Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,956
Habari za jumapili wangu.
Naomba Tusaidiane mawazo ni kwa namna gani tunaweza kuwapatanisha ndugu hawa wadamu.
Nina rafiki yangu ambaye katika familia yao wamezaliwa wanne na yeye akiwa wa mwisho kuzaliwa.sasa kaka yake ambaye ni mzaliwa wa kwanza katika familia yao, kipindi cha nyuma wakati huyu rafiki yangu akiwa bado mdogo kakayake alikuwa na mahusiano na dadammoja na hata huyu rafiki yangu alibahatika kumfahamu lakini wazazi hawakuwa wakitambua lolote lile. Baadae kakamtu akatengana na yule dada kipindi ambacho akiwa tayari ni mjamzito, yule dada hakwenda kwa wazazi kulalamika na hatahivyo walikuwa hamtambui.
Kaka mtu akakataa ujauzito huo hivyo yeye akaendelea na maisha yake na yule dada akabaki mwenyewe hadi akajifungua bila kaka kufahamu. Kipindi hicho ilikuwa 2005. Sasa miaka mitatu iliyopita huyu rafiki yangu alibahatika kukutana na shemej yake ambaye kwa sasa anaishi miono, baada ya kukutana alimfahamisha kuwa mtoto wa kakayake aliyemtelekeza yupo. Alishangaa kusikia kuna mtoto wao kwasababu yeye hakujua kama yule dada alikuwa na mimba ya kakayake. Alipojaribu kumwambia kakamtu ambaye kwa sasa ni MCHUNGAJI akakataa kwa kusema yule mtoto sio wake na yeye kwa sasa ana mke na watoto wawili. Rafiki yangu hakukubaliana na kakayake, akalipeleka kwa wazazi na hata wazazi walipowaweka kikao bado kaka alikataa.
Jamaa yangu akaamua kuwaomba wazazi wakaongee na familia ya yule dada ili aluhusiwe yeye kumtunza yule mtoto kwa hakuna ubishi kwamba mtoto ni kweli kabisa ni wakakayake.
Wazazi wakafanikisha hilo na jamaa akapokea rasmi jukumu la kumlea mtoto wa kakayake.
Sasa tatizo likaja kwa upande wa kakayake kwamba anamgombeza mdogo mtu kwa kumchukua yule mtoto. Ugomvi umekuwa mkubwa hidi kufikia hatua ya kaka kumtamkia mdogowake kuwa hana undugu nae wazazi wamejitahidi kuwasuluhisha lakini bado hakuna muafaka wowote wa maana mpaka sasa.
Kwa kweli bado hatuelewi lengo hasa la huyu kaka ni nini, sijui anataka mtoto huyu aishije.
Je nini kifanyike hapa kutatua tatizo hili? Nawasilisha kwenu.