Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 6,750
- 14,524
- Thread starter
-
- #21
Kiongozi, kwakweli hiyo ndio hali tunayoishi nayo na inasikitisha.Umezungumza Wataalamu wapo!,nadhani hapo ndio tatizo lililopo kwa jibu lako hapo!!
Kwa nini nasema hivyo, Watanzania bado hatujui nini kilichobomoa utendaji wetu hata wa wataalaam wetu!!
Ndugu, Mayor, kwa hali ambayo tumefikia sio rahisi kuwapata hao wataalaam watakaotupeleka mbele, kama aina ya watoa maamuzi ndio hawa tulionao leo( Wanasiasa) .
Ambacho kipo vichwani kwa binadamu wa Tanzania ni kuchukua chako mapema na julingishia wenzako,
Binadamu walioajilia serikalini sasa hivi , wanaenda kazini ili kuangalia nini cha kuiba leo, sio kufanya kazi tena, sasa huyo mtaalaam atafanyaje kazi ya kitaalaam na kichwani kuna wazo la kuiba tu.
Mungu afanye wepesi, aturudishe kipindi kile cha Nyerere, ambapo mpaka ufikilie cha kuiba au kufanya ufisadi , basi uwe nje ya mfumo wa serikali.
Mwalimu alikuwa kweli anafundisha, Daktari kweli anatibu, polisi ana utu.
Leo Dk anaenda jazini kuiba , Nurse naye anaiba, Mwal hana cha kuiba, lakini anafikiria kazi yake ya bodaboda,
Polisi analala kukuche haraka akamate mtu apewe rushwa, na walivyo na roho mbaya, usipompa rushwa yupo tayari akubambikie kesi hata ya kuua , wala hajali!!
Mkuu wa nchi anawaambie wasaidizi wake waibe lakini kidogo,
Sasa hapo kuna nini,
Nchi inatakiwa Total reform, Mfanyabiashara ndio awe tajili, wewe mfanyakazi wa serikali kuwa tajili , unaupataje huo utajili
Ndio shida. hawa watu wanadhani senior civil service posts ni za kujiamulia tu and bypass the succession planningTatizo kubwa lipo kwenye namna ya serikali inavyofanya kazi, how government works everyday.
Pili, civil service imekuwa set up vipi? kwani kazi kubwa ya civil service ni kuisaidia serikali kusukuma ajenda na pia kuhakikisha malengo ya serikali yanatimizwa katika muda wote wa serikali ile inapokuwa madarakani. Civil Service ni non- ministerial department kama TRA, UDART na department zingine lakini utakuta department hizi zaingiliwa utendaji wake na serikali mara kwa mara.
Pia Department and agencies jukumu lao kuwa ni kuhakikisha sera za serikali zatekelezwa.
Tatu, wenzetu wana public bodies ambazo hufanya kazi independently ili kuisaidia serikali katika maeneo kama mazingira, sheria na kutoa ushauri au uangalizi (monitoring) kwenye maeneo mbalimbali kwa mfano bodo inoangalia mazingira wanokaa wafungwa Inspector of prisons) huyu hutembelea magereza kuangali ubora wa jela hizo na kama kuna mapungufu basi hutoa taarifa yake kwa serikali kupitia waziri anehusika.
Nisitoe maelezo mengi lakini kwa ufupi Tanzania bado sana, ila yawezekana maana kuna mtu aliteuliwa kutoka kuwa mwandishi wa habari kuja kuwa katibu mkuu wa wizara na sidhani kama alipata wapi uzoefu huo.
Kama kiongozi yupo tiyari kusikiliza ushauri basi kinotakiwa ni total reset hadi ground zero.
"Cronyism"Kiongozi, kwakweli hiyo ndio hali tunayoishi nayo na inasikitisha.
Ndio maana kuna sababu luluki ya kupunguza madaraka ya uteuzi wa raisi kwa kujiamulia tu (nafasi za senior civil servants lazima ziwe recommended).
Na senior civil servants lazima wawe na mamlaka ya kupeleka majina sahihi ambayo raisi hawezi teua nje ya hapo kwa sababu wana succession planning zao.
Sio huu utaratibu wa sasa, raisi anajiteulia tu.
To add kwenye mamlaka ya teuzi kuna shida na hakuna uzalendo or else toka nimeanza kufuatilia siasa za Tanzania.
Nimewahi kumsikiliza mtaalamu wa maswala ya elimu akieleza namna ya serikali kupanga idadi ya wasomi kulingana na uchumi wa muda husika, wa kati kulingana na sera na kuandaa wasomi wa baadae kulingana na global trend.
Nimewahi kumsikiliza mtaalamu wa maswala ya natural resources, Prof Muhongo amfikii hata robo.
Nimewahi msikiliza mkurugenzi wa madini kipindi cha JK jamaa alikuwa hatari.
Nimemsikiliza Dorothy Gwajima na Dr Kimei (Kimei nimesoma maandishi yake before he was nobody).
Hizo ni sector ambazo mimi mwenyewe nimezifanyia research kiasi kwamba nikimsikiliza mtu naelewa huyu ni wa level nyingine.
Ndio maana najua kuna wataalamu Tanzania, kwa sababu wote hao niliowataja ni product ya succession planning ya serikali ndio iliyowapa uwezo. Na wapo wengi ambao sijawasikia.
Something is a miss, kwenye mamlaka ya teuzi and it has to change; kwa sababu wenye uwezo wapo.
Na hili tuliiongelea wiki chache tu zilopita.Ndio shida. hawa watu wanadhani senior civil service posts ni za kujiamulia tu and bypass the succession planning
Kama nchi civil service ni shida na usalama makini lazima ujipange kuhakikisha maslahi yao. Europe
Hilo ni somo la katiba yetu mbovu sawa na baadhi ya nchi zilizoendelea ambazo zimezoea utaratibu wa political etiquette na kusahau unaweza pata raisi wa hovyo na kutumia hayo madaraka vibaya.
Sasa sisemi kwetu shida ni Samia tu, huu utaribu mmbovu unamuda toka nianze kufuatilia siasa za Tanzania (personal observation).
Wanahitajika watu makini mamlaka ya teuzi kufanya appropriate succession planning na kuwa consistent.
Hiyo kazi inafanyika tayari, kuna wataalamu Tanzania waliotengenezwa na serikali ukiwasikiliza unapata somo.
Unabaki unajiuliza sasa huyu mbona sio sehemu ya strategic planning na hana nafasi ya maana kwenye civil services.
Halafu unamsikiliza katibu mkuu wa wizara ambae anatakiwa kuwa technocrat au mkurugenzi wa taasisi/idara ya serikali unajiuliza hivi huyu taahira kafikaje hapo.
Something is amiss kwenye mamlaka ya uteuzi.
Kwa wenzetu kufikia nafasi ya senior civil servant sio mzaha, na ukifikia hapo jamaa katika speciality yake kuongea nae ujipange ata kama wewe ni PhD on the subject.
Hizo nchi aziongozwi na watu wa mzaha-mzaha (in their administration).
Jamaa ananijua kupitia ndugu zake achilia mbali vyombo vyake na ugomvi sitaki ndio maana post yangu nikafuta.Hiyo ni moja maana nakumbuka niliposoma huko nyuma nilipitia hii kitu strategic planning zipo stages za kufuata na ukifanya hivyo utaona taasisi yako au organisation ipo poa sana.
Kwa mfano yatakiwa iwe kosa kubwa sana mtu kuteuliwa kisha hapohapo akatenguliwa kwa kuwa amekosa sifa muhimu, je vetting imefanya nini?
Kwahiyo hapo suluhisho ni kuanzisha idara pekee inoshughulika na vetting (national security vetting) inakuwa chini ya katibu mkuu ofisi ya raisi na hii haingalii jina la mtu bali sifa sahihi. Inakuwa na watu professional wenye ujuzi wa kufanya vetting kwa sensitive posts.
Mbili ni sheria kuzingatiwa na kila mtu bila kujali ni nani na sheria hiyo kutojali nani ni mkosaji. Sheria yasema wizi wa mali ya umma ni kosa la jinai na la kimaadili na pia rushwa ni kosa na jinai na pia ni adui wa haki.
Lakini haya yote yahitaji "commitment" kutoka kwa kiongozi na timu yake mara tu baada ya kuapishwa.
Kiongozi ana washauri lakini pia yeye mwenyewe ni lazima awe na washauri personal kuanzia wa kidini na kiroho hadi mshauri wa masuala ya siasa kwamba aelewe siasa ni sanaa, ukiitumia uzuri utaishi kwa amani ila ukiitumia kama fimbo ya kuchapia (vyombo vya dola) wahasimu wako hiyo siyo siasa ni kukomoana kusiko na msingi wowote.
Akiwa na washauri hohehahe basi hukosa mwelekeo mzuri.
Tanzania imeandaa wasomi wa kutosha.Tuna wasomi viazi wa kudesa ndio basic problem, kutatua hili sio uteuzi wala nini ni "education transformation" kwanza kuosha akili zetu vinginevyo turuhusu international employment kwenye sector za msingi kabisa na tuwatumie wageni kujenga uwezo wa watu wetu kwa muda wa miaka kati ya 20-50 kama walivyofanya wengine. Tukiendelea kubaki wabongo na akili zetu hizihizi tutabaki namna hiihii hadi yesu anarudi!
Ok sorry I just realise now, ila this is not harmful is just brainstorming and general discussion no malice.Jamaa ananijua kupitia ndugu zake achilia mbali vyombo vyake na ugomvi sitaki ndio maana post yangu nikafuta.
Japo nina watu wakunitetea ohoo muache namjua; lakini lazima nikubali ugomvi na huyo mjomba kwa nafasi yake. Kwetu tunasema umeyataka mwenyewe siku yakikukuta.
Ndio maana post nimefuta, tuongee jumla jumla.
Tanzania imeandaa wasomi wa kutosha.
Shida ni kutaka watu wa kutumia hao wataalamu na kuwalinda.
Kwa kweli ukiona makatibu wakuu wetu, ni aibu wakati ndiyo think tank ya wizara. Siku hizi ATI think tank ni WaziriBandugu huko Ulaya, hawajafika walipo kwa kubahatisha.
Hizo nchi senior civil servants ni vipanga kweli kweli.
Yaani kufikia uwezo wa kufikiria inabidi usome kweli kweli, hao watu asilimia kubwa ni very very clever.
Africans we need to take knowledge serious.
Hawa jamaa wanazoongoza hizo (senior civil servants) wamesoma, you only have to try reading; halafu ukutane na mtaalamu wa serikali akiongelea hilo jambo ndio ujione bado.
Huwezi kubabaisha mbele ya wazungu, watakuchora tu; hizo nchi aziendeshwi na wababaishaji na hizo jamii hutoboi academically if you don’t match up.
Kwanini naandika hivi, it’s sad kudhani vitu ni rahisi vile duniani; kama watanzania tunavyodhani.
Things don’t work like that huko kwa wenzetu, you can just fake your way in Tanzania and mobilise support.
Sad
Narudia, wizara think tank ni wakurugenzi na katibu mkuu wao. Waziri ni political appointee anatafuniwa na wataalam. Ila kwetu, mh!Mfano hai ni Mtaalam wa Trab n Trat na wenzie kwenye genge la mbuzi hata swali jepesi linalohusu taaluma yake majibu ni USANII mtupu.
Kwa hii mifano, unajichanganya. Inaonesha hujawahi kuwa Civil Servant. Lazima utofautishe managerial position na wataalam.Tunarudi pale-pale mamlaka ya teuzi ni shida.
I agree kuna trained heads huko serikalini, lakini hakuna meritocracy ya uteuzi.
Unakuta mtu ana uwezo hana nafasi au anapokonywa nafasi na mtu ambae hana uwezo kabisa.
Mfano ni vipi Dorothy Gwajima (mtaalamu) alitolewa afya na wizara kupewa Ummy Mwalimu ambae hajui lolote kuhusu hiyo sector.
Au ni vipi Mwigulu Nchemba aliachwa aongee ujinga wa maswala ya uchumi, wakati Kimei ni bank bencher.
OK hizo ni political appointment posts, sasa ni vipi hawa watu (yaani) Mwigulu na Ummy walikuwa wapumbavu vile ambao hakuwa na washauri wa kuwapa nyenzo za kufikia reasoning ya wataalamu waliowakataa.
Utagundua shida sio mawaziri, bali technocrats wa serikali, hata ukiwasikiliza tu. Mfano Kafulila na Nehemia uelewa wao wa maswala ya investment ni mdogo mno.
Kiongozi kwa mwaka unaweza kuwa wahitimu 100,000+ kwa mwaka.Ni kweli tuna wasomi wenye vyeti tu! Jamii yoyote yenye wasomi "wa kutosha" kama ulivyosema haipo kama ya watanzania. Wasomi hawa wanaosubiri kuajiriwa na serikali wote? Ukielimisha watu sawasawa utaona sector mbalimbali zinakua kwa uwiano (balanced) sio sekta ya utumishi tu, wataalam walioelimika wengine wangekuwa busy wanajenga sector binafsi ungeona harakati bila hata kufanya research, wabunifu wangekua wanafanya ubunifu kila eneo.
Tazama China ilivyobadilika miaka ya 80 hadi leo. Yani waliibuka watu wenye elimu ya kati na wakaanzisha biashara, viwanda, mashamba, utafiti, vyuo vya elimu kama uyoga. Leo hii China ni global economic powerhouse sio kwa sababu serikali iliamua bali hao "wasomi" wao. Nasimamia kauli yangu Tanzania haina wasomi ila wakariri madesa.
Ndio shida ilipo, hakuna wataalamu wa strategic planningKwa kweli ukiona makatibu wakuu wetu, ni aibu wakati ndiyo think tank ya wizara. Siku hizi ATI think tank ni Waziri
GirisHon Msigwa?Halafu unamsikiliza katibu mkuu wa wizara ambae anatakiwa kuwa technocrat au mkurugenzi wa taasisi/idara ya serikali unajiuliza hivi huyu taahira kafikaje hapo
Unatakiwa uelewe serikali inavyofanya kazi.Kwa hii mifano, unajichanganya. Inaonesha hujawahi kuwa Civil Servant. Lazima utofautishe managerial position na wataalam.
Nakumbuka wakati wa watu kama Marehemu Kazaura wakiwa makatibu wakuu, Waziri haongei bila kuandikiwa na Katibu Mkuu. Katibu Mkuu anaweza kumsahihisha Waziri.
Nakupa mfano mmoja live, Wakati Doriye ni Katibu Mkuu alimnyima Waziri wake mafuta ya gari ya kwenda katika Jimbo akimweleza kuwa anatoa mafuta kwa ajili ya kazi za mipango TU. Imagine. Leo hii Kuna Katibu Mkuu anayeweza Hilo. Siku hizi Katibu Mkuu ni msaidizi wa Waziri