Tuseme: Makonda, Haya hapa Majina ya Wauzaji Madawa ya Kulevya wakubwa

Hapa tunapiga kelele tu makonda mwenyewe anajua hii ngoma si ya kitoto.

Na kingine naamin hata yeye anawafahamu vizuri tu.

Kwa siasa za bongo zilivyo huenda hata bungeni kuna kitu fulani na wanahamisha mawazo ya watu.
Umeaema kweli wanahamisha mawazo ya watu kutoka Dodoma issue ya njaa inayoendelea na matokeo form four
 
Kuna siku niliandika uzi hapa naona makonda aliusoma sasa namwagiza aende mtaa waufipa tena
tena bila kuchoka atawakamata mapapa wengi sana. Sii wasanii tu hadi makada wa CCM. Nao wapo wanakuja na magari ya kifahari.
[URL="https://www.jamiiforums.com/threads/dawa-za-kulevya-ni-janga-la-kitaifa-mungu-wanusuru-watoto-wetu-wa-kike.1176584/#post-19130702"]Dawa za kulevya ni janga la kitaifa, Mungu wanusuru watoto wetu wa kikehttps://www.jamiiforums.com/threads/dawa-za-kulevya-ni-janga-la-kitaifa-mungu-wanusuru-watoto-wetu-wa-kike.1176584/#post-19130702[/URL]
 
Ufipa mwanzo na ufipa mwisho.....ndy Kna wauza mitkas.....miaka ya nyuma nmekaa sana huo mtaa in short nmekulia hapo....kulikuwa na maskani kubwa ya wsuza unga wakati huo watu wanaenda kufata Mzigo Pakistan na Iran kwa kuleta kwa njiaa ya kumeza...
Hyo sehemu mtaani kuanzia asubuhi mpaka Huoni ni nyomi tu la watu kuanzia wauzaji hadi MATEJA.
Ila sjui kama kwa sasa atawapata wauzaji pale maana wengi wao watakuwa wamekimbiaa...
Ufipa,wibu,sekenke kote huko Kna mapusha

Ova
 
Ufipa mwanzo na ufipa mwisho.....ndy Kna wauza mitkas.....miaka ya nyuma nmekaa sana huo mtaa in short nmekulia hapo....kulikuwa na maskani kubwa ya wsuza unga wakati huo watu wanaenda kufata Mzigo Pakistan na Iran kwa kuleta kwa njiaa ya kumeza...
Hyo sehemu mtaani kuanzia asubuhi mpaka Huoni ni nyomi tu la watu kuanzia wauzaji hadi MATEJA.
Ila sjui kama kwa sasa atawapata wauzaji pale maana wengi wao watakuwa wamekimbiaa...
Ufipa,wibu,sekenke kote huko Kna mapusha

Ova


Ndo maana kumbe chadema wakafungua ofisi hapo? Sasa naanza kuunganisha dots!
 
Ndo maana kumbe chadema wakafungua ofisi hapo? Sasa naanza kuunganisha dots!
Aisee !!!
ae3e209e93a814574e0232a7f2f40e61.jpg
 
Ndo maana kumbe chadema wakafungua ofisi hapo? Sasa naanza kuunganisha dots!
Chadema ilikuja baada Kadi ya uzaji madawa pale kuisha......sahv mtaa ufipa ni sehemu chache tu wanauza sembe....
Unga ulipungua uzwa ufipa baada ya nyumba kuuzwa za urithi wenyeji kuondoka na kuja wageni....ufipa sahv syo kama zamani...
Bado mitaa inayouza sembe ili Mbali na ufipa
Hata pale amerikan chips zamani karibu na duka la maimartha unga ulikuwa inauzwa na karangaaa makini baada ya nyumba kuuzwa nawatu kujenga zaidi frame za biashara wauzaji wakawa wanapunguaaa...ndy hvyo

OvA
 
Asisahau na hili la shule za Dar kuongoza katika kufeli kidato cha nne 2016, wana Dar wanataka majibu kutoka kwake...
 

Attachments

  • SHULE ZA MWISHO 2016.jpg
    SHULE ZA MWISHO 2016.jpg
    40.9 KB · Views: 73
Asisahau na hili la shule za Dar kuongoza katika kufeli kidato cha nne 2016, wana Dar wanataka majibu kutoka kwake...
kaamua kulipotezea hili kiana, kaona atoke ishu ya madawa na kuwasahaulisha wana dsm jinsi elimu ilivyodorora mkoani kwake. Na nnakumbuka kuna kauli za vitisho alizotoa akiwa Jitegemee mahafari ya kidato cha nne mwaka jana dhidi ya walimu wakuu watakaofelisha, je alikumbuki hilo analipotezea au ulikua unafikii tu!!
 
Tatizo sio wananchi bali ni vyombo vya usalama na serikali kiujumla. Kama unabisha kaa kijiweni au kwenye mitandao halafu kiseme vibaya chama tawala au mseme vibaya Rais nafikiri hutachukua muda utaisoma namba. Hawa wauza unga wemesemwa sana na wanawafahamu lakini kwasababu wanazozijua wenyewe hawachukui hatua.
Umeongea jambo la kweli kabisa. Hicho kitengo cha kushughulika na udhibiti wa dawa za kulevya naona hakina nia ya dhati kuifanya kazi hiyo. Matokeo yake Mkuu wa Mkoa ameamua kuingilia na kufanya mambo "yasiyomhusu"
 
Miaka ya 80 mwishoni na 90 mkoa wa Mbeya kulikuwa na Jambazi mmoja maarufu sana alikuwa anafahamika kwa jina la Jombi. Alikuwa maarufu na tajiri. Yeye alikuwa na mtandao mkubwa sana na inasemekana Polisi wengi wakubwa walikuwa kwnye payroll yake kwa njia moja au nyingine pamoja na wanasiasa. Huyu bwana alikuwa akiiba magari TZ anaenda kuuza SA au Zambia na akiiba huko analeta TZ.

Pia alikuwa akifanya Ujambazi mwingine wa humu humu ndani kwa umakini mkubwa sana. Ilikuwa ikitokea anatakiwa akamatwe kuhojiwa anapigiwa simu aende kituoni au anaambiwa kesho kuna vijana wanakuja. So anajiandaa anavyojua. Siku mbili tatu mnamwona mtaani anadunda kama kawaida. Ni Mkapa alikuja kumkamata huyu mweshimiwa Jambazi.

Nimerudia habari hiyo kwa kufananisha na kile kinachoendelea hapa nchini. Kusema wauza madawa wa kulevya wakubwa hawafahamiki ni uongo mkubwa na utatupeleka motoni. Wanafahamika sana wengine ni watoto wa viongozi na viongoz wenyewe, wengine ni wabunge na makada wa vyama vyetu, wengine ni wafadhili wakubwa wa vyama na timu zetu, wafadhili wa wanamuziki, wasanii na wenye kufadhili hata maisha ya watu flan flan hapa mjini.

Wanafahamika sana. Nenda Kinondoni kuna himaya za watu hawa. Nenda Mbezi, nenda kaangalie watoto wanaosoma chuo cha diplomasia wanavyoharibika kwa madawa haya.

Kama Makonda ameamua kupambana na madawa ya kulevya atoe namba yake ya simu apewe majina. Lakini hilo si issue sana anaweza enda omba kwa ndugu Kikwete, yeye anayo list ambayo alisema hadi viongozi wa dini wapo na watu wengine wengine aliosema ni wazito. Yaani walikuwa wanaogopwa kuliko serikali. Hayo majina sidhan kama Kikwete atamnyima.

Lakini ikiwa Kikwete hatotaka kumpa basi sisi vijana tunaweza msaidia akipewa hayo majina hatusemi aje atangaze. Hapana tunaomba afanye uchunguzi ili tusije nasi wengine tukawa tumewasingizia. Awakabidhi polisi kitengo husika, polisi waadilifu wachunguze na kuwakamata wahusika.

Wanafahamika wala si siri. Wengine bado ni wabunge na wengine wanajihusisha na music, usanii au ufadhili wa vyama vyetu.

Makonda tupatie namba yako ndugu, tukusaidie kukutajia wahusika wakuu ukiacha hawa uliowataka waje kukuona ofisini. Sisemi waachwe ila nashangaa kwa nini ulipendelea waje kukona wewe ofisini? Ili iweje? Si ungesema wakamatwe? Wapelekwe polisi? Na halafu mahakamani?

Watanzania tusimung'unye maneno. Tusipepese macho, tusing'ate kucha na kutizama chini.

Tuseme Makonda haya hapa majina ya wauza madawa ya kulevya ili Mungu alinusuru Taifa hili na madhambi yanayolizunguka.
Aseee!! bei ya SEMBE sasa haikamatiki duh!!
 
Back
Top Bottom