Tusipowapa heshima, kamwe hawatatuthamini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusipowapa heshima, kamwe hawatatuthamini

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 11, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna wanaume ambao kwa kutokujua wanadhani mwanamke anachohitaji ni ‘fidia’ baada ya kuvunjiwa heshima, hivyo huwa wanawavunjia heshima wake zao na baadae kujitoza ‘fidia’ kwa kuwanunulia zawadi kubwakubwa wanawake hao.

  Wanawake huwa wanapokea zawadi hizi, lakini hii haina maana kwamba ndoa itaendelea kuwa ya amani na upendo. Mwanamke hata kama atapewa dhahabu yote duniani, kama atajua kwamba mumewe hamheshimu, ni wazi kwamba hatakuwa na furaha ya ndoa. Miongoni mwa mambo sita ambayo mwanamke akiyakosa huhisi kutindikiwa na kukosa furaha ya uhusiano ni heshima.

  Kama haki ya mwanamke hailindwi na mwanaume, hata kama kuna kitu gani, ndoa ni lazima itakuwa ni ya kubahatisha. Mwanume anapokuwa na uhusiano wa kipapenzi nje ya ndoa yake, mwanaume anapomzuia mkewe kuamua masuala yake mwenyewe ambayo ni haki yake, kamwe mwanamke hawezi kuridhishwa na hayo na hata kama ndoa imejaa watoto wazuri wenye afya na akili na fedha nyingi zimeipamba nyumba yake.

  Kama mwanaume ataonyesha kutojali kuhusu matamanio au ndoto za mkewe kamwe mwanaume huyo asitarajie kuwa mkewe atakuwa na upendo naye. Mwanamke huwa anatamani sana kuona mumewe anajali na kuyapa uzito matamanio au ndoto za mkewe. Kwa mfano mwanamke anapoonyesha kwamba, angependa kuanzisha shughuli labda ya biashara au wangependa wapate mtoto na mwanaume akaonyesha kutojali kuhusu matamanio hayo, kamwe mwanamke hawezi kutulia na kuwa na amani.

  Kuna vitu au mambo ambayo mwanamke anayahitaji maishani, mahitaji hayo ni mengi yakiwemo yale ya msingi katika maisha na yale ya kawaida. Inatosha kusema kwamba, mwanamke anapogundua kwamba mumewe hajali juu ya mahitaji yake huwa hajisikii vizuri.

  Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba mwanamke huhitaji heshima katika utashi na matamanio yake. Anapogundua kwamba utashi na matamanio yake havizingatiwi na mumewe hawezi hata mara moja kumkubali mume huyo. Kumkubali hapa ina maana ya kumkubali na kumtambua.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa.........
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ulichoandika na mwanaumepia anahitaji heshima kama ilivyo kwa mwanamke, usisemee upande mmoja....
   
 4. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  a + b=c
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  Very very true.......
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,680
  Trophy Points: 280
  I real like this!
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  nakubaliana nawe mkuuu
   
 8. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante, nimeipenda!
   
 9. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi para mbili nimezipenda zaidi.Asante sana mkuu.
   
 10. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli kabisa asante.
   
 11. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Thanx mtambuzi kwa kutambua hayo hapo juu
   
 12. Dinnah

  Dinnah JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  imekaa vizuri, natamani wanaume wengi wapitie humu, tuweze kujenga mahusiano thabiti
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  kweli!
   
 14. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuache bias na nyinyi pia mtuheshima bana lol.
   
Loading...