Tushirikishane hili, nimeichukua mahali flani

goodhearted

JF-Expert Member
Feb 15, 2015
943
1,110
MUHIMU KWA MUSTAKABALI WA AFYA YAKO SOMA !!!

Azam company ni kampuni inayorisha Watanzania na nchi nyingi kusini mwa jangwa la Sahara. Mzee wetu huyu amekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania na nchi jirani zinazotuzunguka kupitia huduma mbali mbali anazotoa kuanzia usafiri wa majini, vyakula hata vinywaji. Sitasita kumpongeza mzee wetu kwa huduma zako na Mungu atakulipa kwa ili.
Kilichonifanya nikujadili hapa mzee ni hiki kinywaji chako kipya , Watanzania wamekipokea na wanakitumia sana kifupi kinauzika huu ndio ukweli . Na mimi kama miongoni mwa wateja wake nikajaribu kukionja kutaka kujua kina ladha gani kinywaji hiki ?? Kinywaji hiki kinaitwa ‪#‎ENERGY‬ ‪#‎DRINK‬.Baada ya kufungua na kuonja kwa mara ya kwanza kilinishinda kurudia fundo la pili nikajua labda huenda ni gesi ngoja nikiache kwa muda kidogo, lakini hata baada ya kukirudia tena bado kilinishinda.
Nikajikuta navutiwa kusoma kimeungwa kwa kutumia viungio gani(ingredients) hiki nilichokiona ndicho kilichonifanya niandike haya , malengo sio kuharibu biashara yako la ni kuwajuza Watanzania ambao wengi wetu lugha iliyotumika hapa ni changamoto kuijua , lakini pia wengi wetu huwa hatuna utamaduni wa kusoma hivi vibandiko kabla ya kutumia .NI NINI NILICHOKIONA NA KIKANISTUA?? HIKI HAPA !!
1.INGREDIENTS(VIUNGIO)
Water sugar, Carbondioxide,Citric acid,(E330), Taurine, Acidity Regulator Sodiumcitrates E331,Colour plain , Caramel E150a,‪#‎CAFFEINE‬, Inositol,Preservative Potassium Sorbate E 202,Flavouring,Niacin,Pantothenic Acid, Vitamin B6, B12
Baada ya kuandikwa hivi viungia ukiangalia katika chupa hii kilichofatiwa ni muda wa matumizi na mahali kinapozalishwa. Lakini bado sikupata mantiki kwanini kimekuwa kikali mno kwanini!!!!
GHAFRA katika kudadisi zaidi ndipo chini ya maandishi hayo nikakuta maandishi mengine mapya tena yamewekwa juu ya wino‪#‎MWEKUNDU‬# kuashiria TAHADHALI bila kuandikwa neno lenyewe la TAHADHALI
Maandishi haya yameandikwa katika lugha ya KINGEREZA yanasomeka hivi:
"High caffeine content(31.5mg/m100)Taurine(0.03%).Do not Drink More than 2battles per Day, Not suitable for persons Sensitive to Caffeine, Children, Pregnant, Breast feeding women and Avoiding Drinking before sleeping"

‪#‎TAFSIRI‬ YA ‪#‎MANENO‬ HAYA KWA TUSIOJUA!!
Ina kiasi kikubwa cha CAFFEINE, Usinywe zaidi ya chupa 2 kwa siku, Haifai kwa watu wenye matatizo na CAFFEINE, haifai kwa watoto, wajawazito, wana mama wanaonyonyesha na mwisho Usitumie muda mfupi kabla ya kwenda kulala kinywaji hiki.

Kwanini usinywe muda mfupi kabla ujakwenda kulala ?

Kiwango cha 31.5mg/ml100 za caffeine ni nyingi kwa matumizi ya kawaida hivyo kuna hatari ya blood pressure kushuka na ukiwa usingizini na hatimaye ukapoteza maisha hivyo ni hatari kunywa wakati unakwenda kulala, inaathiri ubongo pia. kwa watoto na hata watu wazima. kwa wajawazito, kwa wanaonyonyesha

Sasa Mzee wangu Baresa ni watanzania wangapi wanatumia kinywaji hiki pasipo kujua? kuna wajawazito watoto, wazee wote wanakibugia tu hawajui kinachoendelea katika kinywaji hiki mzee.
Hakuna kinywaji ambacho ni CARBONATED kisichokuwa na CAFFEINE hii inajulikana lakini mzee HIKI KIWANGOCHA (31.5mg/100m) ULICHOWEKA HUMU NI KIKUBWA MNO Sina hakika lakini inawezekana KIKAPITA hata kiwango cha kwenye HEINKEN . CAFFEINE DRIK Kuna baadhi ya nchi kama UFARANSA, MAREKANI, HISPANIA, UINGEREZA WAMEPIGA MARUFUKU Kutokana na athari zake hasa KATIKA UBONGO.
Hakuna shaka Mzee baada ya muda mfupi wa matumizi ya kinywaji hiki WATANZANIA WENGI HASA kina mama na watoto na hata wanaume watapata matatizo haya , MFUMO WA UBONGO kuathirika hili halina shaka , VIDONDA vya tumbo, kwa wana mama wajawazito wanaobugia pia watazaa watoto wenye matatizo hasa AKILI kutokana na Ubongo kuathiliwa, wanaonyonyesha pia, MZEE kama ujumbe huu utakufikia naomba TUONDOLEE JANGA ILI Maana haya matatizo tuliyonayo YANATUSHINDA .

Watanzania wengi wataumia SIKU CHACHE ZIJAZO na hazipo mbali.
#Caffeine ni nini?
Caffeine
Drug
Caffeine is a central nervous system stimulant of the methylxanthine class of psychoactive drugs. It is the world's most widely consumed psychoactive drug, but unlike many other psychoactive substances,
 
Mkuu,naomba unijulishe caffeine kwenye hizo energy drinks nyingine ziko kwa kiasi gani tafadhali
 
Ahsante. Niliitumia siku moja kwa kuijaribu.

Si nzuri.
 
nimekusikia kijana ntastopisha uzalishaji wa hyo kitu kwenye kampuni yangu
 
TBS wako wapi.Kinywaji kinanywewa TZ iweje maelezo yawe kwa kiingereza ? Hii ni shida yitakufa wengi bila kujua.
 
CAFFEINE DRIK Kuna baadhi ya nchi kama UFARANSA, MAREKANI, HISPANIA, UINGEREZA WAMEPIGA MARUFUKU Kutokana na athari zake hasa KATIKA UBONGO.
Coca cola ina caffeine, na hiki kinywaji cha Azam hakina tofauti na Red Bull....ambayo unakosema wamepiga marufuku caffeine drink ndio zinatoka na ni kinywaji maarufu. Kwanini usianze na Red Bull ambayo hapa Tanzania imenywewa miaka na miaka?
 
Angalizo: Energy drinks zote si nzuri kiafya. Zinaweza kuwa chanzo cha kisukari.
 
Red Bull ina 80g/250ml higher than Azam energy drink.
Asante RRONDO,point yangu nilitaka kuianzia hapo kama mwanzilishi wa topic anajifahamu. Katika lita 1 ya red bull utakunywa 320mg ya caffeine,na kwa upande wa azam energy drink katika lita moja hiyo hiyo unakunywa 315mg ya caffeine. Hapo mwenye shida ni red bull. Haya kwenye inshu ya maelekezo,azam kaandika kwa kiingereza vile vile red bull kaandika kwa lugha ile ile. Mbona azam analaumiwa sana kwenye hili kama vile hakuna mamlaka zinazohusika? Thanks mkuu.
 
Energy drink zote dunian Zina maelezo ka hayo ya tahadhari zaid soma maelezo ya shark au ata red bull
 
Mi uzuri wangu..sinywagi hizo takataka..at a kuonja sijawahi.wausika watajijua wenyewe
 
Energy drink zote dunian Zina maelezo ka hayo ya tahadhari zaid soma maelezo ya shark au ata red bull
Asante RRONDO,point yangu nilitaka kuianzia hapo kama mwanzilishi wa topic anajifahamu. Katika lita 1 ya red bull utakunywa 320mg ya caffeine,na kwa upande wa azam energy drink katika lita moja hiyo hiyo unakunywa 315mg ya caffeine. Hapo mwenye shida ni red bull. Haya kwenye inshu ya maelekezo,azam kaandika kwa kiingereza vile vile red bull kaandika kwa lugha ile ile. Mbona azam analaumiwa sana kwenye hili kama vile hakuna mamlaka zinazohusika? Thanks mkuu.
Angalizo: Energy drinks zote si nzuri kiafya. Zinaweza kuwa chanzo cha kisukari.
Muhimu ni kuwafahamisha/kufahamishana hizi energy drinks zote si nzuri kwa afya yetu na si kusema energy drink ya kampuni fulani tu.....
 
Asante RRONDO,point yangu nilitaka kuianzia hapo kama mwanzilishi wa topic anajifahamu. Katika lita 1 ya red bull utakunywa 320mg ya caffeine,na kwa upande wa azam energy drink katika lita moja hiyo hiyo unakunywa 315mg ya caffeine. Hapo mwenye shida ni red bull. Haya kwenye inshu ya maelekezo,azam kaandika kwa kiingereza vile vile red bull kaandika kwa lugha ile ile. Mbona azam analaumiwa sana kwenye hili kama vile hakuna mamlaka zinazohusika? Thanks mkuu.
Nadhani kwenye masuala ya lugha nimtetee kidogo mtoa mada,kwani redbull haizalishwi nchini hivyo ni Sawa wakiandika maandishi ya lugha inamozalishwa,.kwa tz tunahaki yakuandikiwa kwa lugha yetu ambayo inaeleweka ili tujue kilochomo,..kama ni kwa soko la kimataifa basi products ziandikwe kwa lugha zaidi ya moja ikiwemo na lugha mama ya nchi husika.
 
Back
Top Bottom