Tusiwaamshe, wakiamka hawatolala

Tusiwaamshe, wakiamka hawatolala

Right Marker

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
194
Reaction score
625
Nipo nawaza!!!

Nawaza kuwa muda huu kuna ukumbi mkubwa ambao umejaa watu wa MATAIFA MAKUBWA YALIYOENDELEA. Wameketi kikao, ni kikao cha kujadili MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Nawaza kwamba kikao tayari kimefunguliwa, Mjumbe wa kwanza anapewa nafasi ya kutoa maoni yake kuhusiana na MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA. Lakini huyu Mjumbe wa kwanza anawachokoza wenzake anahoji; "Jamani vipi kuhusu Waafrika naona tumewatenga sana, bado wapo nyuma sana kwenye maendeleo ya Sayansi na Teknolojia".

✍️Bado nawaza!!!
Nawaza kuwa baada ya Mjumbe wa kwanza kuwachokoza wenzake kwa kuwatetea Waafrika, kikao kimeanza kuchangamka. Na sasa ni Mjumbe wa pili anasimama kwa hasira huku uso wake umekunjamana, anamjibu Mjumbe wa kwanza; "Kwahiyo wewe unawapenda sana Waafrika? - Kama unawapenda hamia huko huko Afrika".

✍️Naendelea kuwaza!!!
Kikao kimepamba moto! Mjumbe wa tatu anasimama na kuchangia hoja kwenye mada iliyoanzishwa na Mjumbe wa kwanza, yeye anasema; "Hao waafrika achana nao, tumewapelekea dini ili waendelee kukesha na maombi. Waache wakeshe kwenye nyumba za ibada kisha mchana walale, kamwe hatupaswi kuwaamsha".

✍️Bado mwenzenu nawaza!!!
Upande wa kushoto kuna Mjumbe wa nne ananyoosha mkono ili na yeye aseme jambo, mwenyekiti wa kikao anamruhusu. Mjumbe wa nne anasema; "Tusubiri mapenzi ya Jinsia moja yawatafune Waafrika hata kwa miaka 100, kisha tutawaamsha".

✍️Naendelea kuwaza zaidi!!!
Baada ya mjumbe wa nne kutoa maoni yake, wahudhuriaji wa kikao wote wanacheka kwa sauti 😂. Mwenyekiti anamruhusu Mjumbe wa tano aliyekuwa amenyoosha mkono kwa muda mrefu, na sasa Mjumbe wa tano anasema; "Jamani tusijaribu kuwaamsha Waafrika, wakiamka hawatolala. Hao waafrika wanapenda rushwa, ubakaji, ulawiti, uroho wa madaraka, na uchawi wa kurogana wenyewe kwa wenyewe, hivyo waacheni wachoshane wenyewe".

Ghafla mwenyekiti amebadilika! Anapiga meza kwa hasira kisha anasema; "Hee! Jamani hebu acheni hiyo mada, hiyo si mada iliyotuleta hapa. Waafrika wamelala hivyo tusiwaamshe, wakiamka hawatolala".

✍️Bado nawaza!!!
Mjumbe mwingine anajifanya hajamsikia mwenyekiti, huyu ni Mjumbe wa sita. Anasimama bila kuruhusiwa kisha anasema; "Huyo anayewatetea Waafrika kwani ni kitu gani Waafrika wamenyimwa? Kama ni madini wamepewa, ardhi ya rutuba wanayo, mbuga za wanyama wanazo, bahari imewazunguka, hivyo waacheni wapambane na hali zao".

✍️Bado nawaza!!!
Nawaza kikao kimeamka tena, Mwenyekiti anasimama kwa hasira kisha anawafokea wajumbe; "Hivi nyinyi hamnisikii!! Nimesema acheni haraka hiyo mada. Narudia tena kusisitiza tusiwaamshe Waafrika, wakiamka hawatolala".​

Right Marker
Dar es salaam
 
Back
Top Bottom