Tuseme ukweli na tusiwapotoshe wananchi

Tuseme ukweli na tusiwapotoshe wananchi

Padre muasi ana shida sana

out of over 20 multimillion dollar scandals in this country, kaamua kushika moja tu??

hivi muda wake huyu babu huwa anautumia kufanya nini kama hata basic journalism inamshinda??
Tatizo umesoma mstari mmoja ukajifanya kuelewa makala nzima. Taja ufisadi wowote ambao hakuna mwanamtandao yeyote aliyenufaika nao.
 
Majenereta ya Richmond? Hivi unafahamu kuwa richmond ni vacuum? Hai exist, ilikuwa ni dili la wajanja kupiga pesa? Ni kampuni hewa, HAIPO, sasa unaposema majenereta ya richmond sijui unamaanisha nini?

ivi Yale yaliyoletwa kwa dege kubwa yalikuwa ya nani?

Dowans na sasa Symbion imetoa wapi majenereta yake

Tuelezane uukweli

Kampuni ya Richmond haikuwa na pesa ya kuendesha mitambo Ile

N Richmond walileta Ile mitambo

Kampuni aliileta Jk baada ya kuonana na Gire marekani alipoenda kwenye ziara yake ya kwanza.

Kosa la lowasa ni kuwa mwadilifu kiasi cha kujiuzulu kwa uzembe uliofanywa na baraza la mawaziri pamoja na Government Negotiations team.Uzembe uliofanyika kumlinda JK.

Na mambo yapi hayo ambayo kamati ya mwakyembe alisema hawatayasema kuinusuru serikali

Tuwe wakweli

Hatuwezi kumtwisha EL zigo la serikali nzima ya CCM
 
viva Lowasa No matter what, unless nafaidika na mfumo wa fisiemu. haiwezekani kuendelea na siasa za kawaida kawaida.
 
Tatizo umesoma mstari mmoja ukajifanya kuelewa makala nzima. Taja ufisadi wowote ambao hakuna mwanamtandao yeyote aliyenufaika nao.

Mtandao mkuu unaotutesa ni CCM.Tusianze kutafuta scapegoat

Wizi wa halmashauri umesahau?

B mkapa ni mwanamtandao?

Magufuli hujui ametuibia katika nyumba za serikali?
 
anapotosha umma kwa kusema Magufuli aliwakamata wezi wa samaki. Ukweli ni kwamba mwisho wa siku wale jamaa walikuwa wanavua kihalali na serikali imeamriwa kuwalipa fidia..hapo haoni kama ameitia hasara serikali..?achilia mbali tuhuma za ubadhirifu fedha za kandarasi zilizoibuliwa na CAG na ile ya kuuza nyumba hapo serikali inaingia gharama kuwwapangishia watumishi nyumba binafsi e.g Kuna waziri mmoja alipangishiwa New Africa Hotel deni mpaka likafika 100M..nadhani aache ushabiki wa kijinga..achia watanzania wenyewe waamue teir destiny..Huyo Magufuli naye has got his skeleton hidden in his closet

Eti 'ukweli?' Hicho ulichokisema ni propaganda za lowasa na kundi lake. Hao 'wezi' wangekuwa na leseni halali iliwezekanaje kusiwe na nyaraka za kumbukumbu ya leseni hiyo wizarani..? Ok, tuseme hiyo wizara ilikuwa mpya sawa; je,kuna rekodi zozote za ulipaji kodi za kampuni hiyo?
 
Mtandao ulizuia asiwe waziri mkuu. Kumbuka hata uwaziri wa ujenzi alitolewa mwanzoni akawekwa kipenzi cha Lowassa Mr. Vijisent Chenge. Baada ya LOwassa kutimuliwa ndipo Chenge nae akaondolewa. Rudisheni fahamu nyie

Na sahv mtandao hauruhusu.
 
Mtandao mkuu unaotutesa ni CCM.Tusianze kutafuta scapegoat

Wizi wa halmashauri umesahau?

B mkapa ni mwanamtandao?

Magufuli hujui ametuibia katika nyumba za serikali?

Wakati nyumba za serikali zinauzwa waziri Mkuu alikuwa Sumaye, sparetyre wa lowasa. Pia ukumbuke muda huo pia nusu ya ranchi za taifa na waziri wa mifugo alikuwa lowasa. Kwa hiyo ukidai nyumba dai na ranchi pia.
 
Eti 'ukweli?' Hicho ulichokisema ni propaganda za lowasa na kundi lake. Hao 'wezi' wangekuwa na leseni halali iliwezekanaje kusiwe na nyaraka za kumbukumbu ya leseni hiyo wizarani..? Ok, tuseme hiyo wizara ilikuwa mpya sawa; je,kuna rekodi zozote za ulipaji kodi za kampuni hiyo?

hivi uvuvi katka zile wanaita international waters inahitaj kulipa kodi..?ndo maana jamaa walishinda kesi cos they were fishing in international water which is not under Tz jurisdiction mkuu
 
privatus karugendo


tunapoelekea uchaguzi mkuu wa 2015, tutayasikia mengi. Na tumeanza kuyasikia na tutaendelea kuyasikia kufikia tarehe yenyewe ya uchaguzi, oktoba 25, 2015. Mengine ya ukweli na mengine ya uongo. Watu wataanza kupakana matope na kuharibiana majina. Kutakuwa na mapambano makali kati ya chama na chama. Vyama vikubwa vinakabana .

Kila mtu anataka ashinde na kila chama kinataka kishinde. Hiyo ndiyo siasa na huo ndiyo ubinadamu. La msingi ni kusema ukweli.tusipindishe mambo. Wezi wa nchi hii wanafahamika, mafisadi wa nchi hii wanafahamika, wazalendo na watu safi wasiohongeka wanafahamika na ni wengi. La msingi ni kuacha siasa za chuki na kumshambulia mtu binafsi. Vile vile ni vyama kutangaza sera na kuyaeleza yale watakayoyafanya wakiingia madarakani.

Maisha ya mtu binafsi, maisha ya familia yake, maisha ya afya yake si suala la kisiasa. Pamoja na uangalifu wa kuzuia kurudia uchaguzi kwa kipindi kifupi, mengine tumwachie mwenyezi mungu, yeye akitaka, tunaweza kuurudia uchaguzi hata mara tatu kwa mwaka. Tuache siasa za uongo na chuki. Siasa hizi za uongo, chuki, umbea na uhasama, zimeanza kujitokeza kwa nguvu.

Tumeweka mambo ya msingi pembeni na kuanza kushughulikia umbea na uhasama. Baadhi ya vyombo vya habari vinavyoaminika vimeanza kupotea njia. Magazeti yanaandika uongo na kueneza chuki. Watu tulioambiwa ni magamba, wakatangazwa na vyombo vya habari kwamba ni mafisadi, leo hii wamesafishwa na watu wale wale walio watangaza. Tunaambiwa wametubu na kusamehewa.

Wametubu wapi? Fedha za richmond zimerudi? Aliyepitisha mkataba huo mbovu amekamatwa na kufikishwa mbele ya sheria? Sifa za edward lowassa, tunazifahamu.

Hata ukirudi nyuma kwenye vyombo vya habari utauona ukweli huo. Leo hii ndiye anapamba magazeti yote. Leo hii ndiye baadhi ya watu wanamtaka awe rais wa tanzania. Huku ni kuupotosha ukweli na kuwapotosha wananchi. Hizi ndizo tunaita siasa za uongo na siasa za hatari.

Tumekuwa tukisikia sifa za dk. John magufuli. Hata ukirudi nyuma na kupekuwa magazeti yote, utakuta magufuli, mchapakazi. Magufuli, anayejenga barabara na kupambana dhidi ya wezi kama alivyoshika meli iliyokuwa ikivua samaki kwenye bahari ya hindi. Leo hii tunaanza kusikia uongo juu yake kwa vile anapambana na mtu mwenye nguvu za kifedha.

Tuseme ukweli na kuacha uongo. Lowassa na magufuli, wamekuwa ndani ya serikali. Ni wazi kwa wagombea urais waliojitokeza, hawa wawili wana nafasi kubwa mmoja wao kutokea mshindi. Sote tunajua utendaji kazi wao. Tukiacha ushabiki wa vyama vyao vya siasa na kulitanguliza taifa letu. Tutakubaliana kwamba sifa za magufuli ziko juu zaidi. Na kama kweli tunayataka mabadiliko, tunayoyalilia, tunalazimika kumchagua magufuli.

Jambo la msingi ambalo tunapaswa kuliangalia kwa makini ili tuhesabike kati ya jamii iliyostaarabika na inayoheshimika duniani ni lazima tufanye siasa zinazozingatia ukweli. Ni jambo la kawaida katika ushindani wa kisiasa watu kutafuta kuangushana, na kila mmoja anataka kushinda, ili ushindi uwe wa amani, ni lazima washindani kueleza ukweli dhidi ya wapinzani wao. Maana kama lengo ni kuijenga tanzania bora, yenye amani na utulivu, hakuna haja ya kuupindisha ukweli. Gharama ya kupindisha ukweli ni kubwa na yenye hasara kuliko faida.

Ni ukweli kwamba lowassa, aliachia ngazi ya uwaziri mkuu, kwa kashifa ya richmond. Hadi ninapoandika makala hii, hatujamsikia akifafanua juu ya suala hili.

Nani alihusika na richmond? Ni ukweli kwamba lowassa, ndiye baba wa mtandao. Mashabiki wake wanatamba kwa hili hadi kusema kwamba mtandao huo, aliouanzisha lowassa na kuendelea kuuratibu ndio ulimwingiza madarakani rais jakaya kikwete.

Mtandao umekivuruga chama cha mapinduzi, mtandao umelivuruga taifa letu. Kama una kitu cha kujutia ni mtandao. Mfumo huu ndio uliozaa “kichaa” cha kila mtu kufikiri anaweza kuwa rais wa nchi, kila mtu anaweza kuwa mbunge. Mtandao umezaa utamaduni mpya wa kutumia fedha kwenye uchaguzi, utamaduni wa kununua kura na kununua shahada za uchaguzi.

Huu ni mfumo mchafu ambao hauwezi kuanzishwa na mtu msafi, mtu wa kuwa na sifa za kuliongoza taifa letu.uchunguzi wa kina unaonyesha magufuli, si sehemu ya mtandao huu, ndiyo maana maadui zake wanasema hana mizizi ngani ya ccm. Kuwa na mizizi ni kuwa kwenye mtandao, na kuwa kwenye makundi. Hivyo huyu ana nafasi ya pekee ya kukiunganisha chama chake na kuliunganisha taifa zaidi ya baba wa mtandao. Huyu ndiye anayefaa kuliongoza taifa letu.

Haya tunayasema bila ushabiki wowote na bila lengo au nia ya kuomba fedha kutoka sehemu yoyote ile. Tunayesema bila kuangalia vyama vya siasa, nguvu na ushawishi wa vya hivi. Tunaangalia uhai wa taifa letu. Tunaiangalia tanzania ya leo na kesho. Huu ni ukweli ambao ni lazima kuusema na ni ukweli utakaotuweka huru.

Hapa tanzania, ukiachia mbali kiti cha rais, nafasi nyingine zinazokuwa na ushindani mkubwa ni ubunge na udiwani. Hizi zote ni nafasi za uwakilishi. Mbunge anawawakilisha watu wa jimbo lake bungeni na diwani anawawakilishia watu wa kata yake kati vikao vya halmashauri ya wilaya. Nafasi hizi zinakuwa na siasa za uongo, chuki, umbea na uhasama.

Ni bahati mbaya kwamba baadhi ya wale wanaochaguliwa kwenye nafasi hizi wanafikiria zaidi juu ya posho kuliko kuuzingatia na kuutafakari wajibu wao wa kuwawakilisha wananchi, wajibu wa kuelezea ukweli, kulinda ukweli na kuusimamia ukweli. Kazi hii ni ngumu kiasi kwamba kama watu wangeifahamu vizuri, ni wachache wangeikimbilia!

Ni bora wananchi wakatambua hili kwamba wanapomtafuta mbunge wa kuwakilisha jimbo lao ni lazima wamtafute mtu mwenye uwezo na karama ya kutetea ukweli na kuusimamia bila kuyumbishwa na vitisho, rushwa, upendeleo au ubinafsi. Bunge ni chombo muhimu katika taifa letu. Katiba inasema:

“sehemu ya pili ya bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha jamhuri ya muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya jamhuri ya muungano na vyombo vyake vyote katitika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii” (ibara 63(2)).

Tumekuwa na utamaduni wa mafiga matatu. Kila chama cha siasa kina kauli mbiu ya mafiga matatu. Utatu mtakatifu wa kura ya rais, mbunge na diwani. Yawezekana ni utamaduni mbaya au mzuri, la msingi ni kuchagua kwa kuzingatia vigezo. Tusichague kwa ushabiki wa vyama vya siasa.

Tuchague kwa kulitanguliza taifa letu la tanzania. Tumchague rais wa kuliongoza taifa letu, rais wa vyama vyote vya siasa, rais wa makabila yote, rais wa waumini wote. Hii ndiyo kazi kubwa iliyo mbele yetu. Ni kazi inayohitaji ukweli zaidi ya upotoshaji

raia mwema

umejitahidi kujieleza sana na kusaidia kuomba kura lakini umesahau wananchi kuelewa ukweli hayo yote unayotaja yamefanyika ndani ya ccm ambao walishindwa kuwachukulia hatua watu hao ya kisheria kwasababu hiyo sisi tumeamua kukiadhibu hicho chama kilichoshindwa kudhibiti hayo yote hatumwadhibu magufuli maana magufuli siyo chama.hapo ndipo mnaposhindwa kuelewa nini kinachoendelea tatizo ni ccm wala siyo mtu na kwaku tatizo ni ccm basi tunaiondoa ccm kwanza.
Ujumbe umeupata bila shida
 
Eti 'ukweli?' Hicho ulichokisema ni propaganda za lowasa na kundi lake. Hao 'wezi' wangekuwa na leseni halali iliwezekanaje kusiwe na nyaraka za kumbukumbu ya leseni hiyo wizarani..? Ok, tuseme hiyo wizara ilikuwa mpya sawa; je,kuna rekodi zozote za ulipaji kodi za kampuni hiyo?

binafsi simtetei Lowassa cos naye has got hell of scandals none of which ametoka in public kukanusha..bt ifke point let us be realistic..watu wanampamba sana Magufuli as if he is a saint while naye ana madudu yake tht is y in my post nikasema let watz waamue wenyewe 25th Oct na sio kujaa humu ndani na Richmond Song
 
Magufuli kwanini hatumii ccm katika kujinadi, anajonadi kwa Tanzania ya magufuli, chagua magufuli anaogopa kutaja ccm. Ndiyol sababu nasi tumeamua kuiadhibu ccm
 
Magufuli kwanini hatumii ccm katika kujinadi, anajonadi kwa Tanzania ya magufuli, chagua magufuli anaogopa kutaja ccm. Ndiyol sababu nasi tumeamua kuiadhibu ccm

Namimi niwaulize swali hilohilo ntangu lina umemsikia mgombea wenu wa urais anasema chagua chadema nabadala yake anasema nipeni kura nyingi alafu mkishapiga kura anataka mseende nyumbani mbaki vituoni
 
Nitachagua ukawa maana najua ndani ya ukawa kuna akina Magufuli zaidi ya 20 wanaenda kuwa mawaziri, kulikoni kuhangaika na huyu Magufuli mmoja ambaye akipita najua mawaziri wake watarajiwa ni Akina Ridhiwani, wasira, Ghasia na wengineo ambao hawawezi kuja na jipya
 
Wakati nyumba za serikali zinauzwa waziri Mkuu alikuwa Sumaye, sparetyre wa lowasa. Pia ukumbuke muda huo pia nusu ya ranchi za taifa na waziri wa mifugo alikuwa lowasa. Kwa hiyo ukidai nyumba dai na ranchi pia.
Ndio maana nakwambia tatizo ni CCM

Ndio maana hata bada ya wao kundoka yamefanyika mengi ya kuogofya chini ya CCM
 
Ndani ya ccm hakuna msafi, wote ni watu wa madeal, hata nape akitoka leo akaenda chama kingine mtasikia uchafu wake, na huu uchafu ndani ya chama utaendelea milele na milele amina kwani wao wako juu ya sheria na miungu watu, utaona baraza la mawaziri la ccm litakuwa ni wale wale, tukandamizeni tu manake tumechoka sasa na hakuna namna
 
Ccm mmesomba watu na malori kutoka wilaya mbali mbali huko dom na kuwaahidi kuwapa posho, na kuwazuia wasitoke ndani ya uwanja baada ya burudani za bongo flava kwisha hatimae tunawaona dom wanazunguka zunguka dom kwani malori yaliyowasomba yamesepa na kuwaacha wanazurura ovyo kama headless chicken
 
Muleta Mada wewe ndiye unapotosha watu unasema mkataba wa Richmond ulisainiwa na Lowasa!! Huo ni uongo. Tafuta ukweli ujuwe ni nani alisaini huo mkataba.
 
Mwinyi, Mkapa, Kikwete ni wezi na mafisadi waliotukuka. Watafanya chini juu kuwadanganya watanzania ili tu Ukawa isishinde ashinde Makufuri ili awalindie maslahi yao. Na kama Makufuri atashinda basi naye atakuja na staili yake ya wizi huku akitetea viongozi waliopita chini ya CCM. Inabidi nchi ichukuliwe na Ukawa na hawa mafisadi wakamatwe na kunyongwa pia ikiwa watabainika which I am 100% sure kuwa watabainika tu. Kina Mwinyi wanahofia kunyongwa, hawana lolote. Watanzania hamkeni tuwamalize viongozi wezi ili iwe fundisho kwa wengine wajao.
 
Back
Top Bottom