwa mtu wa kujali hata kidogo, japokuwa taarifa nyingi mama alikuwa anamwambia baba, baba anamjibu jeuri na kuona ana jifanyisha kuumwa. Mama yangu aliumwa sanaa mnooo, nikiwa kidato cha nne mpaka uvumi ukatokea shuleni mama yangu amefariki.

Ila ilikuwa uongo! Niliongea na mama yangu siku mbili mbele na kujua ni mzima.

Nilivyomaliza sikufanya vzuri sana darasani kwasababu muda mwingi niliutumia kulia na kusali bila mafanikio.

Nikiwa nyumbani baada ya kumaliza form four niliona dharau na majibu ya baba wazi wazi bila chenga, mama alikuwa na miradi mingi sana ya kuingiza pesa nasema ni ya mama kwasababu baba alikuwa hafanyi kazi wakati huo na alikuwa akichukua mayai na kuuza huku hela akizinywea pombe na wanawake.

Mama alichoka sana, miradi yote ikayumba na kuisha akiwa amebakiwa na ng'ombe wa maziwa wawili tu pamoja na kazi yake akipata mshahara kiduchu kwasababu ya kuchukua mkopo wa kumalizia nyumba ambayo hakuwahi kuishi.

Niseme nini Mimi? Maisha ya mama yangu yamenifundisha mambo mengi sana mno! Yamenifundisha mengi sana! Mnooo.

Mama aliumwa sana nikiwa kidato cha tano na kabla hajafariki nilifanikiwa kumuona ,mama alikuwa amechoka sana zaidi ya kawaida.. Mama alikuwa amelala kitandani utasema hakuna mtu! Mama alikuwa anaumwa mno.

Nilirudi shule baada ya siku mbili mama yangu alifariki.

Mungu mpumzishe pema.

Ni mengi ila baba alichangia sana kwa kiasi kikubwa mpaka mama anafariki hajawahi oa ni miaka zaidi ya 13. Nalia Mimi nalia sana.

Kaka inauma sana kuona wanawake wanapanda chuki mbayaa juu ilhali wanaume waharibifu ni wachache sana

Kwa mfano binafsi sijawahi kumtenda binti hata mara moja ila mi yamenikuta mara kadhaa na mara zote ex wangu yakimbumia hunirudia kwa vilio ila ndo hivyo forward ever backward never
 
Basi simulizi za namna hii, kuna watu wanazifanya zao. wana beba maumivu ya simulizi wanayafanya yao. Kwa gharama za kusema wamefanyiwa na wanaume wao!!!
 
Hii simulizi imenikumbusha mambo mengi.

Mama yangu alifariki kwa cancer ya ziwa ambayo ilipelekea cancer kusambaa mpaka kwenye ini. Niseme nini Mimi?

Baba yangu hakuwa mtu wa kujali hata kidogo, japokuwa taarifa nyingi mama alikuwa anamwambia baba, baba anamjibu jeuri na kuona ana jifanyisha kuumwa. Mama yangu aliumwa sanaa mnooo, nikiwa kidato cha nne mpaka uvumi ukatokea shuleni mama yangu amefariki.

Ila ilikuwa uongo! Niliongea na mama yangu siku mbili mbele na kujua ni mzima.

Nilivyomaliza sikufanya vzuri sana darasani kwasababu muda mwingi niliutumia kulia na kusali bila mafanikio.

Nikiwa nyumbani baada ya kumaliza form four niliona dharau na majibu ya baba wazi wazi bila chenga, mama alikuwa na miradi mingi sana ya kuingiza pesa nasema ni ya mama kwasababu baba alikuwa hafanyi kazi wakati huo na alikuwa akichukua mayai na kuuza huku hela akizinywea pombe na wanawake.

Mama alichoka sana, miradi yote ikayumba na kuisha akiwa amebakiwa na ng'ombe wa maziwa wawili tu pamoja na kazi yake akipata mshahara kiduchu kwasababu ya kuchukua mkopo wa kumalizia nyumba ambayo hakuwahi kuishi.

Niseme nini Mimi? Maisha ya mama yangu yamenifundisha mambo mengi sana mno! Yamenifundisha mengi sana! Mnooo.

Mama aliumwa sana nikiwa kidato cha tano na kabla hajafariki nilifanikiwa kumuona ,mama alikuwa amechoka sana zaidi ya kawaida.. Mama alikuwa amelala kitandani utasema hakuna mtu! Mama alikuwa anaumwa mno.

Nilirudi shule baada ya siku mbili mama yangu alifariki.

Mungu mpumzishe pema.

Ni mengi ila baba alichangia sana kwa kiasi kikubwa mpaka mama anafariki hajawahi oa ni miaka zaidi ya 13. Nalia Mimi nalia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana Mungu akufute machozi yako. Mama zake wamejua kutulinda sana na wengi wanefichia siri waume zao.
 
Nakubaliana na wewe, shida inaanzia kwenye kuchagua mume wa kukuoa. Vigezo ni mali na pesa wanasemaga mengine watavumiliana mbona hawavumiliani sasa?
kiuhalisia wanawake hatuchagui Bali tunakubaliana na anaekuchagua..
kuna mwanaume mnaweza kuanza vyema kabisa,
akafika katikati mambo yakabadilika kabisa unabaki kujiuliza hivi ni huyu yule ama nimebadilishiwa.
 
Hii ni true story??????
Iddi Makengo
16 hrs ·
STORI YA MAISHA YANGU; MUME WANGU NAOMBA LEO USINIPIGE!
“Mume wangu naomba leo usinipige, nimechoka sana mume wangu, naomba tu usinipige…” Mke wangu aliongea kwa unyonge, alikua amekaa sebuleni kachoka, mimi ndiyo nilikua nimetoka kazini.

“Inamaana unaniona mimi mjinga nakupiga tu bila sababu, kama umefanya kosa utapigwa tu mpuuzi mkubwa! Yaani mume wako anarudi kutoka kazini badala ya kumpokea unaanza kuongea habari za kupigwa! Mbwa mkubwa wewe! Shetani wewe, unataka nijisikie vibaya kuwa nakupiga piga bila sababu!” Nilijikuta nawaka, sijui hasira nilizotolea wapi lakini mke wangu alinitibua, kwa maneno yake nilimfuata na kutaka kumpiga.

Tofauti na siku nyingine mke wangu alikua amekaa tu, nilimsogelea mpaka alipokua kakaa, nikamshika nguo yake na kumnyanyua huu, nilishangaa alikua mwepesi sana, lakini sikujali, nilimsukuma na kumkanyaga tumboni, nikamalizia kwa matusi kadhaa kisha nikaingia zangu ndani. Hakunyanyuka pale alipokua amekaa na wala hakupiga hata kelele.

Sikua nimepanga kutoka, lakini niliona kama mke wangu amenikosea heshima, kaniharibia siku yangu, nilitoka na kumpita pale sebuleni, sikumsemesha kwani nilikua na hasira, nilienda mpaka mezani na kuchukua ufunguo wa gari, gari ya mke wangu.

Ingawa ilikua na jina langu lakini ilikua ni gari ambayo mke wangu alinunua kwa pesa zake lakini baadaye nilimlazimishia akabadilisha jina na kumpa. Nilikua nikiitumia kama yangu, alinunua kwaajili ya kuendea kazini, wakati huo sina kazi lakini nilikua nazurura nayo kufanya umalaya. Hata nilipopata kazi na kuwa na gari la kazini lakini bado nilimnyanyasa, sikumruhusu kuendesha na kama ikitokea anaendesha nilikua nampiga sana.

Niliondoka mpaka kwa Mama mmoja mtu mzima ambaye alikua ni mchepuko wangu wa muda mrefu, naye alikua ananihudumia na mara nyingi alikua akimpigia simu mke wangu kumtukana.
Mimi ndiyo nilikua namuambia, ampigie kumtukana ili mke wangu ajue kuwa mimi ni kidume na si kama yeye anavyonidharau.

Kila siku nilikua naamini kuwa mke wangua nanidharau ndiyo maana nilikua namdhalilisha kila siku. Usiku nilipigiwa simu, ilikua kama saa nane usiku, ilikua ni simu ya Mama yangu, nilishangaa na kuhisi kitu kibaya kimetokea, Baba yangu alikua anaumwa ana hali mbaya Kijijini, nilijua kama Mama ananipigia simu usiku huo basi labda ameshafariki.
“Uko wapi?” Mama aliniuliza baada ya salamu.

“Acha upumbavu, watu wanakutafuta haupatikani, simu umezima ya nini? Inamaana huna taarifa za msiba?” Nilishangaa, simu yangu sikuzima kabisa lakini Mama alikua anasema sipatikani, alitaja msiba nikajua Baba tayari, lakini kwa namna alivyokua anaongea Mama nikama hakuna kitu kimetokea kikubwa.
“Baba amefariki?” Niliuliza kwa kusikitika, nilijifanya kushangaa lakini ukweli ni kitu ambacho wote tulikua tunakisubiria.
“Chunga na mdomo wako! Tema chini! Mama Sadia, Mke wako kafariki! Yaani uasema upo nyumbani hata hujui kama mke wako kafariki?” Nilishikwa na butwaa kwani nilikua sijui chochote.

“Nitakua nimemuua mke wangu!” Niliwaza huku nikinyanyuka na kuvaa nguo, Mama bado alikua anaongea lakini sikujua hata anaongea nini? Niliwaza mambop mengi, niliwaza kuhusu Polisi, nilijua ni mimi, niliwaza labda nilimkanyaga vibaya, niliwaza kuhusu mwanangu Sadia, ndiyo kwanza alikua na miaka mitatu. Baada ya kukaa kwenye ndoa bila mtoto nilishakata tamaa mpaka nilipompata Sadia, kwanza mke wangu alipopata ujauzito nilijua si wangu, nilikua nampiga sana ili mimba itokea lakini Mungu aliniumbua, alikua ni mtoto wakike lakini alifanana kila kitu na mimi, hata ningekataa vipi isingeeleweka.

Nilikua na wasiwasi kuwa si wangu kwani tangu mdogo nilikua na tatizo la nguvu za kiume, nilikua siwezi kufanya mapenzi kwa zaidi ya dakika mbili, nalala na hata goli langu lilikua dhaifu, nlishahangaika kwa waganga mahospitalini kimya kimya kote naambiwa mbegu zangu hazina nguvu. Pamoja na kuujua ukweli lakini siku zote nilikua namshutumu mke wangu, namuambia yeye ndiyo mwenye matatizo nampig na niligoma kabisa kuongozana naye hospitalini, alipopata ujauzito niliukana kwani niliambiwa siwezi kupata mtoto kirahisi kwakua mbegu zangu hazina nguvu.

Nilipewa madawa mengi lakini kila nikipima niliona kama hayasaidii, nikaamua kuacha na kuhamia kwenye pombe na wanawake ili kujione kidume. Baada ya mke wangu kujifungua mwanangu niliacha manyanyaso kidogo, ndoa ikawa na amani lakini nilshazoea, nilikua sina raha, nilikua nahisi kwakua sina nguvu za kiume labda ananidharau, labda ana wanaume wengine, nilikua nampiga sana bila sababu, yaani hata kama akinifumania mimi, kosa ni langu lakini nampiga, sasa alikua amekufa, nilikua nimemuua.

Yule Mama niliyekua natembea naye aliniuliza, nilimuambia mke wangu amekufa kisha nikaondoka. Nilienda mpaka nyumbani nikiogopa, nilimpigia dada wa kazi, alikua analia tu, nikamuambia amtoe mtoto nnje naenda kumchukua. Lengo langu lilikua ni kumchukua mwanangu na kutoroka naye, kwangu ilikua bora kuondoka kuliko kesi ya mauaji. Kila mtu alikua anajua kuwa nampiga mke wangu na nilijua dada wa kazi kaona nikimpiga hivyo kama Polisi wakija basi atahojiwa na mimi nitakamatwa.

Nilifika nyumbani lakini Dada alikua bado hajatoka, niliangalia kulikua na watu wachache, nilitaka kuondoka, lakini kabla ya kufanya hivyo waliniona na kuanza kunipa pole, pamoja na kuwa ilikua usiku watu walikua wanakuja nyumbani kwangu. Nilingia nao, mke wangu alikua chumbani, niliingia na kumuta kama vile kalala..

“Kansa mbaya sana, yaani ziwa lote limeoza, Pole Kaka yangu, mimi sikujua…” Alikua ni Dada yangu, mimi mwenyewe sikujua kama mke wangu anaumwa, niliitikia pole yake na kumuambia atokea nataka kubaki na mke wangu.
Alitoka na kuniacha peke yangu, nilimfuata mke wangu kitandani, nikaamfunia titi moja la kulia lilikua lina kama limeisha flani, huku jingine likiwa limeoza lakini si sana. Nilishangaa kwani ni muda sana sijamgusa mke wangu, tangu ana ujauzito wa mtoto wetu niliacha kutembea naye mpaka alipojifungua.

Nilikua namuambia kuwa ananuka, ameharibika hanivutii lakini ukweli nikuwa nilikua siwezi kufanya mapenzi, hata kwa michepuko mingi niliishia kuilewesha na kuishikashika, sikua na hisia na sikua na nguvu kabisa, hata zile dakika mbili nilikua siwezi tena.

Kumbe baada tu ya kujifungua mke wangu aligundulika kuwa ana Kansa ya titi, alishafanyiwa upasuaji lakini haikusaidia, wakati huo mimi nilikua hapohapo nyumbani lakini sikujua kuwa mke wangu alishawahi kulazwa hospitalini mwezi.

Mara nyingi tu nilikua sirudi nyumbani na kumbe alikua akiwadanganya watu nimesafiri kikazi ili kulinda ndoa yake. Aisee nilipata mwanamke, niliumia sana siku anazikwa, kumbe siku ila ananiambia nisimpige nikuwa alikua anataka kufa kwa amani, mke wangu alifariki nikiwa siji kama anaumwa.

Ndugu walinipa pole, majrani waliniangalia tu kwani walikua wanajua tabia zangu lakini hakuna ndugu hata moja ambaye alijua. Walikua wananilindia siri yangu. Ni mwaka wa kumi sasa tangu mke wangu kufariki, sijaoa mwanamke mwingine, sio kwamba sitaki lakini siwezi, kila mwanamke nineyekua naye nikitembea naye kidogo ananiacha, nina msongo wa mawazo. Wakati Mama yake anafariki mwanangu alikua na miaka mitatu, lakini huwezi amini tangu siku hiyo mwanangu hajakubali nimguse, huwezi amini ni kama alikua anaona mambo yote niliyokua namfanyia Mama yake.

Nakumbuka ilikua ni baada ya kutoka kakaburini, mwanangu alikua analia, watu wakasema mpelekeni kwa Baba yake, walimleta, alilia mara kumi yake, huku akipiga kelele “Hitaki! Shitaki! Shitaki!” Aliongea huku akilia na kujirusha, tangu siku hiyo hakukubali kabisa nimguse. Sasa hivi ana miaka 13, anasoma Dadasa la 6 lakini hanipendi, ananichukia kama vile si Baba yake, Mama yake angekua hai au angekufa akiwa mkubwa ningesema kamuambia mambo mabaya, lakini si hivyo ananichukie tu.

Nafanya kazi, nina kipato kizuri lakini maisha kwangu hayana thamani, sijaoa, nasingizia bado nina uchungu wa mke wangu kumbe nina mengine.

Lakini nawaza je naweza kupata mwanamke mwingine kama mke wangu, pamoja na kujishusha, kujaribu kunipa furaha lakini sikuiona, nilibaki na maumivu yangu tu. Maisha yamekua magumu sana kwangu, natamani kurudisha siku nyuma, angalau niishi kwa amani na mke wangu, nimuonyeshe hata nusu tu ya mapenzi ambayo alikua ananionyesha lakini siwezi, najuta na sijui cha kufanya. Kama una mtu anakupenda na anakuonyesha upendo basi muonyeshe kwelikweli kwani muda wa kuishi hapa duniani ni mchache sana, acha kutumia kwa kuwa na kisirani.

****MWISHO;
Image may contain: 1 person, shoes and outdoor

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiuhalisia wanawake hatuchagui Bali tunakubaliana na anaekuchagua..
kuna mwanaume mnaweza kuanza vyema kabisa,
akafika katikati mambo yakabadilika kabisa unabaki kujiuliza hivi ni huyu yule ama nimebadilishiwa.
Mnachagua maana wanaowachumbia ni wengi....you have wide range of choice
 
kuna baharia mmoja anakwambia uyo mwanamke hakupigwa kwanza jamaa kampiga kiupole sana apo angenunua A.K.A47 ,rungu pamoja na gunia za mkaa kama tatu hivi ndo shughuli ianze sio ivyo alivyo mpiga adi inakela
 
Hii simulizi imenikumbusha mambo mengi.

Mama yangu alifariki kwa cancer ya ziwa ambayo ilipelekea cancer kusambaa mpaka kwenye ini. Niseme nini Mimi?

Baba yangu hakuwa mtu wa kujali hata kidogo, japokuwa taarifa nyingi mama alikuwa anamwambia baba, baba anamjibu jeuri na kuona ana jifanyisha kuumwa. Mama yangu aliumwa sanaa mnooo, nikiwa kidato cha nne mpaka uvumi ukatokea shuleni mama yangu amefariki.

Ila ilikuwa uongo! Niliongea na mama yangu siku mbili mbele na kujua ni mzima.

Nilivyomaliza sikufanya vzuri sana darasani kwasababu muda mwingi niliutumia kulia na kusali bila mafanikio.

Nikiwa nyumbani baada ya kumaliza form four niliona dharau na majibu ya baba wazi wazi bila chenga, mama alikuwa na miradi mingi sana ya kuingiza pesa nasema ni ya mama kwasababu baba alikuwa hafanyi kazi wakati huo na alikuwa akichukua mayai na kuuza huku hela akizinywea pombe na wanawake.

Mama alichoka sana, miradi yote ikayumba na kuisha akiwa amebakiwa na ng'ombe wa maziwa wawili tu pamoja na kazi yake akipata mshahara kiduchu kwasababu ya kuchukua mkopo wa kumalizia nyumba ambayo hakuwahi kuishi.

Niseme nini Mimi? Maisha ya mama yangu yamenifundisha mambo mengi sana mno! Yamenifundisha mengi sana! Mnooo.

Mama aliumwa sana nikiwa kidato cha tano na kabla hajafariki nilifanikiwa kumuona ,mama alikuwa amechoka sana zaidi ya kawaida.. Mama alikuwa amelala kitandani utasema hakuna mtu! Mama alikuwa anaumwa mno.

Nilirudi shule baada ya siku mbili mama yangu alifariki.

Mungu mpumzishe pema.

Ni mengi ila baba alichangia sana kwa kiasi kikubwa mpaka mama anafariki hajawahi oa ni miaka zaidi ya 13. Nalia Mimi nalia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana Wiser, Mungu amemgifafhi mahali salama na siki ys meisho tutaonana naye huko mbinguni kwa Baba.

Wanaume wengi hata humu utawasikia wakijimwambafy kuishi maisha mazuri kila pombe njema, kuhonga wanswake huku kwenye familia zao hata kilo ya nyama hakuna.
 
Mnachagua maana wanaowachumbia ni wengi....you have wide range of choice
Saaaafi jibu mujarabu ambalo hata mimi huwaambia hivyo tatizo wanapenda sana visingizio
WANAUME TULIO WEMA NI WENGI KULIKO WABAYA ILA HATUTAZAMWI KWA UPEO
 
Back
Top Bottom