Tusihamishie Dodoma kero za Dar es Salaam

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Kero kubwa ya Dar es Salaam kushinda zote ni foleni ndefu za magari kuelekea na kutoka Posta. Shida hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ofisi na huduma nyingi kupatikana mitaa ya Posta.

Je, huko Dodoma kosa kama hili wamelizingatia? Je, ofisi nyingi za serikali zimetawanywa au zote ziko mtaa mmoja?
 
Mmmmh mchumba ya kweli haya?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasomi wetu utadhani hawakusoma, inawezekana hata huko Dodoma hakuna mipango miji inayozingatiwa. Ingekuwa vema baadhi ya ofisi na wizara zikajengwa Tabora, nyingine Morogoro, nyingine Singida, nyingine Kigoma, Kongwa, Msalato, Kibaigwa, Mbeya, Mwanza, Tanga, nk ili kutawanya maendeleo na kurahisishia watu baadhi ya huduma.
 
Mbona unalaumu bila kuwa na ushahidi wa kazi iliyofanyika hadi sasa?..
 
Zimetanyiwa wapi,wakati Ofisi zote za serikali na taasisi zake,zipo Mtumba na ni njia ya Dar

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio ofisi zote...
Hapo ni wizara ambazo kwa sasa baadhi ziko UDOM

Ofisi zingine za umma ziko mjini na kule maeneo ya Hazina ambako si mjini katikati

Dodoma imetawanywa sana kwa maoni yangu
 
Wasomi wetu utadhani hawakusoma, inawezekana hata huko Dodoma hakuna mipango miji inayozingatiwa. Ingekuwa vema baadhi ya ofisi na wizara zikajengwa Tabora, nyingine Morogoro, nyingine Singida, nyingine Kigoma, Kongwa, Msalato, Kibaigwa, Mbeya, Mwanza, Tanga, nk ili kutawanya maendeleo na kurahisishia watu baadhi ya huduma.
Halafu watu wapige perdiem za safari kama hawana akili nzuri?!
 
Perdiem zitapungua Sana kama ofisi zitatawanywa kuliko kila mtu Tanzania nzima asafiri kwenda Dodoma kuhudumiwa. Mfano Wizara ya maliasili na utalii ingekuwa Arusha, Wizara ya madini ingekuwa Mwanza, Wizara ya kilimo ingekuwa Morogoro,SUA
 
Back
Top Bottom