Tusibiri kusikia "contradiction" kati ya Ripoti ya CAG na ya Serikali kuhusu Watumishi Hewa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Mkitaka kujua na kuthibitisha kuwa hivi sasa watu wanafanya kazi kwa hofu zaidi kuliko kuzingatia sheria na kanuni za utendaji wao wa kazi,subirini tofauti kubwa kati ya Rpoti ya CAG itakayowasilishwa Bungeni na hii ya Serikali kuhusu Watuhmishi Hewa hasa kwenye hizi Halmashauri za Wilaya ambako zoezi hili limesimamiwa na Wakuu wa Mikoa.

CAG bila shaka atakuwa amefanya kazi yake kitalaamu lakini hawa wengine watakuwa wamefanya kazi kwa hofu na kwa uharaka pasipo umakini na sidhani hata kama taratibu zitakuwa zimefuata kutokana na mashinikizo ya wanasiasa.

Tusubiri.
 
Huu upuuzi wa watumishi hewa ni wakiwango saana, ni aibu kwa chama na serikali miaka nenda rudi ati ndo wanashtuka Leo? kila nikitafakar hainiingii kabisa, Nahis kuna jambo nyuma yake
 
Jambo nyuma yake ni Usanii tu. Mkuu hii movie ya "Watumishi hewa" imepata soko zuri huko Hollywood na Nolywood kiasi ya kwamba inatajwa kupata tunzo Oscar! Magufuli na Angela wamecheza vizuri mno na kupewa tunzo za wasanii bora!
 
Asante hata ile ya kipindupindu ilikuwa ni geresha tu ya wao kukusanya pesa, serikali hii haiishi vioja, mbaya zaidi inapotumia uongo kuaminisha watu,
 
Mwaka Jana au juzi Mwigulu baada ya kuteuliwa kuwa naibu Fefha alikuja na hii single ya mishahara hewa na kusema anadhibiti.
Nakumbuka akabeba sifa nyingi bungeni hata hapa JF, kumbe zilikuwa ngojera tuu hakukua na kitu kinafanyika bali sifa.
Utendaji wa serikali hii ni kama getto tuu
 
Mkitaka kujua na kuthibitisha kuwa hivi sasa watu wanafanya kazi kwa hofu zaidi kuliko kuzingatia sheria na kanuni za utendaji wao wa kazi,subirini tofauti kubwa kati ya Rpoti ya CAG itakayowasilishwa Bungeni na hii ya Serikali kuhusu Watuhmishi Hewa hasa kwenye hizi Halmashauri za Wilaya ambako zoezi hili limesimamiwa na Wakuu wa Mikoa.

CAG bila shaka atakuwa amefanya kazi yake kitalaamu lakini hawa wengine watakuwa wamefanya kazi kwa hofu na kwa uharaka pasipo umakini na sidhani hata kama taratibu zitakuwa zimefuata kutokana na mashinikizo ya wanasiasa.

Tusubiri.
Mkuu si ajabu kuwa na tofauti kati ya CAG na serikali katika namba ya watumishi hewa. CAG katika ukaguzi wake wake wa kawaida huwa anatumia sample na si kufanya 100% of the population lakini Serikali imefanya verification ya 100%.
Ngoja wataalam wa ukaguzi waje watusaidie hapa.
 
Nafikiri hamuelewi vizuri chanzo cha watumishi hewa. Watumishi hewa wanatokana na sababu kuu 3, moja mtumishi kufariki halafu kwa bahati mbaya haondolewi kwenye payrol. Mbili mtumishi kufariki na kwa makusudi haondolewi kwenye payrol, tatu mtumishi kuacha kazi au kuto report kwenye kituo chake cha kazi na mamlaka kutokuchukua hatua za kusimamisha mshahara au kumuondoa kwenye payroll.

Kwa kuzingatia hivyo watumishi hewa wanazalishwa kila mwezi. Hivyo report ya CAG haiwezi kufanana na ya wakuu wa mikoa kwa sababu wamefanya katika vipindi tofauti. Pili CAG anafanyaga sampling siyo 100%.

Hata baada ya uhakiki kufanyika, baada ya miezi miwili kutakuwa na watumishi hewa kibao. Kinachotakiwa ni kuweka utaratibu (business processes) ambazo zitahakikisha mtu anayestahili kuondoka kwenye payrol anaondolewa mara moja. kwa kuwa hili halijafanyika tutegemee fedha kuendelea kupotea kupitia watumishi hewa
 
Mkitaka kujua na kuthibitisha kuwa hivi sasa watu wanafanya kazi kwa hofu zaidi kuliko kuzingatia sheria na kanuni za utendaji wao wa kazi,subirini tofauti kubwa kati ya Rpoti ya CAG itakayowasilishwa Bungeni na hii ya Serikali kuhusu Watuhmishi Hewa hasa kwenye hizi Halmashauri za Wilaya ambako zoezi hili limesimamiwa na Wakuu wa Mikoa.

CAG bila shaka atakuwa amefanya kazi yake kitalaamu lakini hawa wengine watakuwa wamefanya kazi kwa hofu na kwa uharaka pasipo umakini na sidhani hata kama taratibu zitakuwa zimefuata kutokana na mashinikizo ya wanasiasa.

Tusubiri.

CAG hafanyi ukaguzi kwa asilimia 100 kwa hiyo ripoti yake haiwezi kufanana na hizo za wakuu wa mikoa ambao wanahakiki payroll kwa kulinganisha na wafanyakazi binafsi walioko. CAG analinganisha payroll na faili za wahusika, tena anachagua Vipindi tu ili kupata mwelekeo isipokuwa kama kuna tuhuma halisi.
 
Mwaka Jana au juzi Mwigulu baada ya kuteuliwa kuwa naibu Fefha alikuja na hii single ya mishahara hewa na kusema anadhibiti.
Nakumbuka akabeba sifa nyingi bungeni hata hapa JF, kumbe zilikuwa ngojera tuu hakukua na kitu kinafanyika bali sifa.
Utendaji wa serikali hii ni kama getto tuu

Government operations are not static but dynamic.shughuli hubadilika kila siku na wafanyakazi huhamishwa, hustaafu, hufariki nk kwa hiyo ni juu ya wakuu wa idara kuwa na rekodi sahihi kila siku. Waziri au mkuu wa Mkoa hawezi kujua kinachaendelea katika kila idara. Kwa hiyo popote penye wafanyakazi hewa wakuu wa idara ni lazima wakamatwe na kushitakiwa kwa uzembe na walipishwe fedha zilizoibiwa.
 
Hehehe sio kila jambo kupinga
Hiyo single yako sasa inechosha. Lazima kupinga maana nyie mnaona kama hii ni serikali mpya wakati ni ileile ila uongozi wa juu tuu ndio unebadili MTU.
Uzembe huu umekuwepo miaka mingi ndani ya serikali kushindwa kuweka kumbukumbu za watumishi wake sawa.
Wakati hayo yanafanyika kumbuka JPM alikuwa waziri for 20 years, Samoa alikuwa waziri, Majaliwa naye ndani ya Tamisemi jee wakati humo hawakuyaona haya? Au Luna ushahidi gani kuwa walijaribu kuzuia wakakwamishwa?
Ili mambo yaende sawa ni lazima wasemwe sana wasijisahau kama walivyokuwa wamejisahau humo nyuma.
Hiyo tabia ya kuwapamba viongozi wa kiafrika kwa vilemba vya ukoka ndio inayozaa viongozi kama JK, kujisahau na kuacha mchwa wanajula nchi bila huruma
 
Kwahio mlitakaje kwa sasa?
Badilikeni nyie
Kwanzmtambue maana ya Mabadiliko
Pia mtambue changamoto za nchi haziwezi kumalizika
Marekani yenyewe unasikia kila siku watu wakikosoa japo wanatumia Akili kuliko ninyi
 
Hapa sijakuelewa umesimamia wapi, full kujichanganya
 
Back
Top Bottom