Tusiwasahau Wazee Kiasi Hik Aisee.

Tusiwasahau Wazee Kiasi Hik Aisee.

Angalau huyo babu watoto wake japo walimnunulia simu,kuna wazee wengine hawana hata simu! Kumpigia ikitokea dharura watampigia tu kuliko kutokua na simu kabisaa!
 
Ujumbe mzuri Mkuu. Japo tunahangaika na maisha inatakiwa tupange muda kuwasiliana na wazee wetu
 
Huko kuwatreat kwake kibabe pengine ndiko kuliko pelekea hao wanae kufanikiwa kimaisha,pengine hakupenda waje kua rege rege! Mwisho wa siku mzazi ni mzazi tu hakuna kitakachombadilisha kwako.

Unachosema ni sahihi kabisa mkuu.
 
Halafu mtu kama huyo akisikia baba yake amekufa unakuta analia msibanu hadi anazimia. na msiba ukiisha anaenda kuchora chata kifuani anaandika i love you dad.

Umenikumbusha binam yangu mmoja aisee mshua wake tumemuuguza kama miezi 6 hivi hajaja kumtazama kila siku anasema ntakuja ntakuja mpaka mshua amefariki akaambiwa akasema nachukua ndege leo leo nakuja.

Na wala hakuwa mbali alikuwa Dom tu hapo lakini amekuja kukuta maiti ya mzee wake ipo kwenye jeneza tunataka kwenda kuizika mkuu. Mpaka sasa hana mbele wala nyuma ana kama 45yrs hana mke wala mtoto muda wote yee na starehe starehe na yeye hana hata cha maana alichokifanya aisee.

Acha tu mkuu.
 
Back
Top Bottom