Tusipotoshane, kulikuwa na sababu za msingi kabisa kwanini Marais waliopita hawakununua ndege kama awamu hii ya tano ilivyofanya

Hiyo ndio sababu ungempa Nyerere kwa nini inatupasa tununue ndege? Kwamba tununue ndege ili tuwaonyeshe watu hatufi kiuchumi pamoja na kuwa sisi ni mojawapo wa mataifa ambayo ni LDC (Least Developed Countries)
Nchi yetu itaendelea kuitwa LDC miaka yote. Jambo la msingi, ni kupambana ili maisha ya meet standards basi.
 
Fast forward to your point: on this century lazma u diversify, watu wansomea field mbali mbali tafaut: nikupe mfano nchi ya marekani, russia, china you name them.. wanawekeza zaidi ya 100B kwenye uvumbuzi wa anga: nkimaanisha nini, moja ya mission zao ni kufanya sayari ya mars kua sehem ya wanadam kuishi, sasa huezi sema sio vipaumbele, thats how the world is moving: huo usafiri haujawahi leta profit ata sku moja katika hizo nchi bali ni part ya research plan yao ambayo kwa mahesabu profit zitakazopatikana mbelen ni kubwa sana:

Kurudi kwenye swali lako, more and more people wanapanda ndege sio kama miaka ya zaman ilikua ni wazungu tu wanapanda ndege, then how can you conclude kulikua na sababu kwanini miaka ya nyuma hwakununua? times are changing.. Tanzania ni nchi ya nne afika nzima tangia hizo usafiri zimekuja: yaani kweli tushika namba nne afrika na hatuna usafiri wa namna hii? watalii wapanda mabasi ya moshi arusha ama?

kuongezea: inaonekana we una mawazo ya kimaskini sana, unawezaje kusema eti ushindan ni mgumu sana, kwamba tumekosa wasomi wa kufanikisha ama? saaahv Dunia sio Tanzania tu, mtu yoyote anaweza kuja kufanya kazi tanzania ama kuwekeza, mtanzania yoyote anaweza kwenda kufanya kazi nje ya nchi, thats how the world is, we are the citizens of the world, sio citizens of Tanzania: so you need to comply with the competition: i can trade in dollars, someone can trade in tsh, sasa tukifuata akili zako si ajira zote zitachukulia na ambao wanaweza ushindani, kusema competition ni ngumu tayar ni akili ya kimaskini
 
Afazali wewe umeongea vizuri na pointi. Na pointi zako ni nzuri sana, kuwa kusema kweli biashara ya usafirishaji wa ndege una CHANGAMOTO si haba.

HATA HIVYO changamoto lazima ziwepo ili kupata namna na njia ya kuzikabili.
Tuige mfano wa Shirika la Ethiopian Airlines. Shirika hili limekuweko na KUONGEZA ndege tangu lilipoanzishwa Desemba 21 Mwaka 1945, na sasa ni miaka 74 lingali KWENYE BIASHARA HII.na linazidi kununua ndege mpya.
Kinachohitajika ni USIMAMIZI bora na UZALENDO wa kuzitunza ndege zetu.

Tukiangalia sanachangamoto tutakata tamaa bure na hivyo si vizuri.
TUZIUNGE mkono JUHUDI zake ili nasi tuwe na shirika lenye nguvu na lenye KUJIENDESHA kwa FAIDA kama lilivo la Ethiopia.
Ama unaonaje mkuu?
Mkuu ni kweli kabisa. Ila sasa mara nyingine lazima uwe unatumia busara na kuwa "pragmatic" katika kufanya maamuzi, usiseme tu mie ni changamoto nitaziweza. Katika ubora wa enzi za Mike Tyson, mwanamasumbwi asiye na uzoefu angekuwa mwendawazimu ikiwa angejitoa kwenda kupambana na Mike Tyson kwa kudai uzoefu na ubora wa Mike Tyson ni changamoto ambazo anakubali kuzikabili.
 
Huwa nachukia sana ninaposikiliza viongozi wetu wakitumia cheap propaganda na kutamba juu ya mafanikio yao kwa kujilinganisha na viongozi waliopita. Kwa mfano, mara kadhaa nimesikia tamko kwamba awamu zilizopita hawakuweza kununua ndege kama awamu ya sasa.

Watu wanaoeneza hizi propaganda huwa hata hawashughulishi ubongo wao kwa kujiuliza kwa nini awamu zilizopita hawakununua ndege kama awamu hii ya tano. Wanasahau kuwa hali za sasa na wakati ule ni tofauti kabisa na kwamba kila raisi anakuwa na vipao mbele vyake, hivyo huwezi kufanya huo ulinganifu.

Tumchukulie Nyerere kwa mfano. Kumbuka wakati fulani, kulikuwa na wimbi la kuanzishwa vituo vya television. Nyerere alipopewa pendekezo la kuanzisha television ya taifa alikataa. Akasema, kwanza ni nani watakaokuwa na uwezo wa kununua television nchini, hawa wakulima na wafanya kazi wetu? Pili akauliza, hizo gharama za kuendesha television ya taifa, tutazimudu vipi pamoja na kuhakikisha inapatikana nchini kote ikiwa radio tu inatupa shida kuna sehemu za nchi inasikika kwa taabu? Kisha akamalizia kwa kusema kuwa na television ya taifa kwa wakati huo hakukuwa jambo la msingi la kupewa kipao mbele, lakini itafika wakati muafaka wa kuwa na television ya taifa. Zanzibar wao walisema wangeanzisha, wakidai gharama yao isingekuwa kubwa kutokana na udogo wa kisiwa.

Sasa fast forward. Katika hali yetu hii ya sasa, fikiria Mwalimu Nyerere ndiye angekuwa Rais wa Tanzania, halafu unatoa pendekezo kwamba Tanzania tununue Dreamliner, Airbus na Bombardier, kwa kuwa fedha za walipa kodi zipo za kuweza kununua ndege hizo. Kumbuka ni Nyerere yule ambae alikuwa akisema ushindani wa kibiashara na mataifa makubwa ni mgumu sana, watatumia kila mbinu kukufanya usifanikiwe na wewe kwa umasikini wako utakuwa huna la kufanya. Hata aliwahi kuuliza, hivi mnafikrir benki yetu ya Taifa NBC inaweza kwenda Uingereza na kufungua tawi pale London ikafanikiwa kirahisi tu? Lakini wao wakitaka kuja kwetu, kwanza wanakupa masharti, ivunje NBC vipande vipande kwanza ili tushindane nayo!

Ni Nyerere huyo huyo, miaka ya 1983 - 85 dhahabu ya Bulyanhulu lipogunduliwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni za Outo Kumpu na Kone Corp aliwakatalia kugawana faida kwa 49% Tanzania na wao 51% akawaambia Tanzania iwe na 51% na wao 49%. Walipokataa akawaambia kama hawataki waondoke, akisema iacheni hiyo dhahabu ikae huko shimoni, kwani itaoza? Akasema wazi wakati muafaka ukifika tutaichimba hiyo dhahabu, hata kama ni vizazi vyetu vijavyo. (Kwa kusikitisha baadae Mkapa alikubali 5%, wala sio ile 49% aliyokataa Nyerere ili tupewe 51%).

Sasa tumia akili zako na za kuambiwa kutambua Nyerere angekupa jibu gani; sawa tukanunue ndege, au hapana si wakati muafaka?

Kwa hiyo kabla ya kufanya hizi cheap propaganda kuwa viongozi huko nyuma hawakununua ndege kama awamu hii, tujiulize kwanza kama hao viongozi wa huko nyuma wangekuwa ndio maraisi leo hii wangenunua ndege au la, na kwa nini.
Hata hivyo viongozi waliotangulia waliwezesha uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya anga na makampuni mengi yalianzisha biashara hiyo ikaipatia serikali kodi. Mifano ni mwingi kama vile Precision Air, fastjet, community Airline, Earthlink, fly 540 na nyingine nyingi kwa gjarama za chinu sana.. Sasa ukitaka kutoka Kigoma kama hujabook Sikh 4-5 has a kuanzia ijumaa mpaka jumatatu utataabika mno.. Achilia mbali gharama kubwa ya nauli.. Na wamemonopolize route ile kwa Air TZ tu..Siku moja ilibidi nikapandie precision baada ya kukosa Air Tz niliyotaka kubook 3 days before.
 
Hizi ndege mbona zinawauma sana?
Nisingependa sana kuongea mambo ya Nyerere ningependa tuongee mambo ya Maendeleo ya SASA ya Awamu hii.
Huyu rais ni perfomer.Period.

UKWELI ni kuwa WALIOMTANGULIA vipau mbele vyao vilikuwa ni vya AVERAGE/WASTANI.
Huyu maono yake yako juu sana. Hasira za nini? Utaumia bure wewe fanya shughuli zako za kimaisha.
Kwa staili hii ya kutaka Mtu hasihoji matumizi ya kodi yake, Tanzania itabaki kiwa maskini wa kutupwa.

Hii yote naona inatokana na kukosa Democrasia, Mtu anasifia mawazo ya Kijinga ya Kiongozi sababu tu anajua yeye ndiyo anagawa vyeo.
 
Hatukatai. Kama ni hivyo basi tuwasikie wakisema wazi kwamba wakati wa Mkapa hadi Kikwee nchi ilikuwa na wezi. Lakini unapokuja kuingiza vitu kama kununua ndege ambavyo havihusiani kabisa na kuwa mtawala bora hapo inabidi ukosolewe. Kununua ndege kwa raisi ni suala la option, sio kwamba maraisi wote waliopita walilazimika kununua ndege wakashindwa hivyo wapimwe mafanikio yao kwa hilo.

Kama lingekuwa suala la ufisadi wakati wa Mwinyi hadi Kikwete, mie nitaunga mkono 100% kwamba Magufuli ameweza sana, lakini sio huu upuuzi wa kwamba hawakununua ndege.
Usisahau, Ufisadi unaousema ulionekana kupitia Report za Wakaguzi wa mali na Matumizi ya serikali.

Kwa hali ya sasa ambayo report hazisomwi kabisa, Unawzaji kusema JPM kafanikiwa kutokomeza Ufisadi???
 
Huwa nachukia sana ninaposikiliza viongozi wetu wakitumia cheap propaganda na kutamba juu ya mafanikio yao kwa kujilinganisha na viongozi waliopita. Kwa mfano, mara kadhaa nimesikia tamko kwamba awamu zilizopita hawakuweza kununua ndege kama awamu ya sasa.

Watu wanaoeneza hizi propaganda huwa hata hawashughulishi ubongo wao kwa kujiuliza kwa nini awamu zilizopita hawakununua ndege kama awamu hii ya tano. Wanasahau kuwa hali za sasa na wakati ule ni tofauti kabisa na kwamba kila raisi anakuwa na vipao mbele vyake, hivyo huwezi kufanya huo ulinganifu.

Tumchukulie Nyerere kwa mfano. Kumbuka wakati fulani, kulikuwa na wimbi la kuanzishwa vituo vya television. Nyerere alipopewa pendekezo la kuanzisha television ya taifa alikataa. Akasema, kwanza ni nani watakaokuwa na uwezo wa kununua television nchini, hawa wakulima na wafanya kazi wetu? Pili akauliza, hizo gharama za kuendesha television ya taifa, tutazimudu vipi pamoja na kuhakikisha inapatikana nchini kote ikiwa radio tu inatupa shida kuna sehemu za nchi inasikika kwa taabu? Kisha akamalizia kwa kusema kuwa na television ya taifa kwa wakati huo hakukuwa jambo la msingi la kupewa kipao mbele, lakini itafika wakati muafaka wa kuwa na television ya taifa. Zanzibar wao walisema wangeanzisha, wakidai gharama yao isingekuwa kubwa kutokana na udogo wa kisiwa.

Sasa fast forward. Katika hali yetu hii ya sasa, fikiria Mwalimu Nyerere ndiye angekuwa Rais wa Tanzania, halafu unatoa pendekezo kwamba Tanzania tununue Dreamliner, Airbus na Bombardier, kwa kuwa fedha za walipa kodi zipo za kuweza kununua ndege hizo. Kumbuka ni Nyerere yule ambae alikuwa akisema ushindani wa kibiashara na mataifa makubwa ni mgumu sana, watatumia kila mbinu kukufanya usifanikiwe na wewe kwa umasikini wako utakuwa huna la kufanya. Hata aliwahi kuuliza, hivi mnafikrir benki yetu ya Taifa NBC inaweza kwenda Uingereza na kufungua tawi pale London ikafanikiwa kirahisi tu? Lakini wao wakitaka kuja kwetu, kwanza wanakupa masharti, ivunje NBC vipande vipande kwanza ili tushindane nayo!

Ni Nyerere huyo huyo, miaka ya 1983 - 85 dhahabu ya Bulyanhulu lipogunduliwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni za Outo Kumpu na Kone Corp aliwakatalia kugawana faida kwa 49% Tanzania na wao 51% akawaambia Tanzania iwe na 51% na wao 49%. Walipokataa akawaambia kama hawataki waondoke, akisema iacheni hiyo dhahabu ikae huko shimoni, kwani itaoza? Akasema wazi wakati muafaka ukifika tutaichimba hiyo dhahabu, hata kama ni vizazi vyetu vijavyo. (Kwa kusikitisha baadae Mkapa alikubali 5%, wala sio ile 49% aliyokataa Nyerere ili tupewe 51%).

Sasa tumia akili zako na za kuambiwa kutambua Nyerere angekupa jibu gani; sawa tukanunue ndege, au hapana si wakati muafaka?

Kwa hiyo kabla ya kufanya hizi cheap propaganda kuwa viongozi huko nyuma hawakununua ndege kama awamu hii, tujiulize kwanza kama hao viongozi wa huko nyuma wangekuwa ndio maraisi leo hii wangenunua ndege au la, na kwa nini.
Musiba sijui kama akisoma hili bandiko ataelewa kitu. MATAGA wanakuambia kabla 2020 haijafika JP ashamaliza kila kitu. Sijui ni mambo gani hiyo aliyomaliza
 
Mambo ya kiuchumi na kiulinzi hayaendi kama unavyo fikiria, kwenye uchumi duni kama wa kwetu ambapo watu wa kuweza kuwekeza haupo ni lazima serikali iwekeze ili kuweza kuchochea maendeleo, kukuza uchumi na kuweka ulinzi wa nchi .mfano huwezi kuacha kununua vifaru kwa sababu kuna sehemu hakuna barabara au maji. Na hata Mwl aliponunua Boeing sio kwamba barabara zote zilikuwa ok, alivyo jenga kiwanda cha taboratex au mutex sio kwamba nchi ilikuwa kamilifu
Unaongea vifaru wakati mjadala ni ndege?

Ushawahi ona hata hivyo vifaru vikinunuliwa?

Tunaongea tunavyoviona.
 
Mnachosahau ni ukweli kuwa Tanzania ya Nyerere ilikuwa na watu wasiozidi milioni 20, leo tunakimbilia milioni 60.

Mnachosahau ni ukweli kwamba Tanzania ya awamu ya kwanza dunia ilikuwa ni ya pande mbili, ile ya kijamaa na ile ya kibepari.

Mnachosahau ni kuwa ujamaa ulikufa rasmi mwaka 1991 na imebakia dunia ya kibepari isiyo na huruma hata kidogo.

Usipokuza sekta ya anga majirani zako hawatahangaika na ujinga wako, wao wataikuza.

Huwwezi ukapewa na Mungu hizi mbuga tulizonazo, mito na maziwa halafu ukakosa shirika imara la ndege ili vivutio hivyo viweze kufikiwa na kila mgeni, hata huyo Mungu atakushangaa!.

Huwezi kuwa na mawazo ya kizamani halafu ukategemea yakupe mafanikio ya leo na kesho.
Marekani yenye watu 400 Million, ina interaction ya watu almost bilion 2 wanaoingia na kutoka marekani.

Serikali haiendeshi shirika la ndege, sekta binafsi ndo inafanya hiyo kazi.

Tanzania kuna mashirika binafsi, kwanini wasifanye hiyo kazi?
 
Watanzania hawajaenda shule. Reasoning kwao ni mtihani.

Ndio maana kila ujinga unasemwa majukwaani na watu wanajichekesha tu.

Miaka nenda rudi mnasoma vitabu kama cha Walter Rodney cha How Europe Underdeveloped Africa. Wakati waafrika wenyewe kwa wenyewe mnanyimana maendeleo.

Unanunua ndege wakati barabara zimekatika watu wamelala njiani, kuna sehemu watu hawana maji safi na salama, elimu duni, afya ndo hohehae.

Hata hao wanaotengeneza hizo ndege hawafanyi hiyo biashara moja kwa moja. Either wananunua hisa kidogo au waachia sekta binafsi ihusike na risk zote wao wanabaki kama regulators.

Usimlaumu beberu kwa ujinga wako wa kukosa maendeleo manake hata Australia, Singapore, Japan, Brazil walitawaliwa kama nyie ila wao wakawa na vipaumbele vinavyomake sense. Wakafika hapo walipo.

Wanasema afrika ni kama jungle. Mnaishi kama wanyama.
Hii ni kwa serikali za afrika na si wenzetu weupe
tapatalk_1571462120452.jpeg
 
Lakini wewe sio mtanzania!
VIPAO MBELE ndio nini kwa mfano?
 
Huwa nachukia sana ninaposikiliza viongozi wetu wakitumia cheap propaganda na kutamba juu ya mafanikio yao kwa kujilinganisha na viongozi waliopita. Kwa mfano, mara kadhaa nimesikia tamko kwamba awamu zilizopita hawakuweza kununua ndege kama awamu ya sasa.

Watu wanaoeneza hizi propaganda huwa hata hawashughulishi ubongo wao kwa kujiuliza kwa nini awamu zilizopita hawakununua ndege kama awamu hii ya tano. Wanasahau kuwa hali za sasa na wakati ule ni tofauti kabisa na kwamba kila raisi anakuwa na vipao mbele vyake, hivyo huwezi kufanya huo ulinganifu.

Tumchukulie Nyerere kwa mfano. Kumbuka wakati fulani, kulikuwa na wimbi la kuanzishwa vituo vya television. Nyerere alipopewa pendekezo la kuanzisha television ya taifa alikataa. Akasema, kwanza ni nani watakaokuwa na uwezo wa kununua television nchini, hawa wakulima na wafanya kazi wetu? Pili akauliza, hizo gharama za kuendesha television ya taifa, tutazimudu vipi pamoja na kuhakikisha inapatikana nchini kote ikiwa radio tu inatupa shida kuna sehemu za nchi inasikika kwa taabu? Kisha akamalizia kwa kusema kuwa na television ya taifa kwa wakati huo hakukuwa jambo la msingi la kupewa kipao mbele, lakini itafika wakati muafaka wa kuwa na television ya taifa. Zanzibar wao walisema wangeanzisha, wakidai gharama yao isingekuwa kubwa kutokana na udogo wa kisiwa.

Sasa fast forward. Katika hali yetu hii ya sasa, fikiria Mwalimu Nyerere ndiye angekuwa Rais wa Tanzania, halafu unatoa pendekezo kwamba Tanzania tununue Dreamliner, Airbus na Bombardier, kwa kuwa fedha za walipa kodi zipo za kuweza kununua ndege hizo. Kumbuka ni Nyerere yule ambae alikuwa akisema ushindani wa kibiashara na mataifa makubwa ni mgumu sana, watatumia kila mbinu kukufanya usifanikiwe na wewe kwa umasikini wako utakuwa huna la kufanya. Hata aliwahi kuuliza, hivi mnafikrir benki yetu ya Taifa NBC inaweza kwenda Uingereza na kufungua tawi pale London ikafanikiwa kirahisi tu? Lakini wao wakitaka kuja kwetu, kwanza wanakupa masharti, ivunje NBC vipande vipande kwanza ili tushindane nayo!

Ni Nyerere huyo huyo, miaka ya 1983 - 85 dhahabu ya Bulyanhulu lipogunduliwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni za Outo Kumpu na Kone Corp aliwakatalia kugawana faida kwa 49% Tanzania na wao 51% akawaambia Tanzania iwe na 51% na wao 49%. Walipokataa akawaambia kama hawataki waondoke, akisema iacheni hiyo dhahabu ikae huko shimoni, kwani itaoza? Akasema wazi wakati muafaka ukifika tutaichimba hiyo dhahabu, hata kama ni vizazi vyetu vijavyo. (Kwa kusikitisha baadae Mkapa alikubali 5%, wala sio ile 49% aliyokataa Nyerere ili tupewe 51%).

Sasa tumia akili zako na za kuambiwa kutambua Nyerere angekupa jibu gani; sawa tukanunue ndege, au hapana si wakati muafaka?

Kwa hiyo kabla ya kufanya hizi cheap propaganda kuwa viongozi huko nyuma hawakununua ndege kama awamu hii, tujiulize kwanza kama hao viongozi wa huko nyuma wangekuwa ndio maraisi leo hii wangenunua ndege au la, na kwa nini.

SSababu ya msingi iliyofanya ndege zisinunuliwe kwa wawamu ya 2-4 ni kwamba Serikali haikuwa na hela ya kununua ndege. Awamu ya kwanza iliwahi kununua ndege kwa hiyo hiyo tuionde. Awamu ya 5 wamenunua ndege zitafikia 11 by 2021, nadhani wao hela labda wanapata kutoka kwa mjomba wetu huko majuu, kwa sababu kama miongo zaidi ya mitatu hatukuwa na uwezo wa kununua ndege, ghafla ndani ya miaka minne hela inapatikana ya kununua ndege zaidi ya 10, hiyo hela imetoka wapi? Na kama ni yetu sisi wenyewe, je huko nyuma hii hela ilikuwa inakwenda wapi? Mimi kila siku najaribu kuwasihi sana watu waiache Serikali ifanye kazi, na kama unaumia kwa kile inachokifanya, basi ngalau kaa kimya, acha bughudha.
 
Swissair
The airline was initially owned by institutional investors (61.3%), the Swiss Confederation (20.3%), cantons and communities (12.2%) and others (6.2%). Swiss also owns subsidiaries Swiss Sun (100%) and Crossair Europe (99.9%). ... Swiss talked to Air France–KLM, British Airways, and Lufthansa.

Alitalia
On 1 January 2015, Alitalia-CAI formally passed its operations to Alitalia-SAI, a new entity owned 49% by Abu Dhabi-based Etihad Airways and 51% owned by the former Italian stakeholders of Alitalia-CAI.

SABENA
In 1989, British Airways and KLM purchased stakes in Sabena, which were later sold back to the Belgian government. In 1993, Air France purchased a large minority stake in Sabena, which it sold soon after. Finally, in 1995, Swissair purchased a 49 percent stake in Sabena and took over management

Etihad
.Etihad Aviation Group is headquartered in Khalifa City, Abu Dhabi and is Government-owned. Etihad Aviation Group retains equity holdings in the following carriers: Etihad Airways (100%); Air Serbia (49%);
 
And that should send a clear warning to all those that think running an airline is just a matter of buying a couple of aircrafts!

Mie Magufuli hata akiniambia atanilipa mara tano ya mshahara wake ili niwe Mkurugenzi wa ATCL sintakubali!

Kagame alimuita aliyekuwa MD wa Ethiopian Airways na kumpa offer kabambe. Ndio ana run Rwandair. Natumaini atafanikiwa.
 
Hebu tuambieni ni wakati gani Nyerere alinunua ndege 12. Ni lini ATC ilikuwa na ndege 12, zaidi sana ya zile ilizorithi toka East African Airways.

Nachokumbuka ATC walikuwa na ndege 2 Boeing 737 baada ya EAA kuvunjika, pamoja na Fokker Frienship. Na moja ya Fokker waliyotumiwa ni ile Nyerere alipewa zawadi nadhani na nchi fulani siikumbuki. Hili la wakati fulani ATC kuwa na ndege 12 zilizonunuliwa na Nyerere wengine tunahitaji kukumbushwa. Hizo ndege 12 zilikuwa zikienda wapi?
Akikujibu hili, naomba na mimi uni tag please; maanake hawa vijana wa sasa hivi yaelekea wao wanajua Zaidi kuliko watu wazima!
 
Back
Top Bottom