Kukubali kushindwa ni hatua moja ya kuwa mshindi wa kweli. Ni njia ya kujifunza, kukua, na kuona mambo ambayo zamani hukuweza kuyaona.
Katika nchi hii, hakuna chama kikubwa na chenye historia ndefu kama CCM. Tunaweza kukosoa, tunaweza kulalamika, lakini ukweli unabaki kwamba CCM imejenga misingi mingi ya taifa hili. Hata hivyo, pamoja na ukubwa huo, sasa wameanza kufanya makosa yanayoweza kuiingiza nchi kwenye hatari ambayo ikitokea — hakuna CCM, CHADEMA, wala mtu wa dini yoyote atakayeweza kuivumilia.
Taifa letu liko katika hali ngumu. Maandamano yanayoongezeka si ya wakristo pekee; ndugu zetu Waislam pia wapo, bega kwa bega, wote wakiomba haki zao kutoka serikalini. Huu ni ujumbe mzito kwamba kilio hiki ni cha kitaifa, si cha kundi moja.
Katika heka heka hizi, taasisi ya Kikristo ilitoa waraka kama ishara ya kuungana na wanaopigania haki. Badala ya CCM kujibu hoja, kusikiliza kilio cha wananchi, au kutafuta njia ya utatuzi, wameamua kuingiza udini katika mjadala. Hii ni hatari kubwa sana kwa mustakabali wa taifa.
Ndugu zangu viongozi wa dini — msikubali kuingia kwenye mtego huu. Wananchi hawapambani na Uislam. Hawapambani na Ukristo. Wanapambana na taasisi ya kisiasa kutaka haki, uhuru, na mabadiliko mazuri kwa nchi yao.
Tuunge mkono umoja. Tuunge mkono amani. Tusikubali kugawanywa kwa misingi ya dini katika mapambano ya kupata haki zetu kama Watanzania.