Anaemshauri mwenyekiti wenu wa CCM, njia anayompeleka anampotosha sana. Na nyinyi (Wana CCM pamoja na viongozi wa dini wanaojali matumbo) mnae msifia kila kitu hata akikosea au akiingia chaka, mmempotosha sana.
Mlimfanya aamini kwamba yeye ni mfano wa kuigwa, hata kwa yale aliokua/anayo kosea. Mmempotosha sana.
Picha aliojijengea kichwani kwake (Kutokana na nyinyi kumpotosha) na picha iliopo sasa hivi kidunia (kihalisia) ni vitu viwili tofauti kabisa.
Mmemfanya aonekane kama "ADUI WA DUNIA" anaepingwa kila kona ya dunia na kila kukicha, asie na rafiki wa kweli, ana watu wachache sana wenye kumsifia na kumfanya aamini mambo ambayo hayapo, watu chache wanaojali matumbo yao tu. Kamwe hawezi kusimama "YEYE VS DUNIA", na hawezi kushinda hilo pambano.
Dunia haitajua Polepole au Bashiru au watapia tumbo ndio wanaomshauri kufungia mitandao/kuua/kukandamiza demokrasia/kuvuruga uchaguzi kwa kuiba kura, itajua ni maamuzi na mawazo yake ndio yamefanya yaliofanyika.
Na tunapoelekea, mtaifanye Tanzania iangamie.