Kwanza,
Ukifatilia kwa makini tatizo la ajira kwa sasa sio mtaji kama linavozungumzwa na vijana wengi.
Personality ya vijana imekua ya hovyo sana humu kwenye jamii yetu tunayoishi.
Mtu anayewekeza pesa yake,
lazima ajiridhishe kwanza pesa yake iko sehemu salama.
Unamwangalia kijana kuanzia uvaaji wake, unyoaji wake, uongeaji wake, nidhamu yake kwa jamii unajua kabisa hapa nitapoteza tu pesa zangu bure bora nikanywe BIA.
Kijana unapewa kiroba cha unga upeleke nyumbani, unakwapua kilo 2 ukauze ununue bando.
Kijana unatumwa dukani vitu, unazidisha jero jero juu ya bei husika ya vitu.
Kijana unatumwa ukamtafutie boss chumba lodge, unampiga ya udalali
Kijana unapewa gari ukajaze mafuta la laki 2, unaweka ya 190,000
Nataka kuwaambia vijana,
PERSONALITY yako (UAMINIFU WAKO) ni mtaji mkubwa sana ambao ukiutumia vizur unaweza kufika mbali.