Tushare hizi namba kwa usalama wetu

Tushare hizi namba kwa usalama wetu

dropingcoco

Senior Member
Joined
Jun 21, 2008
Posts
124
Reaction score
11
Wadau nimeona si vibaya kuweka hizi namba hapa, ili kila mmoja atakaependa aweze kuzisave kwenye simu yake kwa ajili ya dharura. Namba hizi ni za jeshi la polisi wa usalama barabarani.

Kutokana na ajali hizi za kila siku ni vema kama watanzania tukashiriki katika kujali usalama wa maisha yetu. Popote pale ulipo au utakapokuwepo katika chombo cha usafiri na ukaona huridhiki na matendo ya dereva, basi piga namba mojawapo au unaweza kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda 0682 887722 au
0713 631780 ili kutoa taarifa.

Kwa pamoja tukishirikiana tunaweza kudhibiti hali hii ya ajali za barabarani.
 
na mkivamiwa na majambazi ama kuona trace passers mnaweza kupiga kwa polisi wa patrol 0713034244. asante kwa kushare nasi mkuu.
 
Hii namba ni kwa watu gani,,namaanisha maeneo gani,au hata kama nipo huku NANGURUKURU ?????
na mkivamiwa na majambazi ama kuona trace passers mnaweza kupiga kwa polisi wa patrol 0713034244. asante kwa kushare nasi mkuu.
 
Wangapi walikwishapata msaada baada ya kupiga simu POLISI?
 
Nimejaribu kizipiga hizo number wakaniambia watanipigia, baada ya muda tena nikapiga wakanitumia ujumbe unaosema Please Recharge me!
 
Kama ni namba za kweli....Tunakushukuru sana mkuu!!!
 
Nimejaribu kizipiga hizo number wakaniambia watanipigia, baada ya muda tena nikapiga wakanitumia ujumbe unaosema Please Recharge me!
Hivi unajua coment yako inashitakika?
 
Wangapi <b>walikwishapata msaada baada ya kupiga</b> simu POLISI?
<br />
<br />
nilishawai kuwapigia wakanitukana matusi ya nguoni..sijui matusi ni moja ya mbinu za kujihami walizopata mafunzoni? Au ni juhud binafsi..
 
Back
Top Bottom