Tusiwafundishe watoto wetu kuwa na elimu bali kuwa na matumizi ya hiyo elimu

spleen

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
3,224
4,663
Ukienda kwenye shule kubwa kama FEZA,IST ama kwenye vyuo kama MUHAS,hutakosa kuwaona watanzania ama raia wenye asili ya ki"asia"wakisoma kozi kama medicine,dental,nursing ama pharmacy.
Lakini wakimaliza shule hutawaona hao watu wakiomba ajira ama wakipangiwa kwenye hospitali zetu za mikoa,wilaya n.k.

Ukiletewa orodha ya wamiliki wa night club,casino na sehemu kubwa za starehe,70% ni zao wenye asili ya kiasia(wahindi,waarabu etc,) lakini hata siku moja hutamuona muhindi amelewa chakari yupo kwenye club,hutamuona muhindi akicheza kamari,ama akila bata kwa kuhama kiwanja na Alteza yake,kama wafanyavyo vijana wengi wa mjini wenye asili ya kiafrika.

Ni kawaida kwa mwanafunzi aliyesoma sekondari za St Francis na Marian,ama zinazofanana na hizo...na kufaulu vizuri kisha kupata first class chuo,kumuona akiomba kufanya kazi kwenye kampuni za transportaions ama clearing na forwarding za waarabu ama wahindi.

Sijasema elimu sio muhimu,ama kumsomesha mwanao shule za bei apate elimu bora si muhimu la hasha.

Nachopenda kuzungumzia hapa ni "malezi",elimu ya awali ambayo itamsaidia huyo msomi kujitambua na kuitumia hio elimu.

Kuwa na elimu na kuitumia hio elimu ni vitu viwili tofauti. Nigeria ina wasomi wengi wa chuo kikuu kuliko Algeria,lakini ni ndoto ya kila mnaijeria kufanya kazi ama kusoma tena angalau certificate Algeria.

South africa ina wasomi wengi wa phd mara 1000 ya kuwait,ila kuwait dinnar ndio pesa inayoongoza kwa thamani.

Hata ukiwa elimu za juu,ni ngumu sana kukutana na wanafunzi wenye asili ya kiasia,wakiwa na tabia za wizi,umalaya,uzinzi,ulevi,majungu,unafiki,eteti mkute yupo UVCCM au BAVICHA kama sisi ngozi nyeusi.
Unadhani tatizo ni nini?

Tatizo ni wazazi wanatuaminisha tusome tupate elimu,lakini hawatufundishi jinsi ya kuitumia hio elimu. Hata asiyesoma anaweza kuitumia elimu ikamsaidia vya kutosha akamuacha msomi anatanga tanga halijui alitendalo.

Ndio huyo anakuja kuingia mkataba wa madini asilimia 3 kwa 97.Unadhani kwa nini nchi za waarabu madini/mafuta/gesi yanawanufaisha wazawa vilivo?

Jibu ni moja tu;watoto wanafundishwa uthubutu,nidhamu,upendo,tabisa njema etc,so anakua na spirit ya kupambania umma kwa maslahi mapana ya nchi.

Sasa unakuta mwanafunzi wa kiafrika anasoma mechanical engineering yupo chuo anawaza amiliki vitz ya mtumba,lini atakuja kugundua gari yake.

Mwanafunzi anayesoma minerals engineering anawaza jinsi atakavyokula bata akiajiriwa mgodini,kwa nini asiingie mikataba ya kipuuzi ili apate chake mapema.

Ni wajibu wetu wazazi kuwafundisha watoto wetu nidhamu ya maisha. Pablo escobar pamoja na kumfundisha mtoto wake kurithi biashara ya madawa ya kulevya,lakini alifanikiwa kumfundisha mtoto wake madhara ya madawa hayo,kiasi anamiliki labs za kutengeneza lakini haonji(discipline).

hata mtoto umpeleke havard(kama Andrew Chenge), kama hajamfundisha,nidhamu,kujitambua,budjeting,kuona fursa kwa jicho la tatu.....bado hio elimu wajanja wataitumia na kumuacha yeye akizunguka kuacha pesa kwenye bar/night club za watoto waliofundishwa matumizi ya elimu.

MATUMIZI YA ELIMU NI JAMBO KUBWA KULIKO HATA ELIMU YENYEWE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mitaala hii inaandaa wahitimu vihiyo na chama cha majambazi hakitaki kubadili mitaala kwa sababu watanzania wataamka kutoka uzingizini
 
UAE,Bahrain,kuwait,Algeria,morocco wana mitaala gani mizuri ya elimu.
Niamini mkuu malezi yana impact kubwa kwenye kujenga carrier ya mtu
Mitaala hii inaandaa wahitimu vihiyo na chama cha majambazi hakitaki kubadili mitaala kwa sababu watanzania wataamka kutoka uzingizini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio uko sahihi ila awo waAsia na wahindi waliosoma IST na kuambiwa waitumie elimu WAMEANDALIWA MAZINGIRA pia...Refer MODEWJI.

Portfolio | 2020
 
Ni kweli mleta mada malezi n kila kitu

Tatizo linaanzia hapa MITAALA yetu inatuandaa kuwa hvyo unavyosema wewe kuwa tujiajiri? Tukiweza hili nadhan tutakuwa mbali sana

Mwalimu wangu Wa uchumi alinimezesha theory nyiiingi sana lakn maajabu yeye hata kiosk hajawah kuwanacho kimbuka Huyo n prof na anaheshma zake mjin alistaafu lakn akaomba aongezewe muda kama part time job

Fikiria mwalimu kama huyu Wa uchumi ngaz ya PhD anawaza kuajiriwa tena msomi nguli Wa uchumi JE MIMI niliyetoka magagura huko songea ntakuwaje nikimaliza chuo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka mitaala inayofundishwa shuleni itakapobadilika ndio tuna observe shift kwenye attitudes za watu......
 
waafrika wengi ni masikini sasa wewe umetoka kijijini maisha magumu umekuja dar ukapiga chuo umemaliza huna hata mtaji unataka ufanyw nini zaidi ya kuanza kutafuta kazi??

usijifananishe na hao wahindi pesa wamezikuta biashara wanaendeleza tu kama kawaida.


Sent using Jamii Forums mobile app
Walizikuta from nowhere??
Huwezi kuanza kidogo vizazi vyako vikaendeleza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mleta mada malezi n kila kitu

Tatizo linaanzia hapa MITAALA yetu inatuandaa kuwa hvyo unavyosema wewe kuwa tujiajiri? Tukiweza hili nadhan tutakuwa mbali sana

Mwalimu wangu Wa uchumi alinimezesha theory nyiiingi sana lakn maajabu yeye hata kiosk hajawah kuwanacho kimbuka Huyo n prof na anaheshma zake mjin alistaafu lakn akaomba aongezewe muda kama part time job

Fikiria mwalimu kama huyu Wa uchumi ngaz ya PhD anawaza kuajiriwa tena msomi nguli Wa uchumi JE MIMI niliyetoka magagura huko songea ntakuwaje nikimaliza chuo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Prof Lipumba wapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mijitu uataisikia ''sisi tumesoma sana kuliko wale bwana '' waulizo usomi wenu umewasaidia nn? hawana jibu wanabaki kubanga tu kwenye nyumba za hao hao wasiosoma ,kinondoni ,sinza,na magomeni
elimu ya tanzania pumba tupu..we prof ndoto yake awe mwana siasa tu
 
Hivi prof kama lipumba n C.E.O Wa kampuni gan au smeanzisha kampun gan ambayo inaajir watu? Au n C.E.O Wa kudumu CUF
Kuna mijitu uataisikia ''sisi tumesoma sana kuliko wale bwana '' waulizo usomi wenu umewasaidia nn? hawana jibu wanabaki kubanga tu kwenye nyumba za hao hao wasiosoma ,kinondoni ,sinza,na magomeni
elimu ya tanzania pumba tupu..we prof ndoto yake awe mwana siasa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom