Tusio na mama tukutane hapa

Tusio na mama tukutane hapa

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,533
Reaction score
3,840
Wakuu,

Leo ni siku ya kina mama duniani, kila inapofika siku kama ya leo sisi tusio na mama tunakua tunapitia katika kipindi kigumu sana. Maana kila mahali watu wanapost wazazi wao na sisi hatuna cha kupost.

Kila siku tunawakumbuka mama zetu lakini siku kama ya leo ni siku ambayo hata kama una roho ngumu unaweza ukalia na kumuuliza Mungu ulimkosea nini mpaka akamuondoa mama yako mapema.

Mama yangu alifariki nikiwa darasa la tano, leo hii namimi ni mzazi lakini pengo la mama halijawahi kuzibwa na chochote kile.

Wito, kama una mama hakikisha unafurahia sana uhai wake. Mfanye awe mwenye kujivunia uwepo wako hata kama huna kitu, napenda namimi ningekuwa na mama yangu lakini haiwezekani tena.

Mama yangu hayupo, baba yangu hayupo, sina wazazi. Naumia sana

Happy mother's day in heaven mom
 
Nikikumbuka mamaangu alivonipenda. Bas tu sikia tu kwa watu yasikukute
 
Mwenyezi Mungu awarehemu akina mama wote waliotangulia mbele ya haki wapumzike salama. Mliopoteza mama zenu jipeni moyo maana ilimpendeza maulana mpevuke mapema na kuikabili dunia kwa jinsi hiyo. "Tushukuru kwa yote"
 
Wakuu,

Leo ni siku ya kina mama duniani, kila inapofika siku kama ya leo sisi tusio na mama tunakua tunapitia katika kipindi kigumu sana. Maana kila mahali watu wanapost wazazi wao na sisi hatuna cha kupost.

Kila siku tunawakumbuka mama zetu lakini siku kama ya leo ni siku ambayo hata kama una roho ngumu unaweza ukalia na kumuuliza Mungu ulimkosea nini mpaka akamuondoa mama yako mapema.

Mama yangu alifariki nikiwa darasa la tano, leo hii namimi ni mzazi lakini pengo la mama halijawahi kuzibwa na chochote kile.

Wito, kama una mama hakikisha unafurahia sana uhai wake. Mfanye awe mwenye kujivunia uwepo wako hata kama huna kitu, napenda namimi ningekuwa na mama yangu lakini haiwezekani tena.

Mama yangu hayupo, baba yangu hayupo, sina wazazi. Naumia sana

Happy mother's day in heaven mom
Kumbe tuko wengi tunao pitia magumu kwa kukosa wazazi wote wawili ...kiukweli kuna siku mtu unalia usiku mzima , unaomboleza ukiwa, ukiwa wa kukosa wazazi wote ni mbaya basi tu, Mama yangu alifariki 2001, baba yangu mwaka jana mwezi wa kwanza , Wazazi wanauma jamani ..mlio na wazazi wapendeni mno. . R.i.p mom and dad ..happy mother's day in heaven.
 
Pole sana mkuu. Tupo wengi tusio na mama. Ila nawashauri wale wenye Mama wasiishie tu kuwaposti mitandaoni, Bali wawajali kwa kuwatimizia haja zao kadri ya uwezo wao.
 
Aaahh mama pumzika Kwa amani huko uliko tunakukumbuka wanao
 
Kumbe!!!!!
Ujinga.
Kama alisha fariki, basi ishakuwa hivyo na maisha lazima yaendelee.

Mtoto mdogo ambae bado anahitaji malezi ya mama ndie anaweza lialia kwa kukosa mama.

Lkn mtu unamiaka zaidi ya 20, na mama alikwisha fariki zama huko, kudeka deka na kulialia ni ushamba na utoto.
 
Dah...poleni sana....ila kichwa cha Uzi kilinishtua sana...nikaja kasi kuona maajabu ya kibaiolojia....
 
Ujinga.
Kama alisha fariki, basi ishakuwa hivyo na maisha lazima yaendelee.

Mtoto mdogo ambae bado anahitaji malezi ya mama ndie anaweza lialia kwa kukosa mama.

Lkn mtu unamiaka zaidi ya 20, na mama alikwisha fariki zama huko, kudeka deka na kulialia ni ushamba na utoto.
Nilikuwa namjibu aliyesama emmyata ndiye kipenzi changu Hajar nimesangaa sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom