Tusipotoshe umma: Hakuna aliyetengwa na hayati Magufuli, bali alikataa uhuni wa Ki-CCM ambao haufai kwa manufaa ya taifa

Hawa ndio walifanya sisi wana CCM tusivae sare zetu mtaani tukionekana wahuni kama wao. Sasa wamerudi tena. Sare yangu napigia deki.

Na sasa wamerudi, ile sare yako hata ukipigia deki, na kuacha mlangoni ili watu wajifutie miguuni (bangusilo). Bado unalo tu, majirani wstakuzomea tu.:p:p:p

Washukuru hakuna chama cha upinzani makini.
 
Hata kipindi Cha Magufuri Nani aliipenda CCM ? Ni unafiki na bendera fuata upepo tu. Watu walijikomba ili wasidhuriwe au kupewa vyeo.

Na Magufuri alilijua hili ndio maana akaharibu chaguzi zote mbili za 2019 na 2020.
Magufuli asingekuwa amefanya makubwa nchi na watu kumuonea husda, isingelitumika nguvu kubwa ya kupinga aliyoyafanya. Lakini, kwakuwa dhahabu ni dhahabu, na ukweli ni ukweli, Magufuli ataendelea kuwa Jabali la Maendeleo Tanzania na hao wengine wataendelea kuwa WAHUNI TU!
 
Na sasa wamerudi, ile sare yako hata ukipigia deki, na kuacha mlangoni ili watu wajifutie miguuni (bangusilo). Bado unalo tu, majirani wstakuzomea tu.:p:p:p

Washukuru hakuna chama cha upinzani makini.
Kutokuwa na upinzani makini nchi hii ndio chanzo cha WAHUNI kuringa eti wamerudi!
 
Msoga Gang wanajua politics, na wanafanya politics! Mtu kama Kinana kasomea masters ya politics na mikakati Havard (Chuo namba moja US kama siyo duniani kabisa), utamwambia nini kuhusu uongozi wa kisiasa! JK kapitia jeshi na kwa kipindi kifupi tu alipanda vyeo hadi kuwa Kanali! Hawa Sukuma Gang ni zero kwenye siasa kwenda mbele, ni vile tu jamaa yao aliokota dodo ile 2015 baada ya maugomvi ya akina Lowassa! Ila ujinga wa Sukuma Gang wachache haimaanishi wote wapo hivyo, kuna wengine wapo smart sana tu (eg Angelina Mabula, Biteko na wengineo wengi, waliharibiwa na hizi takataka akina Makonda and company
Nakuunga mkono
 
Mimi najua kabisa bwa mdogo Tindo unakubali kabisa kuwa JPM alijitoa kwa ajili ya taifa letu. Japokuwa malalamiko yako ni juu ya mapungufu yake ambayo sio kama wewe unavyoelezea.
Hayakuwa mapungufu ndugu. Yalikuwa monumental evils. Nakwambia kisa cha watu kufurahi kurudi kwa Boyz2men ni chuki iliyojengwa na mwendazake kwa walio tofauti naye kisiasa, viongozi na watu wa kawaida. Watu wanafurahi kwa kuwa hawa ni lesser evil than SG. Pamoja na kupiga sana lakini tulikuwa tunatazamana. Wakati wa mwendazake chuki kubwa ilijengwa na bado inadumu mpaka Sasa. Uovu huo uliorithiwa toka awamu ya Tano hauwezi hata chembe kufunikwa na flyover au sgr au bwawa la umeme au dreamliner. Watanzania watachukiana kwa muda mrefu kwa sababu ya sera ovu za mwendazake. Hatutapona kirahisi. Ni bora tukose maendeleo lakini nchi iwe inakalika na kila mtu anatoka kwake akiwa hana mashaka kuwa hatarudi.
Na kuonesha kuwa ni wahuni, angalia wanavyotamba na kuringa, hawana habari na wananchi na tembo wanavyotoa machozi wakililia hatima yao.
Asee wacha watambe. Kazi walioifanya kuondoa uovu ule haikuwa ndogo. Uchafu wa udhalilishaji na ukandamizaji wa kikanda nina hakika hautarudi hivi karibu, sio miaka 50 ijayo. Kaka wamekuja wanaojua siasa za kistaarabu so deal with it
 
Akabomoa nyumba na frem zetu kwa falsafa ya kupanua barabara.
Mkuu umenikumbisha! Nakumbuka S. Kubenea aliyekuwa Mbunge wa Ubunge Jimbo la Ubungo alimwomba Mh awafidie au awape kifuta jasho wale watu walio bomolewa nyumba zao kule Kimara/Mbezi (katika mkutano na wakazi wa Kimara) lakini Mh. alikataa kata-kata, kwa uchungu Mh. Mbunge akawataka walio bomolewa zao kutunza nyaraka za nyumba hizo kwa matumaini kwamba huenda akapatikana Rais mwenye HURUMA na akawapatia kifuta jasho. Aidha namkumbusha Mh. Kubenea kuwa sasa tunaye Rais anayependa na kuwajali wana Nchi wake, mama mwenye huruma, tunakuomba uende kwa niaba yao ukawasilishie tatizo hili.ATAKUSIKILIZA
 
Naona kuna propaganda mnaeneza mitandaoni kuwa mlisaidia CCM kupata ushindi 2015 na baada ya uchaguzi mkuu hayati JPM alipokamata madaraka aliwatenga na kuwaona hamfai wakati mlimuweka madarakani.

Acheni kupindisha maneno. Kila mtu anajua mlishazoea masuala ya kihuni ya kupora mali za umma kama mlivyofanya wakati ule kupitia Epa, Escrow, Kagoda na ufisadi mwingi bila aibu.

Mlitaka hayati Magufuli awakubalie uhuni wenu kisa tu mlifanya kampeni basi mfanye ufisadi mnavyotaka?

Sasa hivi kila mtanzania anawafamu vizuri na ndio maana mnapanga safu yenu ili mfanye uhuni wenu vizuri.

Washamba mmeshindwa na watoto wa mjini
Shubamit
 
JPM hajuwatenga, bali wao walijitenga naye.
Je, tumeshasahau kwamba hawa walimtukana JPM na waliomba radhi hadharani?
Kwa msingi huo, nani alikuwa mkorofi?
 
Naona kuna propaganda mnaeneza mitandaoni kuwa mlisaidia CCM kupata ushindi 2015 na baada ya uchaguzi mkuu hayati JPM alipokamata madaraka aliwatenga na kuwaona hamfai wakati mlimuweka madarakani.

Acheni kupindisha maneno. Kila mtu anajua mlishazoea masuala ya kihuni ya kupora mali za umma kama mlivyofanya wakati ule kupitia Epa, Escrow, Kagoda na ufisadi mwingi bila aibu.

Mlitaka hayati Magufuli awakubalie uhuni wenu kisa tu mlifanya kampeni basi mfanye ufisadi mnavyotaka?

Sasa hivi kila mtanzania anawafamu vizuri na ndio maana mnapanga safu yenu ili mfanye uhuni wenu vizuri.



Uhuni wa kopora maduka ya pesa Arusha na kuchukuwa pesa za wafanyabiashara kwenye banks zilifanywa na nani? Tusisifie ujinga Magu alikuwa na mazuri na mabaya yake.

Lakini mmoja baya alikuwa mbaguzi sana. Kama Mbowe alivyosema na kitendo cha kuwarekodi watu kwenye maongezi binafsi alikosea sana sana.
 
Bwashee ongeza sauti wakusikie vizuri. Naona wanajifanya hawajasikia wakati umma wote wa watanzania wanawajua kuwa hawa ni maadui wakubwa wa ustawi wa taifa letu.
 
CCM ndiye adui mkubwa wa maendeleo ya Tanzania.
Wanafanya mabadiliko kwa ajili ya ustawi wa chama chao lakini hawaoni umuhimu na ulazima wa katiba mpya ili kuweka misingi ya uongozi kwa maendeleo ya wote.
Wasipokuja hapa CHAWA wa propaganda za kikejeli kuwa wewe ni "Sukuma gang", naomba nisisikike tena hapa JF.

Ujinga, maradhi, ufisadi, magonjwa na umaskini ni maadui wa maendeleo TZ, lakini CHAWA ni zaidi ya shetani kiuadui.
 
Back
Top Bottom