Tushauriane vifurushi bomba vya internet

Hivi mnaosema tigo ni wezi mnaungia wapi hivyo vifurushi vyenu?? Mi sijaona mtandao nafuu owa internet kama tigo.
Mkuu Univ offer za tigo hazifanani. Wengine wanapewa bundle kubwa, wengine dogo. Mimi nimeshushwa kutoka kwenye kubwa hadi ndogo.
 
Mambo yote iko ttcl sh 1000 gb 4 masaa 24,sh 5000 gb 8 wiki chagua bandika bandua
 
Satellite internet inakuaje .??? Fafanua.
Sasa afafanuwe vipi? Wewe hujui satelite?

Tanzania ipo kampuni inaitwa Thuraya wapo Samora avenue opp na JM Mall inatowa huduma ya satelite phone malipo ni kwa dola, popote ulipo unatumia simu na internet hizi hazitumii minara zinatumia satelite.

Watalii wengi wakija kwenda mbugani hakuna mawasiliano wanazitegemea hizi satelite phone hazinaga mambo ya sijui network imejamba sijui signal weak, that is meaning of Satelite.
 
Hivi unaezaje kutizama kama simu yako inakubali 4g
 
Sawa mkuu subiri Ni wagoogle ili niwafaham vizur
 
Kwani kile cha gb 60 cha voda hukijui?

60 Gb's Hiki kikoje mkuu na bei yake ikoje

mimi natumia cha 10gb's elfu 35,000 kwa mwez speed iko powa sana - Halotel na Airtell ziko too slow nimeachana nazo
 
Tupe menu ya kuunga
 
Umetuacha njia panda mkuu, Tupe maelekezo ya kuunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…