Tusirudie Makosa ya TAZARA kwenye SGR

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,564
32,206
Wachina walitujengea TAZARA miaka ya 1970s Leo hii shirika linahangaika katika changamoto kadhaa;
1. Kulipa wafanyakazi mishahara ya mwezi kwa mwezi ni mbinde.
2. Senior positions zimekaliwa na wazambia huku watanzania wakiwa kwenye positions za chini
3. Miundombinu kwenye stations nyingi ni chakavu au imerubuniwa ni aibu tupu ukisafiria TAZARA toka Dar mpaka Kapiri Mposhi.

Sasa tumekuja na SGR tumejirekebisha Makosa tuliyofanya TAZARA?
 
Mkuu ungefafanua ili tujue hoja yako ikibidi tuchangie.. Huenda kwa kuiweka wazi hiyo kasoro tutaepuka makosa ya zamani.
 
Sisi lengo letu kubwa ni kuiga Kila wafanyalo Kenya
Fly over inatutoa kamasi wakati Kenya zipo za kutosha. Ma-CEOs/MDs wa leading companies in TZ wanatoka kenya, Kama ni kuiga bado sana.
 
TAZARAni moja kati ya miradi mizuri na mikubwa ambao kama Zambia na Tanzania wangeusimamia vizuri basi ungeleta tija sana...tatizo ni tia maji tia maji..usimamizi mbovu umepelekea huduma mbovu na reli kuonekana haina maana
 
Tungeongea na Rafiki zetu wa damu wachina tuboreshe TAZARA ifike Lusaka mzigo ukipakiwa Dar mteja aupokee Lusaka badala ya Kapiri...dar-moro-dodoma kuna mzigo/abiria wa kutosha?
 
Kuwarahisishia ombaomba njia ya kwenda Dar kutimiza azma yao. Serikali inatakiwa iboreshe kwa kuwekeza zaidi ktk kilimo ili asilimia kubwa ya wananchi wawe na nguvu ya kiuchumi ndio hata hiyo SGR itakuwa na maana.

Tofauti na hapo ni yale yale ya Tazara yatarejea tena. Shirika litaliwa na kufa na majani yataota kwenye mataruma.
 
thinking 1000years ahead is not African culture, Fikra zetu haziwezi hata kuplan ya wiki ijayo..
Unapoanzisha kitu chochote na kama unakitegemea kiwe economical lazima ufikiri miaka mingi mbele na kujenga uwezo wa hiyo miaka mingi mbele..
 
Wagogo na Waluguru wana uwezo wa kuijaza "Treni ya Umeme"?

Wasafiri si waluguru na wagogo tu, kuna watu wanabiashara zao tabora, mwanza, kigoma, shinyanga nk...akifika dodoma mapema manake ataweza kuunga na basi na kuwahi hayo maeneo niliyotaja.
 
Wachina walitujengea TAZARA miaka ya 1970s Leo hii shirika linahangaika katika changamoto kadhaa;
1. Kulipa wafanyakazi mishahara ya mwezi kwa mwezi ni mbinde.
2. Senior positions zimekaliwa na wazambia huku watanzania wakiwa kwenye positions za chini
3. Miundombinu kwenye stations nyingi ni chakavu au imerubuniwa ni aibu tupu ukisafiria TAZARA toka Dar mpaka Kapiri Mposhi.

Sasa tumekuja na SGR tumejirekebisha Makosa tuliyofanya TAZARA?
Mkuu Joshua, bandiko lako ni zuri na hoja ya bandiko hili ni hoja ya msingi sana, Tusirudie makosa ya Tazara kwenye SGR, ambapo kujifunza kwa kutorudia makosa ni kujifunza practical.

Ungetusaidia sana kama ungeyataja hayo makosa ni yapi ili tusiyarudie, hizo hoja tatu za kushindwa kulipa mishahara, uongozi wa wa Zambia, na miundombinu chakavu, sio makosa bali ni matokeo tuu.

Watanzania tuna mtindo wa kulalamikia matokeo badala ya ku deal na chanzo!.

Tatizo kuu la Tazara ni upungufu wa mzigo na uendeshaji.

Bandari ya Dar es Salaam, ndilo tegemeo kubwa na la pekee kwa mizigo ya Zambia, lakini bandari yetu haina uwezo wa ku clear mzigo wote wa Zambia kuishibisha Tazara as a result, treni inalazimika kusubiri for days hadi mzigo ujae, matokeo wenye haraka wanaamua kuwahisha mizigo yao kwa malori kupitia Tunduma. Matokeo ya jumla ni Tazara kukosa mzigo, kukosa pesa za kulipa mishahara, kukosa pesa za ukarabati miundombinu yake, ukijumlisha na matatizo ya uendeshaji, hapo ndipo ilipofikishwa.

Dawa pekee ya kuinusuru Tazara ni kuweka statutory provisions kuwa containers zote za Zambia kupitia bandari ya DSM, zitashushiwa ICD ya Tazara na zitapakiwa direct to Taraza, the collection point ni Kapiri Mposhi.

Ushauri kuhusu SGR yetu umetolewa hapa

Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...

The SGR War: MagufuliKagame vs MuseveniKenyatta ni Vita Kubwa!. Who Will Win, Loose or Its Win Win Situation?.
P
 
Tungeongea na Rafiki zetu wa damu wachina tuboreshe TAZARA ifike Lusaka mzigo ukipakiwa Dar mteja aupokee Lusaka badala ya Kapiri...dar-moro-dodoma kuna mzigo/abiria wa kutosha?
Ukipakia container lako Dar utalipokea popote upendapo Katika S. Africa, Zambia na DR.Congo
Reli hii ilihujumiwa na Frederick Chiluba baada ya kuingizwa madarakani na Wafanya biashara hata mizigo ya Serikali waliacha kutumia Tazara
Kuhusu Menejimenti kyongozwa na Zambia ilikua makubaliano Kwa kua wao ndiyo wasafirishaji wakuu na wako landlocked hivyo nia ilikua kwamba ili kufanya vizuri waongoze wao
Lakini makubaliano baina Marais waliopo sasa hiyo wanaiondoa taratibu.
 
Back
Top Bottom