Tusiwalilie waliokufa tayari. Ni kwa sababu, huyu muuaji (CORONA)tuliyemtishia ati aondoke au abaki kwa heshima ameamua kubaki kwa heshima

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Tusiwalilie waliotangulia, Tusiwalilie waliyowasikia wamekufuta kwasasa,tuwalilie wanaoendelea kupigania maisha yao muda huu. Wengi zaidi wapo mlangoni - kuingia au kutoka ni majaliwa ya Maulana. Basi tuyatunze machozi yetu ili tusiwapunje wengine. Wala tusione ajabu misiba hii mikubwa isipohudhuriwa na viongozi wengi wakubwa, si ajabu. Ni kwa sababu, huyu muuaji tuliyemtishia, ati aondoke au abaki kwa heshima - ameamua kubaki kwa heshima.

Kwanini Raia Mwinyi asifuate nyendo za mwenzake Shein kuitikia kila kitu cha Serikali ya muungano? Ni ukaidi au ujasiri?

Viongozi wengi; wa kisiasa, kiimani na hata viongozi wa kitaaluma wanafuata mkumbo wa Rais wa kumung'unya maneno. Ooh! changamoto za kupumua, uongo mtupu.

Sasa tayari yamekuwa haya ya leo.

Viongozi wachache akiwemo Rais wa Zanzibar wameakataa kumung'unya maneno. Zanzibar inasumbuliwa na janga la Korona, amesema. Tangazo hilo ni sawa na kusema Tanzania inasumbuliwa na janga la Korona kwa sababu Zanzibar ni Tanzania. Pia, hakuna vikwazo vya kusafiri baina ya Zanzibar na Tanzania. Na tangu Rais Mwinyi atangazie dunia juu ya janga la Korona huko Zanzibar, karibu wiki sasa, hakuna jitihada za kuzuia Korona kutoka Zanzibar kuingia bara. Je, ni kwasababu Korona ipo bara muda mrefu?

Na je! baada ya Rais Mwinyi kutangaza kuwa Zanzibar inasumbuliwa na Korona, si wakati sasa wa kukaa na wataalamu ili kujua ni chanjo gani, kutoka nchi gani inafaa kuagizwa ili Wazanzibar wapatiwe chanjo? Hiyo itasaidia ndugu zetu waislamu wenye uwezo wapate nafasi ya kwenda hija. Na sisi Waislamu wa bara itabidi tuzamie tukachanjwe huko Zanzibar ili tukahiji.

Serikali ya Saudi Arabia imepiga marufuku mahujaji kuingia nchini humo bila kupatiwa chanjo katika nchi zao.View attachment 1721466
 
Tusiwalilie waliotangulia, Tusiwalilie waliyowasikia wamekufuta kwasasa,tuwalilie wanaoendelea kupigania maisha yao muda huu. Wengi zaidi wapo mlangoni - kuingia au kutoka ni majaliwa ya Maulana. Basi tuyatunze machozi yetu ili tusiwapunje wengine. Wala tusione ajabu misiba hii mikubwa isipohudhuriwa na viongozi wengi wakubwa, si ajabu. Ni kwa sababu, huyu muuaji tuliyemtishia, ati aondoke au abaki kwa heshima - ameamua kubaki kwa heshima.

Kwanini Raia Mwinyi asifuate nyendo za mwenzake Shein kuitikia kila kitu cha Serikali ya muungano? Ni ukaidi au ujasiri?

Viongozi wengi; wa kisiasa, kiimani na hata viongozi wa kitaaluma wanafuata mkumbo wa Rais wa kumung'unya maneno. Ooh! changamoto za kupumua... uongo mtupu.

Sasa tayari yamekuwa haya ya leo.

Viongozi wachache akiwemo Rais wa Zanzibar wameakataa kumung'unya maneno. Zanzibar inasumbuliwa na janga la Korona, amesema. Tangazo hilo ni sawa na kusema Tanzania inasumbuliwa na janga la Korona kwa sababu Zanzibar ni Tanzania. Pia, hakuna vikwazo vya kusafiri baina ya Zanzibar na Tanzania. Na tangu Rais Mwinyi atangazie dunia juu ya janga la Korona huko Zanzibar, karibu wiki sasa, hakuna jitihada za kuzuia Korona kutoka Zanzibar kuingia bara. Je! Ni kwasababu Korona ipo bara muda mrefu?

Na je! baada ya Rais Mwinyi kutangaza kuwa Zanzibar inasumbuliwa na Korona, si wakati sasa wa kukaa na wataalamu ili kujua ni chanjo gani, kutoka nchi gani inafaa kuagizwa ili Wazanzibar wapatiwe chanjo? Hiyo itasaidia ndugu zetu waislamu wenye uwezo wapate nafasi ya kwenda hija. Na sisi waislamu wa bara itabidi tuzamie tukachanjwe huko Zanzibar ili tukahiji.

Serikali ya Saudi Arabia imepiga marufuku mahujaji kuingia nchini humo bila kupatiwa chanjo katika nchi zao.View attachment 1721466
Mwinyi kapiga chenga kali sana, kachukua ACT kamweka waziri wa Afya ili akitoa tamko ionekane limesemwa na mpinzani.
 
Back
Top Bottom