Tusiotumia Vilevi Twende Wapi Kutuliza akili?

MaT2B

JF-Expert Member
Jul 12, 2019
387
969
Hivi ni kwanini Ukienda Pub, Lounge au Bar kama hutumii kilevi wahudumu wanakuona kama Takataka?

Ina maana sisi tusiotumia Vilevi hatutakiwi kupata refreshment.
 
Sio kwamba wanatuona takataka ni kwamba wanatuona wajanja hawawezi kutuibia kizembe, unajua mtu mlevi ni mtu ambaye akili haiko sawa, hivyo kuibiwa na wahudumu ni rahisi, lakini mtu ambaye sio mlevi anakuwa na akili timamu hivyo hawawezi kumuibia , hivyo basi wanafata walevi maana wanaona fursa yakuwaibia
 
Nisaidie locations

Zinaoperate hadi Usiku.?

Maana wengine tunapenda iwe Usiku na muziki taraaatibu.
Kama ni hilo, nunua chakula kama ni kuku, kitimoto, mbuzi, samaki n.k unakunywa na juice yako una enjoy, tatizo mnafika sehemu ya kutumia unanunua maji/soda mwenzako mlevi ameweka bia 20 mezani anazipiga mpaka usiku sana, lazima aonekane mteja wa thamani.

Chakula huwezi rudia sahani 3 labda kama una njaa sana, soda huwezi kunywa 3, kwa hio bado utatumia gharama kidogo tofauti na mnywaji, muachie mhudumu hata tip kidogo uone kama atakudharau, tatizo wanywa soda bahili sana, bar ni sehemu ya kutumia pesaa we unataka kunywa soda ya jero halafu uheshimiwe umekuwa raisi ama? tumia pesaa ikuzoee uheshimike.
 
Hivi ni kwanini Ukienda Pub, Lounge au Bar kama hutumii kilevi wahudumu wanakuona kama Takataka?

Ina maana sisi tusiotumia Vilevi hatutakiwi kupata refreshment.
Nenda psssf COMMERCIAL complex mkabala na mlimani city kila mwisho wa mwezi kuna platform ya stand up comedy,
Ni sehemu nzuri sana ya kurefresh na ipo very smart
 
Sio kwamba wanatuona takataka ni kwamba wanatuona wajanja hawawezi kutuibia kizembe, unajua mtu mlevi ni mtu ambaye akili haiko sawa, hivyo kuibiwa na wahudumu ni rahisi, lakini mtu ambaye sio mlevi anakuwa na akili timamu hivyo hawawezi kumuibia , hivyo basi wanafata walevi maana wanaona fursa yakuwaibia
Nani kakudanganya?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom