Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Huwa nachukia sana ninaposikiliza viongozi wetu wakitumia cheap propaganda na kutamba juu ya mafanikio yao kwa kujilinganisha na viongozi waliopita. Kwa mfano, mara kadhaa nimesikia tamko kwamba awamu zilizopita hawakuweza kununua ndege kama awamu ya sasa.
Watu wanaoeneza hizi propaganda huwa hata hawashughulishi ubongo wao kwa kujiuliza kwa nini awamu zilizopita hawakununua ndege kama awamu hii ya tano. Wanasahau kuwa hali za sasa na wakati ule ni tofauti kabisa na kwamba kila raisi anakuwa na vipao mbele vyake, hivyo huwezi kufanya huo ulinganifu.
Tumchukulie Nyerere kwa mfano. Kumbuka wakati fulani, kulikuwa na wimbi la kuanzishwa vituo vya television. Nyerere alipopewa pendekezo la kuanzisha television ya taifa alikataa. Akasema, kwanza ni nani watakaokuwa na uwezo wa kununua television nchini, hawa wakulima na wafanya kazi wetu? Pili akauliza, hizo gharama za kuendesha television ya taifa, tutazimudu vipi pamoja na kuhakikisha inapatikana nchini kote ikiwa radio tu inatupa shida kuna sehemu za nchi inasikika kwa taabu? Kisha akamalizia kwa kusema kuwa na television ya taifa kwa wakati huo hakukuwa jambo la msingi la kupewa kipao mbele, lakini itafika wakati muafaka wa kuwa na television ya taifa. Zanzibar wao walisema wangeanzisha, wakidai gharama yao isingekuwa kubwa kutokana na udogo wa kisiwa.
Sasa fast forward. Katika hali yetu hii ya sasa, fikiria Mwalimu Nyerere ndiye angekuwa Rais wa Tanzania, halafu unatoa pendekezo kwamba Tanzania tununue Dreamliner, Airbus na Bombardier, kwa kuwa fedha za walipa kodi zipo za kuweza kununua ndege hizo. Kumbuka ni Nyerere yule ambae alikuwa akisema ushindani wa kibiashara na mataifa makubwa ni mgumu sana, watatumia kila mbinu kukufanya usifanikiwe na wewe kwa umasikini wako utakuwa huna la kufanya. Hata aliwahi kuuliza, hivi mnafikrir benki yetu ya Taifa NBC inaweza kwenda Uingereza na kufungua tawi pale London ikafanikiwa kirahisi tu? Lakini wao wakitaka kuja kwetu, kwanza wanakupa masharti, ivunje NBC vipande vipande kwanza ili tushindane nayo!
Ni Nyerere huyo huyo, miaka ya 1983 - 85 dhahabu ya Bulyanhulu ilipogunduliwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni za Outo Kumpu na Kone Corp aliwakatalia kugawana faida kwa 49% Tanzania na wao 51% akawaambia Tanzania iwe na 51% na wao 49%. Walipokataa akawaambia kama hawataki waondoke, akisema iacheni hiyo dhahabu ikae huko shimoni, kwani itaoza? Akasema wazi wakati muafaka ukifika tutaichimba hiyo dhahabu, hata kama ni vizazi vyetu vijavyo. (Kwa kusikitisha baadae Mkapa alikubali 5%, wala sio ile 49% aliyokataa Nyerere ili tupewe 51%).
Sasa tumia akili zako na za kuambiwa kutambua Nyerere angekupa jibu gani; sawa tukanunue ndege, au hapana si wakati muafaka?
Kwa hiyo kabla ya kufanya hizi cheap propaganda kuwa viongozi huko nyuma hawakununua ndege kama awamu hii, tujiulize kwanza kama hao viongozi wa huko nyuma wangekuwa ndio maraisi leo hii wangenunua ndege au la, na kwa nini.