Tusikubali tabia ya kumponda Hayati Magufuli ili kujipendekeza/kupitisha ombi kwa Rais Samia

Sasa hivi kila anayeta kujipendekeza au kupitisha ombi kwa Rais Samia lazima aanze na kumponda Hayati Magufuli kwanza halafu ndio anaamini hoja yake itapita kirahisi. Nimekuwa niki-observe Sana hili.

Kila anayetaka kujenga msingi wa hoja fulani lazima aanze na madongo kwa Hayati Magufuli halafu mama anafurahia.

Siyo vizuri kabisa.
Vipi mbona kama kuna kitu unakijua kuhusu Magufuli na hutaki kukisema? Kwani imetokea nini?

Mungu wenu hamtaki kabisa asemwe mmekuwa wapumbavu kabisa why mapungufu yake msikubali halafu turudi kwenye mazuri yake tuyaendeleze?

Mie naona hakuna anayekataa mazuri yake na yanaendelezwa Ila nachokiona ni nyie kujikuta zaidi kumtetea kwenye mapungufu au mabaya yake jambo ambalo tunawashangaa sana.

Anyway kumetokea nini mbona makasiriko?
 
Ila sijui katika chaguzi za 2024 na 2025 watawaambia nibi vipenzi wa JPM ili waweze kueleweka. Makundi ya wamachinga na wachuuzi waliohamishwa katika maeneo ambayo yeye binafsi aliwaruhusu kufanya biashara zao, familia za waathirika wa masoko yanayoungua mara kwa mara, wana CCM ambao walimkubali na kukubaliana naye kwa dhati kuhusu miundombinu yake mingi ya kimkakati, kanda pendwa ambayo sasa wanaikebehi kama Sukuma Gang, acha makundi mengine yenye chuki na Mzee wa Msoga, na kundi jipya lililoibuka la wenye kuchukizwa na serikali kukopa kopa hovyo na mgawanyo wa mkopo ukiwapendelea wale wa pande za Mchambawima.
Kura yao siyo lazima. Usitishie
watu nyau.
 
Wanaofanya hivyo hawakosei mkuu maana wameshasoma uelekeo wa mabosi.

Mabosi wa awamu hii wanabadili kila kitu alichokifanya Magufuli.

Hivyo ili uonekane relevant awamu hii, kandia sana Magufuli utapata unachotaka

Na hii tabia ilianzishwa na CAG kwenye ile ripoti yake iliyojaa kashfa na matusi kwa awamu ya tano.
 
Kura yao siyo lazima. Usitishie
watu nyau.
Sijui upo kundi gani? Wewe ni paka, pusi au nyau? Lakini nahisi kabisa unakipaji ambacho kupitia kwake Mods wanaweza kuanzisha kitufe cha "dislike" ili kiende sambamba na kile cha "like"

Lakini ili watu wakutendee haki kwa uhalisia wake wote, pia kinaweza kuwekwa kingine cha "uvundo" ambacho mimi kwa maoni yangu naona ndicho kinakustahili we mbwiga.
 
Back
Top Bottom