Tusianze mwaka na shetani

King Suleiman

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
496
327
Salaam JF, heri ya mwaka mpya.
ndg zangu wapendwa, tumemaliza mwaka 2010 na sasa tumeingia 2011. mwaka 2010 umekuwa wa kihistoria na matukio mengi kwa nchi yetu kama vile uchaguzi mkuu uliokuwa wavuta ni kuvute, huku tukishuhudia kwa mara ya kwanza matumizi makubwa ya fedha wenye kampeni na siasa za majitaka na visasi.
mimi kama watanzania wengine nimeona mambo haya na mengine yamefurahisha baadhi ya watu na mengine yamesikitisha sana ( kama lalamiko la wizi wa kura). mwaka ndio kwanza unaanza ni jukumu letu sote kwa pamoja kuijenga nch yetu bila kujali makundi tuliyojengewa hasa hii isu ya udini (kimsingi haipo, inatengenezwa kwa maslah binafsii na malengo mengine).Ningependa kwa pamoja tushirikiane kwa pamoja kuijenga nchi bila kumkribisha Shetani kama udini, ukabila,visasi na vijembe visivyo na maana.
Jamii Forum, ni jukwaa kubwa sana ktk chi yetu na imekuwa chachu kubwa ya maendeleo, naamini hoja za kijinga na za kebehi kama kuchafuana kipindi cha uchaguzi kutapungua. wale wote vibaraka wa hoja zakijinga (nisingependa kutaja Identity zao kwa sabau wanajulikana) waache sasa kuleleta hoja zao zisizo na mashiko.
ningependa wote tuwe na umoj kwa yafuatayo:-
1.katiba mpya
2.tumehuru ya uchaguzi
3.uhuru zaidi wa vyombo vya habari
4.uwajibikaji wa serikali mpaka kwenye shina

ndg zangu wana jamvi haya ni maoni yangu mwenzenu Suleiman wakati huu wa kuuanza mwaka huu mwema 2011, ningependa mnikosoe kama nimeptoka na kuongezea maoni yenu mazuri bila kebehi na kuonyesha mabadilko yetu tangu sasa.
HERI YA MWAKA MPYA,
wadau nawakilisha.
 
heri ya mwaka mpya.. binafsi nimefaidika na mawazo, maoni na taarifa mbalimbali hapa JF. aidha nimekutana na watu wengi ambao tumekuwa marafiki.. kuna members wengi wameni-inspire katika mambo mazuri wanayoyafanya kwa maisha yao binafsi na kwa jamii.. aidha namshukuru mungu kwamba nimeweza kuiga mazuri ambayo wenzangu wamenimegea....
pia kikubwa nilichojifunza ni kuwa katika JF tujitahidi kutembelea forums mbalimbali zaidi ya forum maarufu ya siasa. kwa mfano mimi nimefaidika sana na forum ya BUSINESS..
tunapoingia mwaka mpya ni vema tukafanya tathmini nini kimeenda vema na kipi kinatakiwa kurekebishwa katika maisha binafsi na ya taifa hili kwa ujumla.. changamoto ninayotoa katika 2011 ni kuwa before changing the world, please change yourself. secondly tukiungana katika masuala mbalimbali tutaweza kushinda kwani kidole kimoja hakiwezi kuua chawa..
ngoja nizidi kumuomba mungu aweze kunivusha maana zimebaki dk 4 tu... happy new year 2011 all.
 
thanks Dreamer, heri ya mwaka mpya pia. naamini mwaka huu ni wa mafanikio ya kifikra na kimaendeleo.
 
heri ya mwaka mpya.. binafsi nimefaidika na mawazo, maoni na taarifa mbalimbali hapa JF. aidha nimekutana na watu wengi ambao tumekuwa marafiki.. kuna members wengi wameni-inspire katika mambo mazuri wanayoyafanya kwa maisha yao binafsi na kwa jamii.. aidha namshukuru mungu kwamba nimeweza kuiga mazuri ambayo wenzangu wamenimegea....
pia kikubwa nilichojifunza ni kuwa katika JF tujitahidi kutembelea forums mbalimbali zaidi ya forum maarufu ya siasa. kwa mfano mimi nimefaidika sana na forum ya BUSINESS..
tunapoingia mwaka mpya ni vema tukafanya tathmini nini kimeenda vema na kipi kinatakiwa kurekebishwa katika maisha binafsi na ya taifa hili kwa ujumla.. changamoto ninayotoa katika 2011 ni kuwa before changing the world, please change yourself. secondly tukiungana katika masuala mbalimbali tutaweza kushinda kwani kidole kimoja hakiwezi kuua chawa..
ngoja nizidi kumuomba mungu aweze kunivusha maana zimebaki dk 4 tu... happy new year 2011 all.
nimependa mawazo yako, nakutakia 2011 yenye mafanikio
 
Back
Top Bottom