Tusaidie Vijana wenzetu wenye plans za biashara lakini wanakosa mtaji

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
16,887
2,000
Hili tatizo la ajira,
hasa kwa wasomi limekuzwa kuliko uhalisia.

Vijana wasomi wamekua na deko sana wakilazimisha waziishi ndoto zao, bila kuangalia hali halisi ya soko la ajira kwa wakati tulionao sasa.

Catoni ya maji ya lita 1.5 inauzwa 3,100 zinakaa chupa 6.
Ukiuza rejareja kwa 1,000 utapata 6,000
Maana ake faida ni 2,900 kwa kila catoni.

Kwa msimu huu wa joto,
Ukiuza catoni 3 (chupa 18) unauhakika wakuingiza 8,700 kama faida.

Ukitoa matumizi ya friji, ushuru n.k, mfano 2700. Unauhakika wa kubakiwa na 6,000 cash.

Hiyo ela 6,000/=
Ni posho inayotosha kuilisha familia nzima ya watu 5 kuanzia asbuh chai, chakula cha mchana na chakula cha jioni.
(Wakishua hawawezi kuamini)

Sasa unakuta,
Kijana analalamika tatizo mtaji,
Ila ukiangalia ilo wazo nlotoa apo juu mtaji wake hauzidi sh. 10,000.
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
16,887
2,000
Biashara nyingi za uku mitaani tunakoishi mitaji yake haizidi elfu 50.

Ukienda sokoni,
Kuna vigenge vingi vinamitaji isiyozidi elfu 20.

Wamama na wababa wanavitumia kulisha na kusomesha familia kabisa.

Ila kijana msomi,
Anaemiliki simu ya laki 5, anakuja sema tatizo ni mtaji.

Kisa tu,
Lengo lake akafanye biashara za mamilioni alizokua akiandikia project uko vyuoni kwake.

Nnachoshauri,
Vijana msibague kazi. Chapeni kazi.

Kama lengo ni ujasiliamali,
Anza na huo huo mtaji wa elfu 10, utakuja tu kufika kwenye hayo mamilioni unayowaza.

Kung'ang'ania uanze na mamilioni wakati hata visheti ujawai uza ni upuuz na kujiletea tu msongo wa mawazo.
 
Lenie

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
4,793

Ushauri murua huu👏
Watu wanatakiwa wafanye kile ambacho kipo ndani ya uwezo wao na sio kuforce mambo makubwa pia ifahamike biashara kubwa inahitaji akili kubwa na umakini zaidi so inabidi kufanya maamuz sahihi ili mambo yasiende ndivyo sivyo ukala hasara
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
16,887
2,000
Ilo la kuchangiana PESA KUANZISHA PROJECT ni upuuzi mwingine pia,
Mtakuja kufeli kisha mwende kulogana na kuanza kuitana matapeli humu.

Kumbe mwezio kaingia kwenye project kichwa kichwa, hana uzoefu na anachokifanya. project imekufa kibudu.

Hata kwenye mabenki hawawezi kumkopesha mtu anayekwenda kuanza biashara.
Mkopo ni kwa ajili ya miradi endelevu.

Nnachomaanisha,
Sio kuwakatisha tamaa vijana.

Nnachosistiza,
Vijana waanze na icho icho kidogo walichonacho.
Wataonekana na wanabustiwa kutoka pale wakikofikia kwa juhudi zao wenyewe.

Kiukweli,
Kudhamini project inayoanza, Ni kama kugamble (kucheza kamari).

Tena hasa kama mwendeshaji mwenyewe hana uzoefu wa anachokifanya zaidi ya nadharia tu za madarasani anazokwambia alifundishwa na maprofesa wake uko vyuoni.
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
16,887
2,000
Kwanza,
Ukifatilia kwa makini tatizo la ajira kwa sasa sio mtaji kama linavozungumzwa na vijana wengi.

Personality ya vijana imekua ya hovyo sana humu kwenye jamii yetu tunayoishi.

Mtu anayewekeza pesa yake,
lazima ajiridhishe kwanza pesa yake iko sehemu salama.

Unamwangalia kijana kuanzia uvaaji wake, unyoaji wake, uongeaji wake, nidhamu yake kwa jamii unajua kabisa hapa nitapoteza tu pesa zangu bure bora nikanywe BIA.

Kijana unapewa kiroba cha unga upeleke nyumbani, unakwapua kilo 2 ukauze ununue bando.
Kijana unatumwa dukani vitu, unazidisha jero jero juu ya bei husika ya vitu.
Kijana unatumwa ukamtafutie boss chumba lodge, unampiga ya udalali
Kijana unapewa gari ukajaze mafuta la laki 2, unaweka ya 190,000

Nataka kuwaambia vijana,
PERSONALITY yako (UAMINIFU WAKO) ni mtaji mkubwa sana ambao ukiutumia vizur unaweza kufika mbali.
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
16,887
2,000
Tatizo kubwa Vijana wengi hatuna uaminifu
Na hatujui kama uaminifu ni mtaji mkubwa wa kwanza.!
Kabisa,
Kuna vijana wengi sana waaminifu wamekabidhiwa ofsi kubwa kubwa kuziendesha.

Hii ni kutokana na uaminifu walokua nao
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
16,887
2,000
Ushauri murua huu
Watu wanatakiwa wafanye kile ambacho kipo ndani ya uwezo wao na sio kuforce mambo makubwa pia ifahamike biashara kubwa inahitaji akili kubwa na umakini zaidi so inabidi kufanya maamuz sahihi ili mambo yasiende ndivyo sivyo ukala hasara
Vijana wengi wanatamani waanzie pakubwa.

Hawataki kabisa kuanza chini.
 
Mashaurijr

Senior Member
Oct 8, 2016
111
250
Mkuu mambo vp. Nilikuwa na maduka ya rejareja mawili . Moja nikaliuwa kutokana na kuugua , na changamoto za Mmiliki wa fremu, by laws za ulinzi , kuharibu kwa mfanyakazi, nikawa nimetaka kubadili biashara na fremu nilikuwa nishapata ila mwenye fremu nilimpa idea yangu nini nataka nifanye hapo , siku ya kulipia kufika nikakuta kaiba plan yangu , nilipanik nikawa nimepeleka hela kwenye ujenzi ambao haukwenda mbali nikajishtukia nimedondokea kwenye hali ngumu sana kiuchumi depression inanitafuna afya inakaa vibaya duka lililobaki lina mtaji unaozunguka 6.7M ila lina mfanyakazi anafanya vizuri sana wateja wamemzoea na anajituma sana, kiasi kwamba nakuwa na mashaka ukimtoa lazima duka liyumbe kwanza kutokana na kuzoeleka kwake na uwezo wake kwenye competition, sasa nipo tu sina ishu yoyote nikitegemea tena duka kuishi hilo moja jambo nisilolipenda natamani kuajiriwa angalau faida ninayozalisha dukani ikae benki nije nifungue biashara nyingine na sio mimi kuitumia
Na pia sijazoea kukaa free nimepona sasa natamani kazi yoyote ile itakayonipa kula na matumizi mengine, nakusave hata kidogo ili niweze kurudi kwenye hali yangu kiuchumi nahitaji nitoke dar mwenye nafasi yoyote ya kazi mimi ni mpambanaji huwa sijali ndio maana siwezi kukaa bila kazi . Naugua nikikaa hivi 0757257810
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom