Hakuna jamii iliyolala Tanzania kama watu wa kusini

Abuu hanifa

JF-Expert Member
Aug 17, 2021
256
274
Tokea Uhuru hakuma mradi wowote wa maendeleo ulioanzia mikoa ya kusini mwa tz . Kusini imekuwa nyuma na ya mwisho kufikirika ktk kila mradi. Miaka 25 - 30 iliyopita serikali ilijinadi kuwa hauna uwezo was kupoleka maendeleo kwa kila mkoa kwa wakati Mmoja.

Na kwakua ilikuwa ndio miaka 30 tokea Uhuru wananchi was kusini walikuwa na matumaini kuwa Siku zao ya kupelekewa maendeleo. Hata hivyo walikaa tens miaka 20 zaidi ndipo wakaambulia kupata barabara ya lami inayounganishana jiji la dar.

Ule usemi kuwa serikali haihangaiki na jamii zilizo lala nakubaliana nao kwa asilimia zote.

Miradi yote mikubwa ikiwemo hospitali ya rufaa kusini hakuna tokea Uhuru

Chuo kikuu au tawi lake hakuna tokea Uhuru

Kuna mradi huu wa reli SGR kusini hawafikiriwi kabisa wakati kanda nyingine hii wakipelekewa awamu ya pili ya reli. kusini sio tu hawajafikiriwa lkn wenyewe pia hawajitambu, wamelala fofofo.

Ukweli ni kuwa jamii yangu ya watu was kusini wanafurahisha na wanasikitisha na wanahitaji maombi ya haraka kutoka kwa watz.

Wanafurahisha na kusikitisha kwasababu; kusini ndio jamii pekee ambayo ccm inavuma kura nyingi wakati wa uchaguzi na huwa ni watu was mwisho kupelekwa maendeleo na serikali hii ya ccm.


Unaweza kuuliza kuna faida itapatikana ikijengwa reli kusini.

kuna rasilimali na bidhaa muhimu ambayo kama ingesafirisha kwa reli bidhaa hizo zingenuaisha watz walio wengi. Bidhaa hizo no pamoja na cement ambapo kwasasa kina zaidi ya maloli 1000 na hivyo kupelekea barabala ya lami kushindwa kuhimili uwingi na ujazo was maloli endapo kiwanda kingezalisha ktk uwezo wake halisi, kuna makaa ya mawe kuna uranium ambazo michakato ya uzalishaji bado inasuasua. Bila shaka uwepo was reli umgesisimua miradi hii mikubwa.

Jana Mh SSH ameshuhudia utiwaji saini mkopo was pesa kwa ajili ya wa ujenzi wa SGR kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi Tabora chenye urefu wa kilometa 368, kitakachogharimu Dola za Kimarekani 1.908 Bilioni sawa na Sh4.41 trilioni kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Yapi Merkez kutoka Uturuki.

Mkopo huu ambao kwa ujumla wake no zaidi tri 14 watu wa kusini watakuwa in wasindikizaji na walipaji wakuu wa deni hili lisilo na faida yyt kwao.

Sijaja hapa kulia lia kama watz wengine bali huu in Uamsho kwa kwa waliolala fofofo. AMKENI

Huu sio uamsho haya ni malalamiko tu.

Kumuambia mtu kwamba "aisee wewe ni mjinga saaaaana" hapo hujamtoa ujinga bali muambie wewe ni mjinga kwa sababu hii na hii na dawa ya kuondoa fanya kadha wa kadha.

Sasa wewe hujawaamsha lolote bali umewaambia tu kwamba wamelala baaasi.

Weka mikakati namna gani wamelala,weka mikakati wafanyeje ili WATOKE HAPO WALIPOLALA ?

JE waibe ili watoke kwenye huo usingizi fofofo ?
Waingie kwa fujo kwenye siasa ili watoke kwenye usingizi fofofo ?
Wahame wote wahamie Dar ili watoke kwenye usingizi fofofo ?

Wafanyeje mkuu ?
Click to expand...
Ukweli nimechokoza mada hii kwa kuwa Nina njia niliyofikiria ni muarubali wa mabadiliko ktk jamii ya wakusini.

Hata hivyo nilitaka kusikia kutoka kwa wadau wenyewe kabla sijaleta mwelekeo wa njia mpya ya kutembea nayo.

Hadi sasa sijapata wazo mbadala zaidi ya kauli zinazoonyesha unyonge kutoka kwa wadau.

Mwelekeo sahihi.

Chanzo cha tatizo nini:-

Kuelekea kupata suluhisho lazima tujue chanzo kikuu cha tatizo mini, lazima tujue tulipojikwaa na sio tulipoangukia.

Kikwazo kikubwa kimojawapo cha kanda ya kusini kusahaulika ktk masuala maxima ya maendeleo ni kuwa Tanzania ni kubwa na mfuno was serikali kuu hauna na wala hautapata uwezo was kupeleka maendeleo Tanzania yote. Mfumi huu unalazimisha kuwepo ubaguzi kwa baadhi ya kanda.

Kuendelea kukumbatia mfumo huu wa utawala was Serikali kuu kwa jamii ya watu wa kusini, Mfumo ambao ushakuwa mkongwe wa miaka zaidi 60 ya Uhuru. Kuuendelea kuuegemea ni sawa kuupa sapoti mgomba dhaifu ukizaa mkungu mkubwa wa ndizi ili usinguke unazuia na nguzo. Lkn ndizi hizo zikishakomaa hupati manufaa yake. Serikali kwasasa ccm imeelemewa na maitaji ya wa tz. Lkn kubwa zaidi imeelemewa na madeni kiasi kwambainaelekea kuvuka mstari wa kukopesheka.

Mwelekeo
Ni lazima jamii iamke usingizini wa fofofo na ifanye Maamuzi magumu, maamuzi mapya, lkn lazima yafanyike maamuzi magumu. Kwa kuukataa mfumo huu ulioelemewa.

Vyama vyote vinavyoamini mfumo was serikali kuu vikataliwe. Vyama vinavyoamini mfumo wa serikali tatu pia hauna faida kwa wana kusini. Tunahitaji mfumo ule wa kikoloni na baada ya Uhuru. Mfumo wa seriKali za Majimbo ambapo kusini lilijulikana kama Southern Province. Kwa lugha nyepesi lazima wanakusini waunganishe nguvu na kusimama au kuanzisha chama kitakachi amini na kusimamia mfumo wa serikali za majimbo yatakayokuwa na Uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Jambo hili so geni na wala halitakuwa geni. Kwasasa serikali ya ccm imelipatia nguvu na Uhuru zaidi jimbo moja tu la znz. Tunahitaji chama ambacho kitazipa nguvu Majimbo na uhuru was kujiamulia uchumi wao, utamaduni wao, elimu yao, mambo yao ya kijamii nk

kila jimbo lihodhi 75% ya rasilimali zake. 25% ziende serikali kuu kwa ajili ya kujiendesha na kwa ajili ya kusaidoa majimbo yasiyo na rasilimali yajitengenezee artificial rasilimali. Eg elimu maalum kama ya engineering au IT.

Hakuna haja kukumbatia chama Kama bendera kufata upepo. Kipindi Fulani nilikwenda kufanya kijiutatfiti kwa kuwauliza kwann mmetoka CUF na kwenda ACT wengi walijibu tumemfata Maalim . nikawauliza maalim akishinda urais znz jamii ya watu wa kanda ya kusini mtafaidika vp urais wa Maalim Seif (Mungu Amrehemu) hawakuwa na jibu. Hawakuwa na jibu kwa kuwa Maalim seif alijipambanua kuwa anapigania Uhuru zaidi wa znz kujiamulia mambo yao wenyewe.

Ndugu zangu najua wamenielewa lkn watakuja na swali moja kuuliza. Sasa kama tutaipunguzia nguvu serikali kuu sasa hayo madeni ya tri 71 ya serikali kuu atalipa nani!??

Jibu rahisi ni guys mind ur business. Else majimbo husika yaliyonufaika na madeni hayo ndio watakuwa walipaji wakuu. Nawatalipa kulingana na faida kayozaliswa na miradi hiyo.

Ndugu zangu hili wazo linaingia akilini, je linatekelezeka?

R U ready U my fellow guys kufata njia hii
 
Hapo CCM kuvuna Kura tutake radhi, unalijua vibe la CUF kusini? Au bado ulikuwa hujaanza kufatilia siasa? Unawajua chadema tu?
Anyway tulishazoea kubaguliwa tangu enzi za Mwalimu, na reli aliing'oa....kikubwa uhai tu, wote tunavuta pumzi moja.
 
..wekeni jitihada kwenye KILIMO.

..hakikisheni mnayo mazao ya muda mfupi, na muda mrefu.

..kwa mfano, chukulia mfano wa " Mchele wa kyela. "

..angalia jinsi Mbeya ilivyoinuka na kuwa maarufu kutokana na kilimo.

..fanyeni juhudi mikoa ya kusini iwe maarufu kwa kilimo cha zao fulani na kuji-brand kama ilivyo kwa Mbeya.

..eneo lingine la kutiliwa mkazo ni ELIMU.

..MAENDELEO NI WATU SIO VITU.
 
Mleta mada ameona kuandika uzi wake bila kuitaja CCM kutapelekea katibu mkuu wa Chadema aache kumtumia bando na buku ya kula kama anavyowatumiaga wanaharakati wengine. Nchi hii kuna baadhi ya vijana wamekubali kuuza utu wao kwa sababu ya njaa zao.
 
Kuna miradi babu kubwa ni wa ujenzi wa barabara ya lami ya kisasa kabisa kutoka Mtwara hadi Mbambabay ili kuunganisha bandari ya Mtwara na bandari ya Mbambabay yaani Songea Dar kupita Lindi ni lami mwanzo mwisho na kupitia Iringa hiyo siyo ya kuuliza nakufanya mikoa yote ya jirani unavyotoka Songea hakuna vumbi.

Mradi mkubwa mwingine ni ujio wa umeme wa grade ya taifa aisee umeme wa generator umetuweka nyuma sana mkoa wa Ruvuma shukrani za dhati kwa serikali pia miradi kama standi mpya ya shule ya Tanga, mitaa ya mjini kati imepigwa lami.Ila bado serikali ina wajibu mkubwa sana ya kuukumbuka mkoa wa Ruvuma tumeachwa sana.
 
2025 tutaanzisha vuguvugu la kujitenga kuanzia kilwa-jiwe la mzungu Hadi tunduru itakuwa jamhuri ya kusini. Bandari IPO kubwa,madini yapo,kilimo cha biashara korosho kama kawaida,utalii mbuga ya selou IPO yaani tushindwe wenyewe tu
 
Tokea Uhuru hakuma mradi wowote wa maendeleo ulioanzia mikoa ya kusini mwa tz . Kusini imekuwa nyuma na ya mwisho kufikirika ktk kila mradi. Miaka 25 - 30 iliyopita serikali ilijinadi...
Ingependeza zaidi na kusomeka vizuri na kueleweka kama ungeliielezea kwa lugha ya kidplomasia zaidi na pia kichwa cha habari kisichokuwa na ukakasi. Kwanini usingesema tu "Serikali ikumbuke kupeleka miradi ya maendeleo kusini?
 
Hapo CCM kuvuna Kura tutake radhi, unalijua vibe la CUF kusini? Au bado ulikuwa hujaanza kufatilia siasa? Unawajua chadema tu?
Anyway tulishazoea kubaguliwa tangu enzi za Mwalimu, na reli aliing'oa....kikubwa uhai tu, wote tunavuta pumzi moja.
"Kikubwa uhai tu, wote tunavuta pumzi moja".

Kauli kama hii mzee wangu wa Ngunguri yaonyesha hujaridhika na hali iliopo lkn pia huna fikra mpya ya nini kifanyike kuondokana na madhila haya baada ya cuf kusambaratika
 
"Kikubwa uhai tu, wote tunavuta pumzi moja".

Kauli kama hii mzee wangu wa Ngunguri yaonyesha hujaridhika na hali iliopo lkn pia huna fikra mpya ya nini kifanyike kuondokana na madhila haya baada ya cuf kusambaratika
Hizo fikra zitafanyiwa Kazi? Tunasubiri na Sisi tutoe Rais atujengee uwanja WA ndege WA kimataifa, mbuga na mahoteli....Mungu ni wetu sote.
 
Back
Top Bottom