Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,266
- 2,870
Miaka ya 80 mwishoni na 90 mkoa wa Mbeya kulikuwa na Jambazi mmoja maarufu sana alikuwa anafahamika kwa jina la Jombi. Alikuwa maarufu na tajiri. Yeye alikuwa na mtandao mkubwa sana na inasemekana Polisi wengi wakubwa walikuwa kwnye payroll yake kwa njia moja au nyingine pamoja na wanasiasa. Huyu bwana alikuwa akiiba magari TZ anaenda kuuza SA au Zambia na akiiba huko analeta TZ.
Pia alikuwa akifanya Ujambazi mwingine wa humu humu ndani kwa umakini mkubwa sana. Ilikuwa ikitokea anatakiwa akamatwe kuhojiwa anapigiwa simu aende kituoni au anaambiwa kesho kuna vijana wanakuja. So anajiandaa anavyojua. Siku mbili tatu mnamwona mtaani anadunda kama kawaida. Ni Mkapa alikuja kumkamata huyu mweshimiwa Jambazi.
Nimerudia habari hiyo kwa kufananisha na kile kinachoendelea hapa nchini. Kusema wauza madawa wa kulevya wakubwa hawafahamiki ni uongo mkubwa na utatupeleka motoni. Wanafahamika sana wengine ni watoto wa viongozi na viongoz wenyewe, wengine ni wabunge na makada wa vyama vyetu, wengine ni wafadhili wakubwa wa vyama na timu zetu, wafadhili wa wanamuziki, wasanii na wenye kufadhili hata maisha ya watu flan flan hapa mjini.
Wanafahamika sana. Nenda Kinondoni kuna himaya za watu hawa. Nenda Mbezi, nenda kaangalie watoto wanaosoma chuo cha diplomasia wanavyoharibika kwa madawa haya.
Kama Makonda ameamua kupambana na madawa ya kulevya atoe namba yake ya simu apewe majina. Lakini hilo si issue sana anaweza enda omba kwa ndugu Kikwete, yeye anayo list ambayo alisema hadi viongozi wa dini wapo na watu wengine wengine aliosema ni wazito. Yaani walikuwa wanaogopwa kuliko serikali. Hayo majina sidhan kama Kikwete atamnyima.
Lakini ikiwa Kikwete hatotaka kumpa basi sisi vijana tunaweza msaidia akipewa hayo majina hatusemi aje atangaze. Hapana tunaomba afanye uchunguzi ili tusije nasi wengine tukawa tumewasingizia. Awakabidhi polisi kitengo husika, polisi waadilifu wachunguze na kuwakamata wahusika.
Wanafahamika wala si siri. Wengine bado ni wabunge na wengine wanajihusisha na music, usanii au ufadhili wa vyama vyetu.
Makonda tupatie namba yako ndugu, tukusaidie kukutajia wahusika wakuu ukiacha hawa uliowataka waje kukuona ofisini. Sisemi waachwe ila nashangaa kwa nini ulipendelea waje kukona wewe ofisini? Ili iweje? Si ungesema wakamatwe? Wapelekwe polisi? Na halafu mahakamani?
Watanzania tusimung'unye maneno. Tusipepese macho, tusing'ate kucha na kutizama chini.
Tuseme Makonda haya hapa majina ya wauza madawa ya kulevya ili Mungu alinusuru Taifa hili na madhambi yanayolizunguka.