Tusiukubali kamwe uhuni huu wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiukubali kamwe uhuni huu wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pdidy, Sep 2, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,313
  Likes Received: 5,643
  Trophy Points: 280
  Tusiukubali kamwe uhuni huu wa CCM

  Maoni ya Mhariri  KATIKA mchakato wa kupata wagombea ubunge na udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa uchaguzi mkuu ujao, kumefanyika uhuni.


  Bila sababu za msingi, baadhi ya watu waliotangaza nia na hatimaye kuomba ridhaa ya wanachama wateuliwe kuwania nafasi za ubunge na udiwani, waliondolewa kwa kigezo cha utata wa uraia.
  Halafu, baada ya kila chama kumaliza utaratibu wa kupata wagombea wao, tumeshuhudia wagombea wa vyama vya upinzani wakienguliwa kwa madai ya utata wa uraia wao.

  CCM ikajipa mamlaka ya Idara ya Uhamiaji, ikawekea pingamizi wagombea wa upinzani wakidaiwa si raia. Wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya wakakubali pingamizi hizo na hatimaye wakawaengua wagombea husika.

  Matokeo yake, ni kuwezesha wagombea wa CCM kubaki peke yao hivyo kupita bila ya kupingwa.
  Tunajua ni jambo la wazi kwamba nchini petu wapo watu wasiokuwa raia lakini wanapata haki kama ni raia. Lakini suala hili linahitaji uchunguzi makini kulithibitisha. Hilo ni jukumu la serikali katika utendaji wake wa kila siku.

  Baadhi yao walitoka Burundi, Rwanda, Waganda na Jamhuri ya Kideomkrasi ya Congo walioingia nchini tangu wakati nchi zao zikiwa kwenye harakati za ukombozi na baadaye zilipokabiliwa na machafuko. Wengi wao walirudi kwao baada ya vita kumalizika na wengine wamebaki hadi leo. Baadhi waliomba na kupewa uraia.

  Lakini hata baada ya kuwa umewekwa utaratibu mzuri wa kuwabaini wageni na kuwaripoti kwenye vyombo vya serikali, kuanzia serikali za vijiji hadi serikali kuu, CCM wameamua kuwapakazia raia wema kuwa si raia kwa sababu tu hawawataki.

  Mbaya zaidi ni kwamba CCM wanakataa nyaraka halali zilizotolewa na serikali inayoongozwa na chama hichohicho na kuwatuhumu watu wazima kuwa si raia.

  Halafu, mgombea ubunge, kwa vile yeye ni waziri, bila ya kutoa uthibitisho, anamtaja mpinzani wake kuwa si raia. Na Wasimamizi wa Uchaguzi wanakubali.

  Iko wapi haki? Hivi ndivyo CCM inavyoendesha nchi. Kiongozi akijisikia kumvua mtu uraia, anafanya hivyo na kuachia mtuhumiwa atoe vielelezo. Huu ni nini kama si uhuni?

  Hatuna sababu yoyote ya kutetea wanaotuhumiwa si raia. Hatukingii kifua si wao tu bali mtu yeyote mwenye uovu. Hiyo si dhamira yetu. Tunajua Watanzania Tanzania ndio wanaostahili kufaidi raslimali tulizojaaliwa kuwa nazo.

  Ardhi, nafasi za ajira na uongozi ndani ya vyama vya siasa na serikali ni kwa ajili ya wananchi wa nchi hii siyo wageni. Wengine watapata kwa kufuata sheria.

  Tunaunga mkono juhudi zote za serikali kubaini wageni haramu, ila tunapinga utaratibu wa kifisadiunaotumiwa na wanasiasa wa CCM kwani unakandamiza demokrasia.

  Ni matukio kama haya yanayosababisha kukosekana amani katika baadhi ya nchi. Tujiulize, waliovuliwa uraia ni raia wawapi? Serikali itawarejesha lini kwao?

  Kama si raia, kwa nini walisubiriwa wakati wa kugombea nafasi za uongozi? Je, watapiga kura? Uchaguzi utahesabika kuwa halali kama wageni hao wameshiriki? Ndiyo maana tunasisitiza tusiukubali kamwe uhuni huu wa CCM
   
 2. b

  bobishimkali Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunapoongelea uongozi ,tunaongelea mustakabali wa taifa letu,hivyo lazima tupate viongozi ambao ni watanzania na siyo watanzania pandikizi .Kumbuka kwamba serikali ina mkono mrefu na inajua mengi kuliko unavyojua wewe na mimi.
   
 3. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  NI kweli Mkuu. Uongozi wa Taifa ni jambo muhimu sana. Tukiachia tukatawaliwa na watu wa nje, tutapoteza utaifa wetu na si ajabu tukafilisiwa umoja na amani tuliyonayo.

  Lakini pia, ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote wanaothibitika kuwa wamevunja sheria za uhamiaji katika nchi yetu. Kusubiri mpaka watu hao wa nje kuomba nafasi za uongozi ndipo tuanze kuwatenga (wakati muda wote wamekuwa maswahiba), si jambo jema. Ni jambo baya zaidi kuhukumu kuwa mtu si raia bila kuzingatia vithibitisho vya uraia. Kufanya hivyo hakuna tofauti yoyote na ukaburu (ubaguzi).
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :mad2:
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kabisa , kwa nchi changa kama Tanzania mkono mrefu wa serikali haufiki mpaka vijijini na vitongojini.Tatizo ni la watanzania wenyewe kutotoa taarifa za hawa wageni, hasa kutoka nchi zenye vurugu kama Somalia.
  Tusijekubali kuwa na viongozi ambao watakuwa "sleeping agents" wa mataifa mengine, ambao watatumika pale mataifa hayo yatakapowahitaji.
   
 6. K

  KIFARU BOMOA Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika mchakato wa kupata wagombea ubunge na udiwani, si vyama vya upinzani pekee walienguliwa, kwa madai ya utata wa uraia wao. Hata CCM wenyewe baadhi ya wagombea tena ni vigogo walie kuwepo siku nyingi, wamekatwa majina yao kwenye NEC kwa swala la uraia. Na wengine walikua na vyeo huko nyuma, tukichukulia kwa mfano: kama mgombea wa jimbo la NZEGA, HUSSEIN BASHE akiambiwa sio raia wakati ni raia na wazazi wake wote ni raia. Hata waziri wa mambo ya ndani amethibitisha. Alipita kwa kura nyingi kwa kumshinda mpinzani wake kwa kura elfu kumi na mbili, lakini aliwekewa pingamizi. Ingekua mtu wa papara angehamia chama kingine. Lakini bado ni mwana chama wa CCM na anapigania haki yake mpaka kieleweke. Huyo ndio mwenye msimamo thabit.
   
Loading...