Tusidanganyane, pesa ina mashetani

Tusidanganyane, pesa ina mashetani

Kila kitu ambacho mwanadamu ameweka moyo wake kinashambuliwa sana na ulimwengu wa roho. Shetani anataka akudhibiti kwa kutumia kitu hicho. Ukitaka kuwa na udhibiti wa fedha na mali yakupasa kuwa na uwezo wa kudhibiti ulimwengu wa giza ambao ndio huiba kutoka kwa mwanadamu. Ukiweza hivyo basi fedha na mali vinageuka kuwa baraka na utavitumikisha na sio kuvitumikia. Ukijua siri hii utafurahia sana maisha.
Ebu tufahamishe vzr kuhusu siri hiyo.

#MaendeleoHayanaChama.
 
Why by default pesa isiheshimiwe wakati ndo kitu kinatafutwa na watu daily?
Ni kinyume chake, pesa inapaswa ikuheshimu vinginevyo utasumbuliwa sana na pesa. Hapo ndipo watu wanapokosea.
 
Hakuna kitu kama hicho, ni imani yako tu...mbona hujaelezea wale wanaochukua mikopo na kuinvest na kutajirika?

Wewe umeongelea tu kwa upande wa wanaoshindwa, kuna wengi wanatumia pesa vizuri na kufanikiwa.
na mimi nimemshangaa
 
Vipi kwa wale wanaopata pesa na kwenda kujirusha na michepuko ilihali nyumbani watoto hawajui watakula Nini nao pesa Yao inamapepo????😂😂
 
mkuu pesa ni makaratasi yalopewa thamani ili yatumike katka thaman yakulipia vitu, hapo sijaona ushetani wa pesa...

ushetani unaouhusisha na pesa unakuja hivi binadam anavita kuu na shetani katk ulimwengu huu, lengo la shetani nikumuona mwanadam mwenye dhiki na matatizo kila uchao ndo maana kupitia washirika wake wachawi anatusababishia majanga kila tupatapo pesa...

chakufanya unapaswa umdhibiti shetan ktk ulimwengu wa roho kwa mujibu wa imani yako.

na hii vita ya shetani dhidi yetu ni endelevu hivo mapambano ni yakila siku, hivo unachopaswa kujua mharibifu na mtesi mkubwa wa mwanadam ni shetani na washirika wake.
 
Siri ya pesa anayo tunayempinga kila siku kwenye dini zetu.Nasikia waswaili wanasema aliyegundua pesa alikufa akiwa maskini.
 
Kama ilivyo ardhi na anga

Giza na nuru

Mchana na usiku

Mvua na jua

Vile vile kuna ulimwengu wa roho na ulimwengu wa kawaida wa mwili

Ili kitu kitokee katika ulimwengu wa mwili laZima kwanza kitokee katika ulimwengu wa roho na ukikubali kule kwanza kabla ya kitu hicho kutokea ktk ulimwengu wa mwili..

Watu wengi wanautaka utajiri ktk ulimwengu wamwili lkn ktk ulimwengu wa roho ni either wameukataa wanaona utajiri ni ushetani au wameaminishwa kuukataa na vitabu vya dini toka wapo wadogo au wamefungwa kuwa maskini ktk ulimwengu ule wa roho.
Watu hao watakuwa na juhudi nyingi sana za kuutaka utajiri lkn kamwe hawataupata....

Na itaonekana km wana ukaribia kbs utajiri lkn utawaponyoka kirahisi sana lkn siku watakayomini utajiri sio ushetan,wakaamini wanastahili kuwa matajiri deep down kutoka moyoni basi utajiri utaibuka kama miujiza,pesa zitakuja na kukaa mda mrefu sana bila kuondoka kwa njia za ajabu ajabu

Imani bila matendo ni bure sasa kadri unavyoteseka kuutafuta utajiri km hujafungwa popote pale basi kuna siku moyo wako kwa ndani kabisa utaamini unashahili kiwa tajiri kutokea hapo pesa itakutafuta....

Kuna watu wanaota ubaya kabla haujaja mimi ni mmoja wapo pale unakuta kuna mtu anataka kupanga hatma yangu ktk ulimwengu wa roho ili ije itokee ktk ulimwengu wa mwili
 
Wakuu mmewahi jiuliza mbona mara nyingi tukishika pesa -baada ya muda mfupi majuto yanakua mengi?

Bila shaka pesa ina mashetani.

Ebu fikiria- unachukua mkopo unanunua gari , miezi 3 mingi gari inapinduka na kubaki screper, then unasota kurejesha mkopo kwa miaka 5 uku machungu ukiyasikilizia na familia yako nzima.


Ebu fikiria-unachukua mkopo unafanyia harusi- baada ya 6/12 unasikia wife kakucheat na msela wako, unaamua kumpiga chini na utatembea na stress za maisha

Ebu fikiria- unachukua mkopo unaiingiza pesa kwenye bahashara zako. Baada ya muda si mrefu business partner wako anatoroka na pesa yako yote . Yaan unalala na mtaji wa 15M unaamka na deni la 23M utakalolipa bank kwa muda mrefu. Hapo ukichaa usipokupata utaniambia!

Ebu fikiria- unajichanga unapeleka mtoto shule, akimaliza mhula wa kwanza anatiwa mimba na muuza chips afu anajikataa na kusepa. Kinachofuata Kama mzazi au mlezi unahudumia ujauzito, na pia unakuja kulea mjukuu.


List ni ndefu, nachotaka ukione ni kuwa inakuaje mtu akipata pesa kitakachofuata ni majuto na stress ???

Karibuni wakuu tuchangie mada kwa hoja!!! Pia unaruhusiwa Kuendeleza list ya matukio
Kusema ukweli M/Mungu kukataza riba kupitia vitabu vya
vyake hakukosea. Maana mikopo ya riba huwa na laana na iwapo utachukua basi ni mabalaa juu ya mabalaa yatakuandama.
Mwandishi huo uzi wako kuna wengine watapinga lakini mimi nawaambia wajaribu waone na wajiandae kuchanganyikiwa.
 
Hakuna Pesa Yenye Mashetani
Ila Wengi wetu 90% hatujui matumiz ya pesa we fikiria mru unachukua mkopo wa harusi,biashara,kununua gari huu ni wehu tuu lazima pesa uione ina mashetani
 
Mkuu hela ya mikopo ya RIBA hasa riba ikiwa kubwa limefananishwa na:
1.Kupigana vita na Mwenyezi Mungu
2.Imefananishwa na kuzini na mtu na mamayake.
3.Ufisadi katika jamii
hivyo fedha hizi huwa hazina baraka na matokeo yake utakuta nyumba zinaungua,gari inapata majanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom